Moja kwa moja, Marekani yashambulia vifaa vya kurushia makombora vya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

Vikosi vya Marekani vimeshambulia mitambo miwili ya kurusha makombora ya Iran, afisa mmoja wa Marekani amesema, akiashiria mashambulizi ya kwanza yanayojulikana ya Marekani dhidi ya Iran tangu mwishoni mwa Julai.

Muhtasari

  • Mamia ya raia wa kigeni bado hawajulikani walipo katika eneo la mpaka Nepal
  • Nepal yaimarisha juhudi za kuwanusuru mamia ya watu waliokwama mahandaki ya umeme
  • Marekani yashambulia mitambo ya kurushia makombora vya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Mamia ya raia wa kigeni bado hawajulikani walipo katika eneo la mpaka Nepal

    .

    Chanzo cha picha, RSS

    Watalii kutoka kote duniani huja Nepal kwa ajili ya milima na maeneo yake matakatifu.

    Taarifa kuhusu watu hao waliopotea ni kama ifuatavyo:

    • India - Takriban raia 320 wa India hawajulikani walipo, kulingana na wizara ya mambo ya nje mjini Delhi
    • China - Wizara ya mambo ya nje ya China inasema karibu raia 100 wa China hawajulikani walipo nchini Nepal
    • Marekani - Wamarekani 90 bado hawajulikani walipo, kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani
    • Ukraine - Raia 62 wa Ukraine hawajulikani walipo, polisi wa Nepal wanasema
    • Malaysia - Raia 51 wa Malaysia waliokuwa wakisafiri na kampuni ya Fishtail Tours and Travels hawajulikani walipo kufuatia mafuriko, maafisa wanasema
    • Australia - Hakuna taarifa kuhusu walipo raia 41 wa Australia, kulingana na naibu waziri wa uhamiaji wa nchi hiyo
    • Uingereza - Polisi wa Nepal wanasema raia 33 wa Uingereza hawajulikani walipo; shirika la utangazaji la serikali ya China, CCTV, pia linaripoti kuwa raia 15 wa Uingereza ni miongoni mwa waliopotea huko Tibet - haijulikani ni wangapi kati yao ambao tayari wamejumuishwa katika takwimu zilizotolewa na Nepal
    • Canada - raia 30 wa Canada hawajulikani walipo, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo inasema
    • Idadi ndogo ya wasafiri kutoka Korea Kusini, Afrika Kusini, Ureno, Uholanzi na New Zealand pia ni miongoni mwa waliopotea.
  2. Nepal yaimarisha juhudi za kuwanusuru mamia ya watu waliokwama katika mahandaki ya umeme

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ofisi ya Waziri Mkuu wa Nepal imesema kuwa juhudi za uokoaji katika handaki kwenye mradi wa umeme wa maji wa Trishuli-3A zimeongezewa nguvu, zikijumuisha shughuli za ulipuaji.

    Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, ofisi hiyo imesema kuwa timu ya pamoja ya watu 90 imetumwa eneo la tukio, ikijumuisha vikosi vya usalama, polisi, na waokoaji wanaoambatana na mbwa waliofunzwa.

    Awali, shimo lenye ukubwa wa futi 2 kwa 3 (mita 0.6 kwa 0.9) lilitengenezwa kwenye sehemu ya juu ya handaki, na waokoaji wakashuka chini kwa kutumia kamba. Hawakupata majibu yoyote kutoka ndani walipopiga kelele kuita.

    Shughuli za uokoaji zinaendelea, huku timu hiyo ikifanya kazi bila kuchoka usiku na mchana licha ya kuwepo kwa mazingira magumu na hatari, ofisi ya Waziri Mkuu imesema.

    Miongoni mwa watu zaidi ya 2,500 waliopotea, mamia wanadhaniwa kuwa ni wafanyakazi katika miradi ya umeme wa maji nchini Nepal.

  3. Marekani yashambulia mitambo ya kurushia makombora ya Iran kwenye Kisiwa cha Larak

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Vikosi vya Marekani vimeshambulia mitambo miwili ya kurusha makombora ya Iran, afisa mmoja wa Marekani amesema, akiashiria mashambulizi ya kwanza yanayojulikana ya Marekani dhidi ya Iran tangu mwishoni mwa Julai.

    "Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) vilionekana vikijiandaa kurusha makombora yenye mabomu ya baharini kwenye Mlango wa Hormuz," mshirika wa BBC wa Marekani CBS News alimnukuu msemaji wa Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) Cdr Tim Hawkins akisema.

    IRGC ilisema shambulio la Jumapili liliua na kujeruhi watu kadhaa, na kuapa "kulipiza kisasi".

    Baadaye ilisema ilizindua shambulio dhidi ya malengo ya kijeshi ya Marekani huko Jordan, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.

    BBC imewasiliana na Centcom kwa maoni.

  4. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja