Nauru: Nchi pekee isiyo na timu ya taifa ya mpira wa miguu

l

Chanzo cha picha, Paul Watson

    • Author, Nathan Edwards
    • Nafasi, BBC
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Mpira wa miguu ni mchezo usiokuwa na umaarufu katika kisiwa cha Pasifiki cha Naura. Haijawahi kuwa na timu katika mechi rasmi ya kimataifa na ina uwanja mmoja tu wa mchanga.

Ingawa watu wake hufuatilia mechi kubwa za Ligi Kuu England, na watoto huvaa jezi za Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, majaribio mengi ya kuanzisha timu ya mpira yamwekama.

Lakini mambo yanaanza kubadilika polepole huku kundi la watu wa kujitolea, likiongozwa na mchezaji wa zamani wa akademi ya Uingereza Charlie Pomroy wakitaka kuutambulisha mchezo huo katika taifa ambalo zamani lilikuwa tajiri zaidi duniani kwa pato la mtu mmoja mmoja, lakini sasa taifa hilo linategemea sana misaada ya kigeni na lina moja ya viwango vya juu zaidi vya unene duniani.

Chapisho la mitandao ya kijamii kutoka Shirikisho la Soka la Nauru liliwapongeza mabingwa wapya wa dunia Spain na kusema "siku moja tutakuwa katika nafasi ya Uhispania."

Hii ni nchi ambayo haina timu ya kimataifa ya wakubwa. Kuanzisha mpira katika kisiwa ambapo uchimbaji madini kupita kiasi umeacha mandhari katika mazingira, si jambo rahisi.

Kwa nini soka limeshindwa?

l

Chanzo cha picha, Shirikisho la Soka la Nauru

Maelezo ya picha, Wakazi hawa wa Nauru wakitazama fainali ya Kombe la Dunia kwa simu

Nauru ilijaribu kuendeleza soka katika siku za nyuma, lakini haijawahi kufanikiwa. Historia tata inaonyesha ni kwa nini mchezo maarufu zaidi duniani umeshindwa kufanyika huko.

Naura ipo katika Bahari ya Pasifiki maili 2,500 kaskazini mashariki mwa Australia, ina utajiri wa madini ya fosfeti. Nauru, ambayo ilikuwa ni eneo linalojiendesha wenyewe la Australia hadi uhuru mwaka 1968, ilichimbwa madini kwa wingi mwishoni mwa karne ya 20.

Madini hayo yalikauka, na kuiacha nchi hiyo ambayo hapo awali iliitwa Kisiwa cha Pleasant ikionekana kuwa imechakaa, huku sehemu kubwa za maeneo yake ya kati zikiwa haziwezi kukaliwa na watu na kutolimika.

Hii ilisababisha idadi kubwa ya watu 12,000 kukimbilia karibu na kingo za pwani katika kisiwa chenye ukubwa wa kilomita za mraba 21 pekee, huku mabadiliko ya tabia nchi na kuongezeka kwa viwango vya bahari yakitishia uhai wa kisiwa hicho.

Ardhi yake tasa imeifanya nchi hiyo kuagiza zaidi ya 90% ya chakula kutoka nje, hasa kile kilicho chakatwa viwandani, na kusababisha 69% ya idadi ya watu kuwa wanene kupita kiasi na karibu 40% kuwa na kisukari cha aina ya 2.

Mojawapo ya vyanzo vyake vikuu vya mapato sasa ni kituo cha kuzuilia wahamiaji cha Australia ambacho kipo kwa muda mrefu katika karne hii.

Maisha ya kila siku kisiwani ni magumu, lakini mchezo pekee unaopendwa ni Mchezo wa Soka wa Australia, ambao ni mchanganyiko wa raga na mpira wa kikapu, huchezwa na 30% ya wenyeji.

Pia Nauru ni maarufu kwa riadha na kuinua uzito, nchi hiyo imeshiriki katika Olimpiki.

Juhudi za Nauru

o

Chanzo cha picha, Paul Watson

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nauru itaandaa Michezo ya Micronesia mwaka 2028 - tukio la michezo mingi linalojumuisha mpira wa miguu na litaonyesha hamu ya kisiwa hicho kukuza sifa yake ya kimataifa kupitia michezo.

"Wanajaribu kubadilisha taswira ya nchi," anasema Pomroy, mkurugenzi wa ufundi wa Nauru Soccer na mmoja ya watu wanane wanaojitolea, wanaolenga kuendeleza mpira wa miguu kisiwani humo.

Mwingereza huyo, ambaye asili yake ni Stevenage alifanya kazi katika klabu yake ya nyumbani ilipokuwa bado haijacheza katika ligi, ana uzoefu na soka.

Hapo awali alianzisha shirika la hisani katika jiji la Siem Reap nchini Cambodia ambalo liliishia kuwa akademi ambayo hadi sasa imetoa wachezaji 47 ambao wacheza katika timu kubwa katika nchi hiyo ya Asia, na pia inaendesha programu nchini India kwa kupeleka mpira wa miguu kwa jamii zisizohudumiwa vya kutosha.

Kuhusu Naura wameanzisha kampeni ya kuwapa kila mtoto wa miaka minne hadi 14 mpira mmoja takriban watoto 2,000 - na wanafanya kazi na makanisa na shule 11 za kisiwa hicho kupeleka mipira hiyo. Mipira hiyo itawasilishwa 200 kwa wakati mmoja kwa ndege.

Pomroy ambaye amefanya kazi katika ya kukuza mpira wa miguu katika bara la Amerika Kusini na Antaktika, anasema “ndoto yangu binafsi ni kwamba mchezo wa kwanza wa kimataifa wa Nauru uchezwe na watoto wote wenye umri wa miaka 18 ambao wamekuwa watapitia mfumo wetu."

Mara tu Pomroy atakapowasili kwa ajili ya kambi ya mazoezi mwezi Desemba, ataanzisha programu za ukocha kwa wachezaji na makocha wanaotarajiwa ili mchezo huo uweze kuendelea mwaka mzima.

Mengi ya haya yanategemea kupata sehemu za kucheza.

Sehemu kubwa ya ardhi inamilikiwa na watu binafsi au haikaliki, lakini Tyrone Deiye, mmoja wa wanaojitolea anatumai kutumia baadhi ya ardhi ya familia yake kutengeneza viwanja vingi zaidi kuliko ile iliyopo sasa.

Pomroy anasisitiza kwamba Nauru Soccer sio "kulazimisha soka kuathiri kila mtu" lakini anasema ni kuhusu kuweka msingi wa mchezo huo, kukuza mitindo ya maisha yenye afya na kujenga jamii.

"Kama tutakaa hapa katika kipindi cha miaka mitano ijayo, naamini kwa dhati tutakuwa na timu ya wakubwa ambayo itajazwa na wachezaji wa miaka 18, 19, au 20."