Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz

Shirika la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) limetangaza kuwa meli nyengine ya kubeba mafuta katika Lango la Hormuz imeshambuliwa

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Aliyekuwa kiongozi wa genge la Crips apatikana na hatia ya mauaji ya Tupac Shakur

    Aliyekuwa kiongozi wa genge la uhalifu, Duane "Keffe D" Davis, amepatikana na hatia ya kupanga mauaji ya Tupac Shakur – hii ikiwa ni hukumu ya kwanza katika kesi ya muda mrefu ambayo haikutatuliwa na iliyowavutia mashabiki wa muziki wa hip-hop kwa karibu miaka 30.

    Baraza la wazee wa mahakama lilimkuta Davis na hatia ya shtaka moja la mauaji kwa kutumia silaha hatari kuhusiana na kifo cha nyota huyo wa rap, aliyeuawa kwa kupigwa risasi kutoka kwenye gari linaloenda kasi jijini Las Vegas mnamo tarehe 7 Septemba 1996.

    Akiwa amevaa suti nyeusi, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 63 alisimama bila kuonyesha hisia zozote mahakamani huko Las Vegas wakati hukumu ikisomwa, kabla ya kusema kuwa atakata rufaa.

    Jamaa wa Shakur walishikana mikono, huku baadhi yao wakikumbatiana na kulia.

    Shakur alikuwa na umri wa miaka 25 alipouawa akiwa katika kilele cha taaluma yake kama mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa rap.

    Amefanikiwa kuuza zaidi ya rekodi milioni 75 duniani kote.

  2. Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz

    Shirika la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) limetangaza kuwa meli nyengine ya kubeba mafuta katika Lango la Hormuz imeshambuliwa.

    Kulingana na ripoti hiyo, meli hiyo ililengwa "wakati ikipita na kutoka katika Lango la Hormuz."

    Shirika hilo la Uingereza limesema tukio hilo lilitokea kilomita 31 mashariki mwa eneo la Khasab nchini Oman, likihusisha "makombora matatu ambayo hayakutambulika."

    Hakuna ripoti za majeruhi au vifo kutokana na shambulio hilo kufikia sasa.

    Saa moja kabla ya ripoti hiyo kutolewa, vyanzo vya habari visivyo rasmi nchini Iran viliripoti kuwa makombora matatu yalikuwa yamerushwa kutoka pwani ya kusini mwa Iran.

    Kama tulivyotangaza hapa muda mfupi uliopita, Mamlaka ya Uingereza ya Operesheni za Meli za Biashara ilitangaza tukio jingine la baharini siku ya Jumatatu, lakini ilibainisha kuwa tukio hilo katika Bahari ya Hindi lilitokea siku ya Jumapili, tarehe 30 Agosti.

  3. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja