Moja kwa moja, Hamas yakubali kuweka silaha chini Gaza; Trump kutangaza mpango wa Bodi ya Amani

Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuweka silaha chini kabisa katika Ukanda wa Gaza.

Muhtasari

Ruka Video uendelee
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote
  • xx
  • Lydia Wanjiku

Moja kwa moja

Na Asha Juma & Ambia Hirsi

  1. Kwa picha: Hali ilivyo Gaza huku mashambulizi ya Israel yakiendelea

    Wakati Donald Trump akisema kuwa makubaliano yamefikiwa ya "kuwapokonya silaha" wanamgambo ya kundi la Hamas mjini Gaza, mashambulizi ya Israel yanaendelea.

    Wapalestina kadhaa walijeruhiwa katika shambulio la anga dhidi ya Gaza mapema leo, kulingana na Shirika la Habari la Reuters.

    Picha hizi, zilizopigwa hivi karibuni, zinaonyeshahali ya maisja maisha yalivyo kwa wale wanaoishi katika eneo la vita.

    Mahema ya muda ni makazi ya watoto na familia zao katika maeneo makubwa ya Gaza.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Moshi na miali ya moto baada ya shambulio la anga la Israel dhidi ya msikiti mmoja katika Jiji la Gaza siku ya Jumanne.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Moshi na miali ya moto baada ya shambulio la anga la Israel dhidi ya msikiti mmoja katika Jiji la Gaza siku ya Jumanne.
    Mwanamke anakagua nyumba yake ilivyoharibiwa baada ya shambulio la Israel mapema wiki hii.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwanamke anakagua nyumba yake ilivyoharibiwa baada ya shambulio la Israel mapema wiki hii.
    Msikiti mmoja katika Jiji la Gaza umeharibiwa vibaya baada ya kushambuliwa na jeshi la Israel siku ya Jumanne, katika shambulio ambalo kulikuwa na onyo la awali.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mwanamume anaandaa chakula ndani ya hema katika kambi moja jijini Gaza siku ya Jumapili.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Mwanamume anaandaa chakula ndani ya hema katika kambi moja jijini Gaza siku ya Jumapili.
  2. Israel yafanya shambulio jipya dhidi ya Gaza - Ripoti

    Eneo la shambulio la Israel katika Jiji la Gaza siku ya Alhamisi, tarehe 30 Julai.

    Chanzo cha picha, Reuters

    Israel imeripotiwa kufanya shambulio jipya dhidi ya Gaza, saa chache baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kufikiwa kwa makubaliano ya kuipokonya silaha Hamas, katika hatua ambayo ingepelekea majeshi ya Israel kuondoka.

    Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa Wapalestina kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio hilo, likinukuu maafisa wa afya wa Gaza.

    Wakati huo huo, Al Jazeera imeripoti shambulio karibu na msikiti katika eneo la Karama, kaskazini mwa Jiji la Gaza.

    Jeshi la Israel (IDF) limeiambia BBC kuwa linachunguza tukio hilo - tutatoa taarifa zaidi pindi tutakapopata habari zaidi.

    Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na Hamas, takribani Wapalestina 1,168 wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas yalipoanza kutekelezwa Oktoba mwaka jana.

    Wanajeshi wanne wa Israel wameuawa katika mashambulizi ya Wapalestina mjini Gaza katika kipindi hicho hicho.

  3. Israel imeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya Gaza tangu makubaliano yafikiwe

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Katika kipindi cha miezi sita tangu Israel na Hamas walipotarajiwa kuanza awamu ya pili ya makubaliano ya usitishaji vita, hatua zilizopigwa zimekuwa chache sana.

    Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas, takriban Wapalestina 1,168 wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu usitishaji vita kati ya Israel na Hamas ulipoanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka jana.

    Takwimu za wizara hiyo zinachukuliwa kuwa za kuaminika na Umoja wa Mataifa (UN).

    Katika kipindi hicho hicho, wanajeshi wanne wa Israel wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Wapalestina ndani ya Gaza.

    Mnamo tarehe 7 Oktoba 2023, Hamas iliongoza shambulio dhidi ya Israel ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,200, huku watu 251 wakichukuliwa mateka.

    Israel ilijibu kwa kuanzisha operesheni kubwa ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas, zaidi ya watu 73,290 wameuawa wakati wa kampeni hiyo ya kijeshi, wakiwemo watoto 21,280.

    Mnamo mwaka 2024, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, na waziri wa zamani wa ulinzi, Yoav Gallant, pamoja na kamanda wa kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif.

