Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Marekani yashambulia vifaa vya kurushia makombora vya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

Vikosi vya Marekani vimeshambulia mitambo miwili ya kurusha makombora ya Iran, afisa mmoja wa Marekani amesema, akiashiria mashambulizi ya kwanza yanayojulikana ya Marekani dhidi ya Iran tangu mwishoni mwa Julai.

Muhtasari

  • Mamia ya raia wa kigeni bado hawajulikani walipo katika eneo la mpaka Nepal
  • Nepal yaimarisha juhudi za kuwanusuru mamia ya watu waliokwama mahandaki ya umeme
  • Marekani yashambulia mitambo ya kurushia makombora vya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Abiria walala JKIA huku mgomo wa wafanyakazi wa sekta ya anga ukiendelea

    Mamia ya abiria wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi tangu Jumapili.

    Wasafiri hao, ambao walitarajiwa kusafiri kupitia uwanja mkubwa zaidi wa ndege nchini Kenya, walilala katika maeneo ya mapokezi ya uwanja huo wakisubiri maelekezo kutoka kwa mashirika ya ndege.

    Siku ya Jumatatu asubuhi, mashirika kadhaa ya ndege yalikuwa yakishughulikia taratibu za kuwapeleka abiria wao kwenye hoteli.

    Hii ni baada ya wafanyakazi wa usafiri wa anga, chini ya Chama cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga cha Kenya (KAWU), kuanza mgomo wao Jumapili, wakitangaza kupunguzwa kwa muda kwa shughuli katika viwanja vya ndege vya Kenya.

    Wafanyakazi hao wanadai ustawi ulioboreshwa, mazingira bora ya kazi na utekelezaji wa marupurupu ya ajira yaliyokubaliwa hapo awali.

    Kuanzia JKIA jijini Nairobi hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi huko Mombasa, shughuli zilisimama Jumapili.

    Katibu Mkuu wa KAWU Moss Ndiema alisema wanachama waliacha kazi zao katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kenya, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Kenya na Jambojet, na hawangeendelea hadi malalamiko ya chama hicho dhidi ya yote matatu yatakapotatuliwa

  2. Trump atoa video ya shambulio dhidi ya kisiwa cha Kharg iliyotengenezwa kwa akili mnemba (AI)

    Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video iliyotengenezwa kwa teknolojia ya akili mnemba (AI) kwenye mtandao wa Truth Social, ikionyesha kituo kikubwa cha mafuta kikilipuka na kuungua.

    Bw. Trump aliandika katika maelezo ya video hiyo: "Kisiwa cha Kharg kinaharibiwa kabisa na kusawazishwa na ardhi!!!"

    Video hiyo imetoka wakati ambapo mivutano ya kijeshi kati ya Iran na Marekani imepamba moto kwa wakati mwengine.

    Hapo awali, vikosi vya Marekani vililenga mifumo miwili ya kurushia makombora ya Iran kwenye Kisiwa cha Larak, na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi lilitangaza kuwa lilijibu mashambulizi hayo kwa kulenga kambi mbili za Marekani nchini Jordan kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani (drones).

    Kisiwa cha Kharg ni mojawapo ya vituo muhimu zaidi vya Iran vya kusafirisha mafuta nje ya nchi katika Ghuba ya Uajemi, na sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya mafuta ghafi ya nchi hiyo hufanyika kupitia vituo vilivyoko kisiwani humo.

  3. Familia 32 za Kenya zitagawana fidia ya Ethiopian Airlines

    Karibu miaka saba baada ya ndege ya Ethiopian Airlines Nambari 302 kuanguka ikiwa safarini kuelekea Nairobi, familia 32 za Kenya zinatarajiwa kupokea malipo mapya ya fidia kufuatia kesi ndefu dhidi ya kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing katika mahakama za Marekani.

    Kila familia itapokea dola milioni 2.73, sawa na takriban Shilingi milioni 353, chini ya mpango wa hivi karibuni wa fidia kutokana na ajali hiyo ya Machi 2019. Malipo hayo mapya yanafikia jumla ya dola milioni 87.36, au takriban Shilingi bilioni 11.3, kwa kaya hizo 32 za Kenya zilizoathirika.

    Ikijumuishwa na fidia iliyolipwa katika hatua za awali za mchakato wa kisheria, jumla ya fedha ambazo familia hizo zitapokea inakadiriwa kuwa Shilingi bilioni 17.3.

    Ndege hiyo nambari 302 ilianguka tarehe 10 Machi 2019, dakika sita baada ya kupaa kutoka Addis Ababa, Ethiopia, ikiwa safarini kuelekea Nairobi.

    Abiria na wahudumu wote 157 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo walipoteza maisha katika ajali hiyo. Kenya ilirekodi idadi kubwa zaidi ya vifo miongoni mwa raia wa mataifa zaidi ya 30 waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

    Makubaliano hayo ya hivi karibuni ya fidia yanakuja kufuatia kesi zilizofunguliwa nchini Marekani, ambapo familia hizo zilidai fidia kutoka kwa Boeing kuhusiana na ajali hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, familia hizo zilipata hadhi ya kisheria kama waathiriwa wa uhalifu ndani ya mfumo wa haki ya jinai wa Marekani baada ya Boeing kushutumiwa kwa kuwapotosha wadhibiti wa sekta hiyo.

