Tunasitisha mashambulizi dhidi ya Israel, lakini tutaanza tena iwapo Israel itaishambulia Lebanon - Iran

Chanzo cha picha, Reuters
Makao makuu ya jeshi la Iran Khatam al-Anbiya yamesema katika taarifa kwamba "tunasitisha shughuli za vikosi vya kijeshi".
Lakini wameonya katika taarifa hiyo hiyo kwamba ikiwa mashambulizi yataendelea, "ikiwa ni pamoja na kusini mwa Lebanon," Iran itajibu "kwa nguvu zaidi kuliko hapo awali".
Iran ilianza operesheni zake jana kujibu mashambulizi ya Israel kusini mwa Beirut. Israel ililipiza kisasi kwa kushambulia Iran.
Maafisa waandamizi wa kisiasa na kijeshi wa Iran walikuwa wametoa maonyo jana jioni kwamba Iran ingejibu kijeshi kwa kile walichokielezea kama ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Iran imesisitiza kwamba wanachukulia usitishaji mapigano nchini Lebanon kama sehemu ya usitishaji mapigano na Iran vile vile.
Israel na Iran zinatafuta kusitisha mapigano mara moja - Trump
Awali, Rais wa Marekani Donald Trump alisema mazungumzo ya mwisho kuhusu "amani" yanaendelea lakini "yanakabiliwa na ujinga au upumbavu ndani yake".
Alisema katika chapisho lake kwenye mtandao wa Truth Social: "Pande zote mbili, Israeli na Iran, zinatafuta kufanya makubaliano ya haraka ya KUSITISHA MAPIGANO!"
"Vikwazo vitasalia, kwa ukamilifu na athari zake, hadi 'Makubaliano ya Mwisho' yatakapofikiwa. Mambo yanatakiwa kufanyika kwa haraka," aliongeza.
Soma zaidi:
























