Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Everton inamuwinda Vardy ambaye ni mchezaji huru
Everton inafikiria kumsajili Jamie Vardy,39, baada ya kumkosa mshambuliaji siku ya mwisho ya dirisha la usajili, huku mshambuliaji huyo wa zamani wa England akiwa huru baada ya kuondoka Cremonese. (The Sun)
Timu ya David Moyes pia inaweza kumfuata mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa, Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 30, ambaye pia ni mchezaji huru baada ya kuondoka klabu ya Monterrey ya Mexico. (Talksport)
Winga wa Ivory Coast, Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 33, ni mmoja wa wachezaji wanaozingatiwa na AC Milan wanapotafuta kusajili mchezaji huru wa kuongeza nguvu katika upande wa kushoto wa safu yao ya ushambuliaji. (Gazzetta dello Sport)
AC Milan inaangalia uwezekano wa kumsajili Wilfried Zaha, mwenye miaka 33, kama mchezaji huru ili kuimarisha upande wa kushoto wa safu yao ya ushambuliaji. (Gazzetta dello Sport - kwa Kitaliano)
Kiungo mshambuliaji wa Brazil Estevao Willian, mwenye miaka 19, ana wasiwasi kuhusu kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea chini ya kocha Xabi Alonso, na anaweza kutafuta uhamisho mwezi Januari kulingana na hali yake. (ESPN Brazil)
Arsenal imeweka kipengele cha kumrudisha Ethan Nwaneri, mwenye miaka 19 na mchezaji wa timu ya England chini ya miaka 21, mwezi Januari ikiwa itamhitaji, licha ya kuwa amekwenda Borussia Dortmund kwa mkopo wa msimu mmoja. (Sky Sports Germany)
Winga wa Sunderland, Chemsdine Talbi, mwenye umri wa miaka 21, yuko katika mazungumzo na klabu ya Al-Ittihad ya Saudi Pro League, huku klabu za Fenerbahce na Galatasaray pia zikionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco. (Talksport)
Timu ya Arabian Falcons, inayoshiriki Ligi Daraja la Pili ya Umoja wa Falme za Kiarabu na kunolewa na Jonjo Shelvey, inamfuatilia winga wa zamani wa Manchester United na England, Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 26. (Daily Mirror)
Mshambuliaji wa Argentina, Lautaro Martinez, 29, amesema ilikuwa heshima kubwa kuuliziwa na Barcelona, lakini alisisitiza kuwa anataka kuendelea kuichezea klabu ya Inter Milan. (Sky Sports Italia)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi