Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lionel Messi astaafu katika soka la kimataifa
Mchezaji Lionel Messi amestaafu katika michezo ya kimataifa.
Messi mwenye umri wa miaka 39, ambaye ana mkataba na Inter Miami hadi mwaka 2028, alitangaza Jumatatu kuwa kipindi chake cha mafanikio na timu ya taifa ya Argentina kimefikia mwisho baada ya zaidi ya miaka 20.
Messi amesema alikuwa akitafakari kuhusu mustakabali wake katika soka kufuatia kifo cha baba yake, Jorge, mapema mwezi huu.
Katika ujumbe wa kugusa hisia kwa baba yake, alidokeza uwezekano wa kustaafu akisema: "Sijui jinsi ya kuendelea. Nilikuwa nikicheza soka tu, na sasa sina uhakika kama nitaendelea kucheza kwa muda mrefu zaidi."
Mchezaji huyo sasa ameweka wazi uamuzi wake wa kuhitimisha maisha yake ya soka la kimataifa kupitia chapisho kwenye Instagram, akisema: "Muda unayoyoma, sura za maisha hufungwa, na hii ni sura inayoniumiza sana."
Messi, ambaye ni bingwa wa Kombe la Dunia, alifunga mabao 125 katika mechi 207, jambo linalomfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo na mchezaji aliyeichezea timu hiyo mara nyingi zaidi.
Pia amefunga jumla ya mabao 921 akiichezea Barcelona, Paris St-Germain, Inter Miami na Argentina.
BBC Sport inaangazia baadhi ya matukio muhimu na ya kukumbukwa katika taaluma yake ya kipekee.
Hat-trick yake ya kwanza akiwa kijana yaonyesha kipaji chake
Messi alifunga 'hat-trick' yake ya kwanza katika moja ya mechi kubwa zaidi za soka – El Clasico.
Akiwa na umri wa miaka 19, alifunga mabao yote ya Barcelona katika sare ya 3-3 dhidi ya wapinzani wao Real Madrid mnamo tarehe 10 Machi 2007, likiwa ni tukio lake la kwanza la aina hiyo katika uwanja wa Camp Nou – likiwemo bao maridadi la dakika za mwisho baada ya kuwapita mabeki kadhaa.
Hii inaweza kusemwa kuwa ndiyo wakati ambapo alijipatia umaarufu mkubwa na kuwa jina linalojulikana na kila mtu.
Goli la kuvutia la kibinafsi liliibua kumbukumbu za Maradona
Mwezi mmoja baada ya kufunga mabao matatu katika mechi moja (hat-trick), Messi alifunga bao ambalo huenda halijawahi kupitwa na jingine lolote katika kipindi chote cha taaluma yake tukufu.
Bao hilo lilipatikana katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Getafe kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey, tarehe 18 Aprili 2007.
Katika shambulizi lenye kufanana kwa kiasi kikubwa na lile la Diego Maradona (lile lisilohusisha bao la mkono) dhidi ya Uingereza katika Kombe la Dunia la mwaka 1986, Messi alimiliki mpira akiwa katika eneo la timu yake, akawapita mabeki wapatao watano, akamzunguka kipa na kuuweka mpira wavuni.
Goli la kwanza katika fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ingawa inaonekana ni upuuzi sasa, mwaka 2009 baadhi ya mashabiki wa soka wa Uingereza na waandishi wa habari walihoji kama Messi angeweza kufanya hivyo dhidi ya wapinzani wa Uingereza barani Ulaya - baada ya kushindwa kufunga katika mechi 10 za Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu za Ligi Kuu.
Lakini hakukuwa na shaka tena wakati Messi alipopanda juu zaidi kwenye eneo la hatari na kufunga kwa kichwa krosi ya Xavi katika fainali yake ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United - na mchezo wa kwanza ukawa Messi dhidi ya Cristiano Ronaldo.
Miaka miwili baadaye angefunga katika ushindi mwingine wa mwisho dhidi ya vijana wa Sir Alex Ferguson na kushinda medali ya tatu kati ya nne za washindi wa Ligi ya Mabingwa.
Kuifunga Arsenal mabao manne
Messi alifunga mabao manne kwa mara ya kwanza katika taaluma yake alipoiongoza timu yake kuigaragaza Arsenal katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2010, na kushinda mabao 4-1 katika mchezo wa nyumbani.
Bao lake bora zaidi katika mchezo huo lilikuwa lile alilofunga kwa kupiga mpira juu ya kipa Manuel Almunia na kukamilisha 'hat-trick' yake.
Pia inafaa kutaja rekodi yake ya kufunga mabao matano miaka miwili baadaye dhidi ya Bayer Leverkusen, katika ushindi wa mabao 7-1 kwenye hatua ya 16 bora.
Yeye ndiye mfungaji bora wa pili katika historia ya Ligi ya Mabingwa akiwa na mabao 129, akimfuata Ronaldo.
Kuvunja rekodi ya ufungaji ya Barcelona
Messi alivunja rekodi ya ufungaji mabao ya Barcelona, akiwa na umri wa miaka 24 tu kwa mtindo wa kuvutia kwa kufunga mabao matatu (hat-trick) katika ushindi wa 5-3 dhidi ya Granada mnamo tarehe 20 Machi 2012.
Alifikia rekodi ya mabao 232 iliyowekwa na Cesar Rodriguez miaka 60 iliyopita kwa bao lake la kwanza, akaivunja kwa bao la pili, na kuongeza idadi hiyo kwa bao la tatu.
Kufikia wakati anaondoka Barcelona mwaka 2021, alikuwa amefikisha jumla ya mabao 672.