Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Arsenal inatathmini uwezekano wa kumsajili Vinicius Jr

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Arsenal inafikiria uwezekano wa kumsajili winga wa Brazil, Vinicius Jr, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 asipoongeza mkataba wake na Real Madrid. (Athletic -usajili unahitajika)

Kocha mpya wa Real Madrid, Jose Mourinho, huenda akapinga jaribio lolote la Arsenal kumsajili Vinicius msimu huu wa joto, kwani kocha huyo raia wa Ureno ameuambia uongozi wa klabu kuwa anataka kusalia na wachezaji wake wote wakuu (Telegraph - usajili unahitajika)

Arsenal iko tayari kuvunja rekodi ya uhamisho nchini Uingereza ili kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez, mwenye umri wa miaka 26, kutoka Atletico Madrid. (Teamtalk)

Inter Milan ina nia ya kumsajili beki wa Argentina, Cristian Romero, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Tottenham. (Sky Sports)

RB Leipzig imekataa ofa ya pauni milioni 85.4 ya klabuya Real Madrid kwa ajili ya kumsajilia winga wa Ivory Coast, Yan Diomande. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 pia ananyatiwa na klabu za Liverpool na Manchester City, miongoni mwa nyinginezo. (Sky Sports)

Hatua ya Manchester United kutofanya uamuzi wake kuhusu hatma ya kiungo wa Ufaransa Manu Kone,25, kunaihangaisha klabu ya AS Roma. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)

Juventus inafikiria kumsajili nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, mwenye umri wa miaka 31, klabu hiyo ya Italia ikiwa tayari imefanya mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa Ureno. (Caught Offside)

Chelsea imekataa ofa ya tatu kutoka kwa klabu ya Como kwa ajili ya beki wa Uingereza, Trevoh Chalobah, mwenye umri wa miaka 27. (Talksport, kiungo cha nje)

Napoli ina nia ya kumsajili beki wa kati wa Chelsea na raia wa Ufaransa, Benoit Badiashile, mwenye umri wa miaka 25. (Sun, kiungo cha nje)

Julian Brandt amepokea ofa kutoka kwa Leeds United na Ajax baada ya kiungo huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 30 kuondoka Borussia Dortmund kama mchezaji huru. (Sky Sports)

Nottingham Forest imewasilisha ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 17.5 kumsajili beki wa Feyenoord na Uholanzi, Givairo Read, aliye na umri wa miaka 20. (Mail)

West Ham imekataa ofa kutoka Brentford kwa ajili ya beki wa kushoto wa Senegal, El Hadji Malick Diouf, na kusisitiza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hauzwi. (Talksport)

Middlesbrough ina nia ya kumsajili kipa wa Manchester United na Jamhuri ya Czech, Radek Vitek, mwenye umri wa miaka 22, ambaye msimu uliopita alikuwa klabu ya Bristol City kwa mkopo. (Sky Sports)