Mojtaba Khamenei: Kwa nini kiongozi wa kidini wa Iran haonekani hadharani?

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 4

Mojtaba Khamenei haonekani popote wala hasikiki. Imepita zaidi ya miezi 4 tangu ateuliwe kuwa kiongozi mpya wa kidini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kifo cha baba yake, lakini hadi sasa kiongozi huyo mpya hajaonekana kwenye televisheni, kwenye vyombo vya habari, au kuhudhuria mikutano yoyote ya umma.

Kuna barua zimetoka zikihusishwa na yeye, lakini hakuna anayejua alipo. Hakuna mtu aliyesikia sauti yake, hakuna mtu aliyeona picha yake, hakuna mtu aliyeona barua iliyoandikwa kwa mwandiko wake.

Kuna uvumi mwingi kuhusu yeye. Hata Donald Trump amependekeza kwamba huenda tayari amekufa. Nchini Iran, ni Rais Masoud Pezeshkian pekee ndiye aliyesema amemwona. Maafisa wa serikali wanasema kiongozi huyo mpya wa kidini amekataa kuhudhuria mazishi ya babake kwa sababu za kiusalama.

Mohammad Mehdi Mirbagheri, mmoja wa wasomi wakubwa wa Iran na mjumbe wa Bunge la Wanazuoni na kiongozi wa chama cha Paydari, ambaye anasema kutokuwepo kwa Mojtaba Khamenei ni jambo la kawaida katika utawala wa Washia.

Usiri katika historia ya Ushia

m

Katika kipindi cha miaka 47 iliyopita, masuala mengi ya kidini na kisiasa yameibuka ambayo yamehusishwa na imani "za siri".

Hadithi ya Imamu wa 12 wa Washia inasema kwamba baada ya kifo cha Imamu Hassan al-Askari mnamo 260 AH, mwanawe Muhammad bin Hassan, Imamu wa 12 wa Washia, alitoweka hadharani.

Washia wanaamini kwamba mwanzoni huyo aliwasiliana na wafuasi wake kupitia wawakilishi 4 maalum kwa kipindi cha miaka 70.

Wasomi wengi wa historia ya Kiislamu wanakubali kwamba usiri wa Imam wa Kishia hauishii tu kwenye masuala ya dini. Baadhi wanaamini unahusiana pia na changamoto ya uongozi.

Baada ya kifo cha Imamu wa 11 wa Uislamu wa Shia, wafuasi wa imani hiyo walianza kufikiria jinsi ya kuendeleza mfumo wa Uimamu. Hivyo, Ghaiba/usiri ulipitishwa ili kutawala nchi kwa jina la Imamu akiwa hayupo.

Kulingana na mwanahistoria wa Kiislamu wa Ujerumani Wilfred Madelung, matumizi ya Ghaiba au mfumo wa usiri ni "njia ya kuepuka chochote ambacho kingeweza kuharibu utamaduni wa Uimamu wa Kishia". Hatua kwa hatua ikawa nguzo ya Imam wa 12 wa Kishia.

Uundaji wa Baraza la Shura

n

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ingawa wale wanaoamini katika ghaibu ya Imam wa 12 wa Kishia wamekubaliana kwamba kiongozi wao hataonekana hadharani, hiyo haimaanishi kwamba uongozi wake haupo.

Tangu ghaiba ianze kufanya kazi, swali linalowakabili Mashia limekuwa, wakati Imam hayupo, ni nani atakayetoa hukumu kuhusu masuala ya kidini na kutoa fatwa kuhusu masuala ya kijamii?

Polepole, jibu la swali hilo lilifungua njia ya kuundwa kwa Baraza la Shura. Hapo awali, kazi yao ilikuwa ni utekelezaji wa hukumu na utunzaji wa mambo ya kidini, lakini polepole nguvu yao iliongezeka.

Hatua kwa hatua, wakawa watawala, majaji, na wasimamizi wa masuala ya kidini, wakati mwingine hata masuala ya kisiasa.

Mfumo huu uliingia katika awamu mpya katika karne ya 20. Mapinduzi ya 1979 yalileta mabadiliko mengi.

Ruhollah Khomeini alitangaza kwamba wajumbe wa Baraza la Shura wana mamlaka ya kuunda serikali wakati wa kipindi kiongozi akiwa mafichoni.

Alisema, "Wajumbe wa Baraza la Shura wana mamlaka ya kuanzisha serikali."

Baada ya hapo, maamuzi juu ya serikali ya Jamhuri ya Kiislamu hutoka kwa chanzo kingine kisichokuwa Imam mkuu aliyejificha. Hivyo, suala la Imam aliyejificha wa Shia haliishii tu kwenye dini, huingia kwenye siasa pia.

Hata hivyo, kutokuwepo kwa Khamenei kunaweza kuwa kwa muda mfupi. Inaweza kuwa ni hatua ya usalama kutokana na hali ilivyo sasa.

Lakini ikiwa itaendelea hivi, au ikiwa imekusudiwa kuwa ni hali ya kudumu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itakabiliwa na tatizo kubwa kama lile ambalo Taliban walikabiliana nalo walipoficha kifo cha Mullah Omar. Hili lilisababisha kuporomoka kwa kundi hilo.