    Israel imesema kwamba Mohammed Deif aliuawa katika shambulio la anga, ingawa taarifa hiyo imekuwa ikijadiliwa na pande mbalimbali kuhusu uthibitisho wake.

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alilaani uamuzi wa ICC akiuita "wa chuki dhidi ya Wayahudi (antisemitic)", huku Hamas ikisema kwamba hati za kukamatwa zilizotolewa dhidi ya Netanyahu na Gallant zimeweka "mfano muhimu wa kihistoria" katika suala la uwajibikaji wa kimataifa.

    Mnamo mwezi Septemba 2025, tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa (UN) ilisema kwamba Israel ilikuwa imefanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

    Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ilikanusha vikali ripoti hiyo, ikiielezea kuwa "imepotoshwa na ni ya uongo".

  4. Uhispania yatuma wanajeshi huku maelfu wakiingia Ceuta kutoka Morocco

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Uhispania imetuma wanajeshi kuimarisha usalama katika eneo lake la Ceuta, lililoko Afrika Kaskazini, baada ya maelfu ya wahamiaji kuogelea kutoka Morocco na kuingia katika eneo hilo siku ya Alhamisi.

    Takriban watu 15 walifariki dunia kwa kuzama maji walipokuwa wakijaribu kufika Ceuta. Maafisa wa eneo hilo walikuwa tayari wameiomba serikali ya Madrid kutoa msaada kutokana na kuongezeka kwa majaribio ya kuvuka mpaka katika siku za hivi karibuni, lakini hali iligeuka kuwa ya vurugu siku ya Alhamisi wakati udhibiti wa mipaka ulionekana kuvurugika.

    Mapema mwezi huo, Mahakama Kuu ya Uhispania iliamua kwamba wahamiaji wanaozuiliwa baharini wakiwa wanajaribu kufika Ceuta au Melilla, eneo lingine la Uhispania lililoko Afrika Kaskazini, hawawezi kurejeshwa mara moja nchini Morocco bila kufuata taratibu za kisheria zinazostahili.

    Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania ilizishutumu mitandao ya usafirishaji haramu wa watu kwa kutumia hali hiyo "kuhamasisha ongezeko la wahamiaji wasio na nyaraka za kisheria."

    "Vikosi vya ulinzi vitaimarisha usaidizi kwa Kikosi cha Walinzi wa Mpaka (Civil Guard) katika kutekeleza majukumu yake na hatua nyingine zozote zitakazohitajika ili kudumisha usalama katika mji wa Ceuta," wizara hiyo ilisema.

    Ceuta, iliyoko katika pwani ya kaskazini ya Morocco, imetenganishwa na bara la Uhispania na Mlango wa Gibraltar na kwa muda mrefu imekuwa mojawapo ya maeneo muhimu yanayolengwa na wahamiaji wanaojaribu kufika barani Ulaya.

    Soma Zaidi:

  5. Ghana yaunga mkono muhula wa miaka mitano kwa Rais

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Serikali ya Ghana imekubali pendekezo la kuongeza muda wa muhula wa urais kutoka miaka minne hadi miaka mitano, Waziri wa Sheria wa taifa hilo la Afrika Magharibi amesema siku ya Alhamisi.

    Rais John Dramani Mahama aliunda kamati mwaka jana kupitia upya Katiba ya mwaka 1992 na kutoa mapendekezo mbalimbali, ambayo baadhi yake yamekubaliwa na serikali.

    Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria, Dominic Ayine, alisema kuwa muhula wa Bunge pia utaongezwa ili uendane na muhula mpya wa rais wa miaka mitano.

    Aidha, serikali imeunga mkono pendekezo la kupunguza umri wa chini wa kugombea urais kutoka miaka 40 hadi miaka 35, hatua inayolenga kutoa nafasi kubwa zaidi kwa viongozi vijana kushiriki katika uongozi wa taifa.

    Serikali pia imekubali kimsingi pendekezo la kamati la kupunguza umri wa chini wa wagombea urais, ambao kwa sasa ni miaka 40. Hata hivyo, imefanyia marekebisho pendekezo hilo kwa kuweka umri huo kuwa miaka 35 badala ya miaka 30 kama ilivyopendekezwa awali na kamati.

