Tetesi za soka Ulaya: Delap arejea kwenye rada ya Everton huku Salah akimezewa mate Uturuki

Muda wa kusoma: Dakika 2

Everton imefufua nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Liam Delap, mwenye umri wa miaka 23, huku pia ikipima uwezekano wa kuwasajili mabeki wa Uingereza John Stones, 31, anayetarajiwa kuondoka Manchester City mwishoni mwa msimu, na Ben White, 28, wa Arsenal.(i-paper).

Klabu hiyo pia inataka kuongeza muda wa mkopo wa winga wa England Jack Grealish, 30, kutoka Manchester City.

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 33, huenda akakataa ofa kutoka ligi ya Saudia msimu huu wa joto, huku klabu ya Uturuki Fenerbahce ikitajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumsajili nyota huyo wa Misri.(A Spor).

Chelsea inaamini inaweza kupata hadi pauni milioni 60 kwa kumuuza mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, mwenye umri wa 24, ambaye ameitumikia Bayern Munich kwa mkopo msimu huu. (Athletic).

Manchester United inamuwania beki wa kushoto wa West Ham El Hadji Malick Diouf, mwenye umri wa miaka 21, huku nyota huyo wa Senegal akitajwa kama mbadala wa kuongeza ushindani kwa Luke Shaw, 30, katika nafasi hiyo. (Guardian).

Tottenham iko tayari kumuuza kipa wa Italia Guglielmo Vicario, 29, kwa Inter Milan msimu huu wa joto.

Makipa wawili waliopo kwenye rada ya Spurs kuziba nafasi hiyo ni James Trafford, 23, wa Manchester City na Bart Verbruggen, mwenye umri wa 23, wa Brighton. (Teamtalk).

Juventus inamfukuzia kipa wa Liverpool Alisson Becker, mwenye umri wa miaka 33, huku nyota huyo wa Brazil akiwa amebakisha mwaka mmoja pekee kwenye mkataba wake. (Mail)

Aston Villa inachunguza uwezekano wa kumsajili kiungo wa Morocco Azzedine Ounahi, 26, kutoka Girona. (Sportsboom)

Klabu moja kutoka Italia ambayo haijatajwa jina imeanza kuulizia uwezekano wa kumsajili winga wa Manchester United Jadon Sancho, 26, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto. (Sky sports)

Nottingham Forest inakaribia kufikia kiwango cha fedha kinachotakiwa na Fenerbahce kwa beki wa kushoto wa England Archie Brown, 23. (Aspor)

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid