Tazama taharuki na namna Trump alivyoondolewa kwenye shambulio Washington

Tazama taharuki na namna Trump alivyoondolewa kwenye shambulio Washington

Rais wa Marekani Donald Trump aliondolewa haraka na kupelekwa mahali salama kutoka kwenye hafla ya Waandishi wa habari wa Ikulu baada ya milio ya risasi kusikika katika eneo la tukio.

Rais huyo na Mke wa Rais Melania Trump walionekana wakiwa katikati ya mazungumzo katika Hoteli ya Washington Hilton kabla ya kukatizwa na taharuki iliyotokea.

Milio mikubwa ya mlipuko ilisikika, kisha maafisa wa usalama wakamtoa rais kwa haraka kutoka eneo la tukio huku wakipiga kelele "lala chini, lala chini."

Mamlaka za usalama ziilithibitisha baadaye kuwa rais, mkewe na watu wote wanaolindwa walikuwa salama, baada ya milio ya risasi saba hadi nane kufyatuliwa.

Zaidi unaweza kufuatilia hapa chini: