Tetesi za Soka Ulaya: Man City yaongoza mbio za kumnasa Bouaddi

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Manchester City ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na Lille kuhusu kiungo wa Morocco mwenye umri wa miaka 18 Ayyoub Bouaddi, ambaye pia anawindwa na Arsenal, Chelsea, Liverpool na Bayern Munich. (Talksport)
Everton, Leeds United na Nottingham Forest zinafuatilia hali ya mshambuliaji wa England Liam Delap, 23, ambaye Chelsea inasema thamani yake ni pauni milioni 40. (The i)
Kiungo wa Mali Mamadou Sangare, 24, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kwenda Brentford, baada ya kuondoka kwenye kambi ya maandalizi ya msimu ya Lens nchini Italia. (L'Equipe)
Fulham imekubaliana na Real Madrid kuwasajili mshambuliaji wa Hispania Gonzalo Garcia, 22, na kiungo Cesar Palacios, 21, kwa ada ya pamoja ya pauni milioni 43. (The Athletic)
Manchester City inamfikiria kipa wa Marseille na Argentina Geronimo Rulli, 34, kuwa mbadala wa James Trafford. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United inaandaa ofa kwa beki wa Newcastle United na England Lewis Hall, 21, huku beki wa Racing Santander mwenye umri wa miaka 19 Jorge Salinas akiwa chaguo mbadala. (Teamtalk)
Coventry City iko hatua za mwisho kukubaliana na Brighton kuhusu usajili wa kipa wa England Carl Rushworth, 25, ambaye alicheza kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita. (Sky Sports)
Hull City imefanya mazungumzo yanayoonekana kuwa mazuri na kiungo wa Augsburg Mert Komur, 21, kutoka Ujerumani. (Florian Plettenberg on X)
Manchester United imefanya mazungumzo kuhusu kumsajili kipa wa San Lorenzo na Paraguay Orlando Gill, 26, kwa mujibu wa wakala wake. (DSports, via Metro)
Beki wa Sweden mwenye umri wa miaka 19 Genesis Antwi anatarajiwa kujiunga na klabu dada ya Chelsea, Strasbourg, kwa mkopo. (Football Insider)














