Jangwa la Atacama: Kwa nini wanasayansi wanapigania giza lisitoweke?

l

Chanzo cha picha, Yuri Beletsky (LCO

    • Author, Richard Fisher
    • Nafasi, BBC
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 5

Ni saa 8:00 usiku katika Jangwa la Atacama nchini Chile, na ninaamka katika kiza. Ndani ya chumba changu, hujui kama macho yako yamefunguliwa au yamefumbwa.

"Kuna maeneo machache sana Duniani yenye hali hizi," anasema Itziar de Gregorio-Monsalvo, mwanafizikia mkuu wa anga katika Kituo cha Kuangalia Kusini mwa Ulaya nchini Chile. Wanaastronomia kama yeye humiminika kwenye sehemu hii ya mbali ya Jangwa la Atacama kwa ajili ya mandhari hii.

Lakini kila mwaka, mwanga kutoka miji iliyo karibu, majengo ya viwanda na shughuli za uchimbaji madini hufunika anga. Watafiti wanapiga hilo ili kuhifadhi mandhari ya kiza asili.

Ninapoangalia angani eneo ninaloishi London, mwanga wa mamilioni ya balbu za taa unaangaza juu ya jiji, huficha nyota zote isipokuwa zile angavu zaidi. Lakini katika Jangwa la Atacama, anga la usiku ni angavu zaidi kuliko nilivyowahi kuona.

Nilitembelea Paranal, kituo cha anga za juu kinachoendeshwa na European Southern Observatory (Eso), ambacho ni nyumbani kwa baadhi ya darubini za uwezo wa hali ya juu zaidi duniani.

Giza linalopotea

k

Chanzo cha picha, ESO/ P Horálek

Maelezo ya picha, Uchafuzi wa mwanga kutoka miji iliyo pembezoni mwa jangwa kwenye mwonekano wa anga la usiku huko Atacama

Kila mwaka, taa kutoka nje ya Paranal zimekuwa zikizidi kukaribia. Giza ni la thamani - liko hatarini kutoweka. Kadri balbu za umeme zinavyoongezeka, karibu 80% ya idadi ya watu Duniani sasa wanaishi chini ya anga yenye mwanga wa balbu.

Utafiti wa hivi karibuni juu ya nyota uligundua kuwa, kwa wastani duniani kote, anga linazidi kumulikwa na mwanga wa bulbu karibu 10% kwa mwaka kati ya 2011-2022.

Kama mtu angeweza kuona nyota 250 mwanzoni mwa kipindi hicho, watafiti waligundua, ungeweza kuona nyota 100 pekee mwishoni.

Wanasaikolojia wamependekeza kwamba nyota zinazotoweka zinaweza kuzidisha magonjwa ya akili, kwa kuondoa uhusiano wa muda mrefu wa mwanadamu na ulimwengu wa asili.

Na wanasaikolojia wameonyesha kwamba wakati mwanga bandia unapowadanganya wanyama na mimea kuamini kuwa ni mchana, unaweza kuathiri tabia na fiziolojia yao, na kuharibu mifumo ikolojia.

Kwa sababu hizi, baadhi ya watafiti wanasema kwamba mwanga mwingi sasa unapaswa kuainishwa kama uchafuzi wa mazingira, pamoja na uchafuzi wa kemikali wa hewa au maji.

Kwa kifupi, ulimwengu wenye taa nyingi, haumaanishi ndio ulimwengu mzuri.

Maonyo ya kwanza yalitoka kwa wanaastronomia tangu miaka ya 1970 wakati watafiti huko California nchini Marekani walipogundua kwamba taa za San Francisco zingefunika uchunguzi wao kupitia darubini.

Wakati huo, wanaastronomia walitabiri kwamba ongezeko la mwangaza katika anga la usiku juu ya kiwango cha asili litaathiri pakubwa unajimu wa ardhini.