  4. Watu wanane wafariki na wengine 18 hawajulikani walipo baada ya kivuko kupinduka karibu na pwani ya Cyprus

    Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha video iliyotengenezwa kwa teknolojia ya akili bandia (AI) kwenye mtandao wa Truth Social, ikionyesha kituo kikubwa cha mafuta kikilipuka na kuungua.

    Bw. Trump aliandika katika maelezo ya video hiyo: "Kisiwa cha Kharg kinaharibiwa kabisa na kusawazishwa na ardhi!!!"

    Video hiyo imetoka wakati ambapo mivutano ya kijeshi kati ya Iran na Marekani imepamba moto tena. Hapo awali, vikosi vya Marekani vililenga mifumo miwili ya kurushia makombora ya Iran kwenye Kisiwa cha Larak, na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi lilitangaza kuwa lilijibu mashambulizi hayo kwa kulenga kambi mbili za Marekani nchini Jordan kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani (drones).

    Kisiwa cha Kharg ni mojawapo ya vituo muhimu zaidi vya Iran vya kusafirisha mafuta nje ya nchi katika Ghuba ya Uajemi, na sehemu kubwa ya mauzo ya nje ya mafuta ghafi ya nchi hiyo hufanyika kupitia vituo vilivyoko kisiwani humo

  5. Mamia ya raia wa kigeni bado hawajulikani walipo katika eneo la mpaka Nepal

    Watalii kutoka kote duniani huja Nepal kwa ajili ya milima na maeneo yake matakatifu.

    Taarifa kuhusu watu hao waliopotea ni kama ifuatavyo:

    • India - Takriban raia 320 wa India hawajulikani walipo, kulingana na wizara ya mambo ya nje mjini Delhi
    • China - Wizara ya mambo ya nje ya China inasema karibu raia 100 wa China hawajulikani walipo nchini Nepal
    • Marekani - Wamarekani 90 bado hawajulikani walipo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
    • Ukraine - Raia 62 wa Ukraine hawajulikani walipo, polisi wa Nepal wanasema
    • Malaysia - Raia 51 wa Malaysia waliokuwa wakisafiri na kampuni ya Fishtail Tours and Travels hawajulikani walipo kufuatia mafuriko, maafisa wanasema
    • Australia - Hakuna taarifa kuhusu walipo raia 41 wa Australia, kulingana na naibu waziri wa uhamiaji wa nchi hiyo
    • Uingereza - Polisi wa Nepal wanasema raia 33 wa Uingereza hawajulikani walipo; shirika la utangazaji la serikali ya China, CCTV, pia linaripoti kuwa raia 15 wa Uingereza ni miongoni mwa waliopotea huko Tibet - haijulikani ni wangapi kati yao ambao tayari wamejumuishwa katika takwimu zilizotolewa na Nepal
    • Canada - raia 30 wa Canada hawajulikani walipo, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo inasema
    • Idadi ndogo ya wasafiri kutoka Korea Kusini, Afrika Kusini, Ureno, Uholanzi na New Zealand pia ni miongoni mwa waliopotea.
  6. Nepal yaimarisha juhudi za kuwanusuru mamia ya watu waliokwama katika mahandaki ya umeme

    Ofisi ya Waziri Mkuu wa Nepal imesema kuwa juhudi za uokoaji katika handaki kwenye mradi wa umeme wa maji wa Trishuli-3A zimeongezewa nguvu, zikijumuisha shughuli za ulipuaji.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, ofisi hiyo imesema kuwa timu ya pamoja ya watu 90 imetumwa eneo la tukio, ikijumuisha vikosi vya usalama, polisi, na waokoaji wanaoambatana na mbwa waliofunzwa.

    Awali, shimo lenye ukubwa wa futi 2 kwa 3 (mita 0.6 kwa 0.9) lilitengenezwa kwenye sehemu ya juu ya handaki, na waokoaji wakashuka chini kwa kutumia kamba. Hawakupata majibu yoyote kutoka ndani walipopiga kelele kuita.

    Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku timu hiyo ikifanya kazi bila kuchoka usiku na mchana licha ya kuwepo kwa mazingira magumu na hatari, ofisi ya Waziri Mkuu imesema.

    Miongoni mwa watu zaidi ya 2,500 waliopotea, mamia wanadhaniwa kuwa ni wafanyakazi katika miradi ya umeme wa maji nchini Nepal.

  7. Marekani yashambulia mitambo ya kurushia makombora ya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

    Vikosi vya Marekani vimeshambulia mitambo miwili ya kurusha makombora ya Iran, afisa mmoja wa Marekani amesema, akiashiria mashambulizi ya kwanza yanayojulikana ya Marekani dhidi ya Iran tangu mwishoni mwa Julai.

    "Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vilionekana vikijiandaa kurusha makombora yenye mabomu ya baharini kwenye Mlango wa Hormuz," mshirika wa BBC wa Marekani CBS News alimnukuu msemaji wa Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) Cdr Tim Hawkins akisema.

    IRGC ilisema shambulio la Jumapili liliua na kujeruhi watu kadhaa, na kuapa "kulipiza kisasi".

    Baadaye ilisema ilizindua shambulio dhidi ya malengo ya kijeshi ya Marekani huko Jordan, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

    BBC imewasiliana na Centcom kwa maoni.

  8. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja