Meli nyengine ya kubeba mafuta yashambuliwa katika mlango bahari wa Hormuz

Chanzo cha picha, Reuters
Shirika la Uingereza la Operesheni za Biashara ya Baharini (UKMTO) limetangaza kuwa meli nyengine ya kubeba mafuta katika Lango la Hormuz imeshambuliwa.
Kulingana na ripoti hiyo, meli hiyo ililengwa "wakati ikipita na kutoka katika Lango la Hormuz."
Shirika hilo la Uingereza limesema tukio hilo lilitokea kilomita 31 mashariki mwa eneo la Khasab nchini Oman, likihusisha "makombora matatu ambayo hayakutambulika."
Hakuna ripoti za majeruhi au vifo kutokana na shambulio hilo kufikia sasa.
Saa moja kabla ya ripoti hiyo kutolewa, vyanzo vya habari visivyo rasmi nchini Iran viliripoti kuwa makombora matatu yalikuwa yamerushwa kutoka pwani ya kusini mwa Iran.
Kama tulivyotangaza hapa muda mfupi uliopita, Mamlaka ya Uingereza ya Operesheni za Meli za Biashara ilitangaza tukio jingine la baharini siku ya Jumatatu, lakini ilibainisha kuwa tukio hilo katika Bahari ya Hindi lilitokea siku ya Jumapili, tarehe 30 Agosti.