Giza ni zuri

m

Chanzo cha picha, Richard Fisher)

Maelezo ya picha, Uchafuzi wa mwanga unadhibitiwa vikali huko Paranal na wageni wanahimizwa kuhifadhi giza
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kikiwa katikati eneo la mwisho la giza katika ulimwengu unaong'aa, kituo cha uchunguzi cha Paranal cha Eso - kinachoendeshwa na muungano wa nchi wanachama wa Ulaya - kina vifaa kadhaa vya kiwango cha dunia vya kutazama ulimwengu.

Hizi ni pamoja na Darubini Kubwa ya VLT na nyingine kubwa zaidi ya ELT, ambayo inatarajiwa kujengwa kikamilifu ifikapo mwaka 2029.

Baadhi ya ugunduzi muhimu zaidi wa angani wa karne ya 21 umefanywa hapa, kuanzia picha ya kwanza ya moja kwa moja ya exoplanet hadi njia za nyota zinazothibitisha uwepo wa shimo jeusi kubwa katikati ya galaksi yetu.

Mara tu unapofika, unahisi jinsi giza lilivyo la thamani hapa. Eneo lote limeundwa kuzuia mwanga kuingia. Mabango yakiwa yametawanyika kuzunguka majengo, yameandikwa "Dark is Beauty", yakiwahimiza watu kuzima tochi zao. Wakati wa jioni, madereva huagizwa kutumia magari yasiyo na taa kali.

Eneo hili lipo katika mwinuko wa mita 2,600 (futi 8,500), inachukua hadi saa mbili kufika Paranal kutoka mji wa karibu wa Antofagasta, umbali wa maili 81 (kilomita 130). Mbali na barabara, hakuna dalili za uwepo wa ubinadamu; ni jangwa linalozunguka bahari ya Pasifiki.

Sababu ya kituo hiki cha uchunguzi na vingine katika Atacama kubaki gizani ni rahisi, anasema mwanaastronomia Eduardo Unda-Sanzana wa Chuo Kikuu cha Antofagasta, ambaye amekuwa sauti muhimu ya wenyeji wa Chile katika kuonya kuhusu uchafuzi unaotokana na mwanga.

Tishio kwa sayansi ya anga

k

Chanzo cha picha, ESO/ P Horálek

Maelezo ya picha, Kuonekana kwa nyota angani usiku kunaweza kuwa na manufaa kwa ustawi wetu na pia kutusaidia kuelewa nafasi yetu katika Ulimwengu

Tishio kubwa kwa vituo vya uchunguzi vya Paranal na vingine ni viwanda, uchimbaji madini na vituo vya nishati vinazidi kukaribia.

"Tumekuwa tukifuatilia maendeleo ya uchafuzi wa mwanga kwa miaka mingi," anasema de Gregorio-Monsalvo, mwakilishi wa Eso nchini Chile. "Karibu miaka minne au mitano iliyopita, tuliona ongezeko la uchafuzi wa mwanga ambalo lilikuwa kubwa sana, huku viwanda vingi zaidi katika eneo hilo vikikaribia Paranal."

Kinachotokea Atacama kinaweza kuonekana kama tatizo la ndani, lakini kinaweza kuathiri uelewa wa wanadamu kuhusu ulimwengu.

Ingawa inawezekana kupeleka darubini angani ili kuepuka mwanga. Darubini ya Anga ya James Webb, kwa mfano, ni muhimu kwa uvumbuzi wake, lakini wanaastronomia pia wanahitaji durubini za rdhini. Darubini kubwa sana inayokuja - yenye kioo cha mita 39 (futi 128) - ni kubwa sana kuweka kwenye roketi.

Tukiacha mwanga wa nuru ya binadamu ufike mbali zaidi angani, si sayansi pekee itakayopoteza nafasi yake - wanaastronomia wanaonya kwamba tuna hatari ya kujitenga na galaksi na Ulimwengu tunaoishi ndani yake.

Giza la kweli linazidi kuwa gumu kupatikana. "Ni tatizo," anasema Unda-Sanzana. "Miaka hamsini iliyopita, kulikuwa na anga nyingi nyeusi duniani. Haya ni mazingira yaliyo hatarini kutoweka na tunakaribia kuyapoteza, ikiwa hatutayalinda. Hatutakuwa na mbadala ikiwa tutapoteza vita hivi."