    Hatua hiyo inalenga kupanua ushiriki wa vijana katika uongozi wa juu wa taifa huku ikiendelea kuhakikisha kuwa wagombea wa urais wanakuwa na kiwango cha kutosha cha uzoefu na ukomavu wa kisiasa.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Usafirishaji wa siri wa madini ya Urani kutoka Kongo

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watafiti nchini Marekani wanasema kiasi kikubwa cha madini ya urani kinachimbwa na kusafirishwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na mauzo ya madini ya kobalti, jambo linalozua wasiwasi kuhusu usalama na uangalizi wa shughuli hizo.

    Watafiti hao wameripoti katika jarida la Nature Communications kuwa wanakadiria hadi tani elfu tano za madini ya urani huenda ziliondoka DRC kati ya mwaka 2000 na 2024 na chini ya asilimia kumi kutangazwa au kuwekwa chini ya ulinzi wa kimataifa.

    Watafiti wanasema matokeo yao yanafichua pengo kubwa katika uangalizi wa nyuklia na mazingira, katika ufunguo wa ugavi wa mpito wa nishati duniani.

    Madini ya Cobalt kutoka Ukanda wa Shaba wa DRC ni muhimu kwa magari ya umeme, simu janja na mpito mpana wa nishati. Lakini watafiti kutoka Princeton na Chuo Kikuu cha Wisconsin wanasema Urani kiasili hufungamana na cobalt na inasafiri bila kutambuliwa katika mauzo ya nje.

    Wanasema baadhi ya nyenzo za mionzi pia zinaishia kwenye taka za mgodi, na kuziweka jamii katika hatari. Watafiti wanatoa wito wa ulinzi mkali wa kimataifa katika mnyororo wa usambazaji wa cobalt ili kuendana na mahitaji yanayoongezeka. BBC iliwasiliana na serikali ya DRC, lakini bado haijatoa majibu kuhusu utafiti huo

    DRC, ni mzalishaji mkubwa wa kobalti duniani.

    Mbali ya Kobalt nchi hiyo pia ina hazina kubwa zaidi duniani ya madini mengine ya thamani kubwa na yale muhimu, yakiongozwa kama vile, koltani, na dhahabu. Rasilimali hizi zilizoko chini ya ardhi, zenye thamani ya zaidi ya dola za Marekani trilioni 24, ndizo zinazochochea masoko ya teknolojia na nishati safi duniani.

    Lakini nchi hiyo imebakia katika hali ya umaskini kutokana na madini mengi kuchinmbwa kiholela bila udhibiti wa serikali na kiasi fulani kutoka na na maeneo yenye utajiri wa madini kukumbwa na vita vya muda mrefu au vinavyojirudiarudia.

    Pia unaweza kusoma:

  7. UEFA yatishia kususia Kombe la Dunia iwapo mipango ya FIFA itaidhinishwa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mpango wenye utata wa FIFA wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi umepata pigo kubwa. Mashirikisho 41 ya soka kutoka Amerika Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean yameukataa mpango huo, yakijiunga na upinzani wa pamoja wa mashirikisho yote ya Ulaya.

    Rais wa FIFA, Gianni Infantino, anasisitiza kuwa mpango huo ungeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili kwa mashirikisho ya soka ya kitaifa duniani kote.

    Mataifa yote 55 ya soka ya Ulaya yamekubaliana kususia Kombe la Dunia iwapo FIFA itatekeleza mpango huo. UEFA imesema timu zake zitashiriki katika mashindano ya FIFA tu iwapo mpango huo hautatekelezwa.

    Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa dharura wa Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA). Laura McAllister ni makamu wa rais wa Shirkisho la Soka Barani Ulaya.

    "Hatua ni wazi kabisa ni kitisho kwa mchezo wa soka kwa sababu pale tu utakapouza hisa kwa wawekezaji binafsi kwenye mpira ni wazi kabisa inatoa picha tofauti kabisa na msukumo wa tofauti kwa wale ambao ni ni wasimamizi wa Mchezo husika" alisema Laura.

    Uwezekano wa timu za Ulaya kujiondoa katika mashindano ya FIFA huenda ukawakatisha tamaa wawekezaji wa mradi huo wa kuuza hisa katika mashindano yake kwa wawekezaji binafsi chini ya Rais wake Gian Infantino, kwa kuwa timu za Ulaya ndizo zinazotawala mchezo wa soka.

    Soma Zaidi:

  8. Kenya yawa timu ya kwanza kuyaaga mashindano ya WAFCON 2026

    .

    Chanzo cha picha, CAF

    Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake zinaendelea nchini Morocco.

    Kenya imekuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 mbele ya Senegal.

    Kenya imetolewa kwa kufungwa michezo yote miwili ya mwanzo kwani katika mchezo wa kwanza ilichezea kichapo cha 4-0 mbele ya wenyeji Morocco.

    .

    Chanzo cha picha, CECAFA

    Katika mchezo mwingine wa kundi A, Morocco wamewachapa Algeria 1-0 na kufuzu kwa hatua ya robo fainali.

    Leo ni michezo miwili ya kundi B ambapo Ivory Coast inakipiga na Afrika Kusini kabla ya Tanzania kushuka dimbani dhidi ya Burkina Faso.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Rais wa Kenya azungumzia mustakabali wa nchi baada ya mwaka 2030

    .

    Chanzo cha picha, State House

    Rais wa Kenya, William Ruto, amesema atazindua rasmi mashauriano ya kitaifa tarehe 12 Agosti 2026 ili kujadili mustakabali wa nchi baada ya mwaka 2030.

    Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni siku ya Alhamisi, Rais alisema kuwa mjadala huo, aliouelezea kuwa tafakuri muhimu zaidi tangu kupitishwa kwa Katiba ya mwaka 2010, utahusisha serikali, vyama vya siasa, serikali za kaunti, wafanyabiashara na hasa vijana.

    Alisema Kenya inaweza kuwa nchi yenye ustawi mkubwa, mapato ya juu na ushindani wa kimataifa ndani ya kizazi kimoja, iwapo itaendelea kudumisha utulivu na umoja wa kitaifa.

    Rais Ruto aliahidi kuwaunganisha Wakenya wote, akisema kuwa mkataba wa maendeleo wa taifa “lazima uundwe na Wakenya wenyewe kupitia mazungumzo ya wazi na ushirikishi wa kitaifa.”

    “Haya si mazungumzo ya kuandaa waraka mwingine wa serikali. Ni kuhusu kujenga mwafaka mpya wa kitaifa,” alisema rais.

    Rais alikiri kuwa maono ya taifa baada ya mwaka 2030 yaani (Vision 2030), ambayo yalilenga kuifanya Kenya kuwa taifa la kipato cha juu cha kati ifikapo mwaka 2030, hadi sasa hayajafanikiwa kufikia malengo yake.

    Hata hivyo, alisisitiza kuwa serikali yake imefanikiwa kurejesha utulivu wa uchumi mkuu, kupunguza mfumuko wa bei pamoja na gharama za ukopaji, na kuimarisha akiba ya fedha za kigeni.

    Hotuba ya Rais Ruto, ambayo ilijikita zaidi katika maendeleo ya muda mrefu, haikutoa uzito mkubwa kwa changamoto za sasa kama vile deni la taifa, gharama kubwa ya maisha, ukosefu wa ajira kwa vijana, na ukatili wa polisi.

    Kenya itafanya uchaguzi mkuu mwezi Agosti 2027, na rais analenga kugombea muhula wake wa pili na wa mwisho wa miaka mitano kama rais wa nchi.

  10. Hamas yakubali kuweka silaha chini Gaza; Trump kutangaza mpango wa Bodi ya Amani

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha katika Ukanda wa Gaza huku akiongeza kuwa taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.

    Trump atangaza mpango wa Bodi ya Amani

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Bodi ya Amani imefikia makubaliano ya kuhakikisha Hamas na makundi mengine yenye silaha katika Ukanda wa Gaza yanaweka silaha chini kabisa.

    Afisa mwandamizi wa Hamas ameliambia shirika la habari la BBC kwamba kundi hilo limekubali mpango wa Bodi ya Amani wa kuachana kabisa na silaha huko Gaza, na kwamba taarifa rasmi itatolewa hivi karibuni.

    Kwa upande wake, Israel bado haijatoa maoni au kauli rasmi kuhusu tangazo hilo.

    Trump amesema kuwa Israel itaondoka katika Ukanda wa Gaza kadri zoezi la kuachana na silaha litakapokamilika, na akayataja makubaliano hayo kuwa "hatua muhimu kuelekea Gaza hatimaye kutawaliwa na serikali mpya ya Kipalestina."

    Awamu ya pili ya mpango wa usitishaji mapigano huko Gaza ulioratibiwa na Marekani inajumuisha kundi la Hamas kuachana kabisa na serikali.

    Awamu hiyo ya pili pia inahusisha ujenzi upya wa Ukanda wa Gaza, ambao umeathiriwa vibaya na vita vya muda mrefu.

    Soma Zaidi:

  11. Hujambo msomaji wetu. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 31/07/2026