Wachezaji 7 wa Afrika wa kutazamwa katika Kombe la Dunia

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mataifa 10 kutoka bara Afrika yatashiriki michuano ya Kombe la Dunia, huku wachezaji wengi maarufu wakitarajiwa kushiriki.

Morocco waliweka historia miaka minne iliyopita nchini Qatar kwa kufika nusu fainali.

Cape Verde watakuwa wanashiriki mashindano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza, huku DR Congo wakirejea katika michuano hiyo tangu mwaka wa 1974.

BBC imewaangazia wachezaji saba kutoka Afrika ambao watatazamwa na kufuatiliwa sana katika mechi za kombe la dunia zitakazochezwa nchini Marekani, Mexico na Canada.

Antoine Semenyo (Ghana)

Mshambuliaji huyu mzaliwa wa London, ingawa hakushinda ligi kuu ya England kupitia klabu yake ya Manchester City, alifunga bao la ushindi katika fainali ya kombe la FA dhidi ya Chelsea mwezi uliopita.

Akiwa na umri wa miaka 26, mshambuliaji huyo amekuwa na rekodi nzuri kati ligi ya England.

Semenyo anategemewa sana na taifa lake wakati ambapo mwenzake Mohammed Kudus anayechezea Tottenham amepata jeraha.

Mchezaji huyu alishiriki katika kombe la dunia la mwaka 2022 akicheza zaidi kama mchezaji wa akiba.

Ghana itakutana na England, Croatia na Panama katika kundi L.

Yan Diomande (Ivory Coast)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Timu ya 'The Elephants' au Tembo inarejea tena kwenye mashindano ya kombe la dunia tangu mwaka wa 2014, huku wakiwa na mchezaji mdogo sana anayekipiga RB Leipzig katika ligi kuu ya Bundesliga, Ujerumani .

Katika umri wa miaka 19, alijishida tuzo ya kinda bora wa msimu, baada ya kufunga mabao 12 na kutoa pasi nane za mabao na kuisaidia timu yake ya RB Leipzigs kurejea kwenye michuano ya mabingwa Ulaya.

Uwezo wake wa mpira ulionekana katika mechi nne za kwanza za AFCON alizozicheza.

Timu ya Ivory Coast itakuwa ikishindana na Ujerumani, Ecuador kwenye kundi E

Ronwen Williams (Afrika Kusini)

Afrika Kusini inarejea kwenye mashindano ya kombe la dunia tangu kuwa mwenyeji wa mashindano hayo mwaka wa 2010.

Hii ni hatua kubwa kwa timu ya Bafana Bafana baada ya kuondolewa kwenye hatua ya mchujo mwaka 1998 na 2002.

Akiwa na umri wa miaka 34, mchezaji huyo amepata uzoefu baada ya kushinda kombe la ligi ya mabingwa Africa akiwa na timu yake ya Sundwons.

Kwenye kombe la dunia Afrika kusini imepangw akundi moja na Mexico, Jamhuri ya Czech na Korea Kusini.

Roberto "Pico" Lopes (Cape Verde)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki huyo wa kati alikuwa nyota muhimu kwa kuisaidia timu ya Cape Verde, ambayo ilifika robo fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 .

Cape Verde inakabiliwa na kibarua kigumu katika Kundi H, ambako itachuana na mabingwa wa zamani wa Kombe la Dunia, Hispania na Uruguay, pamoja na Saudi Arabia.

Brahim Diaz (Morocco)

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alichezea Morocco katika fainali za AFCON 2025, na kufunga mabao matano yaliyowasaidia wenyeji Morocco kufika fainali.

Timu ya The Atlas Lions watakutana na Brazil, mabingwa mara tano wa michuano hiyo, katika mechi yao ya kwanza ya Kundi C, kabla ya kucheza na Scotland na Haiti.

Ismaila Sarr (Senegal)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Akiwa na umri wa miaka 28, yuko katika kwneye kiwango bora cha kufunga mabao, akiwa na rekodi binafsi ya mabao 21 aliyofungia Crystal Palace msimu huu katika mashindano yote.

Tisa kati ya mabao hayo yalifungwa katika michuano ya Europa Conference League, yakisaidia "The Eagles" kushinda taji lao la kwanza kabisa la Ulaya.

Hii itakuwa kombe la tatu la dunia ambalo Sarr anashiriki baada ya Senegal kutolewa katika hatua ya makundi mwaka 2018 kwa kutumia kanuni ya fair play, kabla ya kupigwa 3-0 na England katika hatua ya 16 bora miaka minne baadaye.

Simba wa Teranga ambao wanajivunia kuwa mabingwa wa Afrika, watakutana na Ufaransa, mabingwa mara mbili wa dunia, Norway ya Erling Haaland, na Iraq katika Kundi I.

Omar Marmoush (Misri)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji huyo ambaye amecheza mechi nane za Ligi Kuu ya England akiwa na Manchester City msimu wa 2025–2026, ni miongoni mwa wachezaji wa kwanza kutajwa katika kikosi cha taifa cha Misri.

Marmoush alifunga mabao mawili katika mechi za AFCON 2025 ambapo timu hiyo ya Afrika Kaskazini ilitinga nusu fainali, na sasa atakuwa anashiriki katika Kombe lake la Dunia la kwanza wakati Mohamed Salah wa Liverpool akiwa ndiyo anarejea baada ya kupata jeraha.