Mwanamke tajiri zaidi Australia agawa utajiri wake

    • Author, Lana Lam Sydney
    • Nafasi, BBC
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Mahakama nchini Australia imetoa uamuzi katika mzozo mkubwa kuhusu utajiri unaotokana na madini wa Gina Rinehart, mtu tajiri zaidi nchini humo, kuwa lazima agawe baadhi ya utajiri wake.

Ana utajiri wa thamani ya takriban dola bilioni 38 (£20bn; $27bn), Rinehart alirithi miradi ya uchimbaji madini ya chuma ya baba yake mwaka 1992, kabla ya kuiendeleza katika mgodi wa eneo la Pilbara lenye utajiri wa madini la Western Australia (WA).

Watoto wawili na warithi wa mshirika wa kibiashara wa marehemu baba yake wanasema wana haki ya kupata ya mirabaha na haki za uchimbaji madini.

Siku ya Jumatano, zaidi ya miaka 13 baada ya vita vya kisheria kuanza, jaji wa Mahakama Kuu alitoa uamuzi kwamba Rinehart lazima alipe mirabaha ya zamani na ya baadaye kwa warithi hao lakini haki za uchimbaji madini zinabaki kuwa zake.

Mzozo huo wa kisheria unatokana na mradi wa Hope Downs, mojawapo ya miradi mikubwa na yenye faida kubwa zaidi ya madini ya chuma nchini Australia.

Mahakama ilielezwa kuwa baba yake Rinehart, Lang Hancock, na mshirika wake wa kibiashara, Peter Wright - ambao ndio waanzilishi wa uchimbaji wa madini ya chuma huko WA - waliandika makubaliano ya kusimamia maslahi yao ya pamoja chini ya biashara inayoitwa Hanwright.

Wakati wa kesi ya siku 51 mwaka 2023, watoto wa Wright walidai Rinehart alivunja makubaliano hayo, na alikuwa na deni la haki zao za uchimbaji madini na mirabaha inayotokana na Hope Downs.

Eneo hilo linaendeshwa kwa pamoja na kampuni kubwa ya uchimbaji madini duniani Rio Tinto na Hancock Prospecting, na mwaka jana walitumia dola milioni 832 katika hazina ya kampuni ya Rinehart.

Rio Tinto inalipa 2.5% ya mrabaha kwa Hancock Prospecting, huku Jaji Jennifer Smith ameamua kwamba nusu ya malipo hayo ni ya familia ya Wright.

Hukumu

"Wright Prospecting imeshinda nusu ya kesi hiyo, ikipoteza nusu ya kesi, na Hancock Prospecting... imeshinda nusu na kupoteza nusu ya kesi yake," anasema Smith.

Kesi hiyo ya kisheria pia iliwahusisha watoto wawili wa Rinehart - Bianca Rinehart na John Hancock - ambao walidai mama yao amehamisha haki za uchimbaji madini kutoka amana ya familia hadi sehemu ya biashara ambayo hawakuweza kuigusa.

Wawili hao walisema babu yao alikuwa na nia ya kuwapa sehemu ya utajiri kutokana na migodini ya Hope Downs lakini Rinehart aliwanyima kwa makusudi fursa ya kupata utajiri huo.

Mawakili wa Rinehart walidai amehamisha haki za uchimbaji madini kutoka katika amana ya familia baada ya kuwa na mashaka na shughuli za baba yake za kibiashara, lakini watoto wake walidai alifanya hivyo ili kuficha pesa kutoka kwa mke wake wa pili na mfanyakazi wa zamani wa nyumba Rose Porteous.

Ingawa madai ya watoto wa Rinehart kuhusu haki hizo yalikataliwa, zabuni nyingine ya mirabaha kutoka Hope Downs na familia ya marehemu mhandisi Don Rhodes yalikubaliwa kwa kiasi.

Mkurugenzi mtendaji wa Hancock Prospecting, Jay Newby, alikaribisha uamuzi wa mahakama, akisema ulithibitisha umiliki wa kampuni hiyo ya Hope Downs na "kukataa vikali" madai ya familia ya Wright na watoto wawili wa Rinehart.

Msemaji wa Wright Prospecting pia alikaribisha uamuzi huo, akisema "wamefurahi na uamuzi huo.”

Rinehart ni mmoja wa wafadhili wakubwa Australia wa michezo, mashirika ya kutoa misaada na vyama vya siasa vya kihafidhina.