Mambo matano makubwa katika ripoti ya matukio ya Oktoba 29 Tanzania

Hatimaye kile klichokuwa kikusubiriwa kwa muda mrefu, sasa tayari kiko hadharani. Ripoti ya tume iliyoundwa na serikali kuchunguza matukio ya vurugu ya wakati na baada ya uchaguzi imewasilishwa kwa rais siku ya leo.
Kwa muda wote huo kulikuwa na idadi ya vifo na mejurudi kwa mujibu wa mashirika ya haki za binadamu na vyama vya kisia, sasa serikali ya Tanzania imekuja na majibu yake ya juu ya kile kilichotokea Oktoba 29, kuhusu vifo, mejeruhi na uharibifu.
Ni ripoti iliyokusanywa kwa miezi kadhaa chini ya Mwenyekiti Jaji Mohamed Chande, ambayo imewahoji maelfu ya watanzania, imetumia picha na video za wakati wa Oktoba 9 na siku zilizofua. Katika ripoti hii kuna mambo makubwa matano ya kuyazingatia.
Chanzo cha ghasia
Jaji Chande ametaja sababu za kisiasa, ikiwemo madai ya Tume huru ya uchaguzi, changamoto za kiuchumi ajira ugumu wa maisha, kijamii kama vile kukosekana kwa uzalendo kuwa miongoni mwa vyanzo vya ghasia za uchaguzi wa Oktoba 29.
Masuala ya kisasa ikiwemo madai ya katiba mpya, maboresho ya tume huru ya uchaguzi. Masuala ya kijamii, ukosefu wa ajira, maisha magumu na mazingira ya kibiashara, utitiri wa kodi, Masuala ya kijamii yanayohusisha mmonyoko wa maadili na kukosa uzalendo na kutokushughuliwa kwa madai ya rushwa, kupotea na kutekwa kwa watu
Pia, Utendaji wa wafayakazi wa umma. Uhusiano wa kimataifa - Tume inasema kumekuwa na mkakati wa jamiiya kimataifa kuingilia maswala ya ndani ya Tanzania.
Lengo la ghasia
Tume imetaja malengo matatu ya vurugu hizo. Moja ikiwa ni kuzuia uchaguzi. Lengo hili linathibitshwa na matukio mbali mbali, ikiwemo kushambulia askari, mawakala na wasimamizi wa uchaguzi, kuharibu mali za wasimamizi, vitisho, kuvamia vituo vya uchaguzi, kupora mali, kutishia waliojitokeza kupiga kura na waliopiga kura kukakwa au kujaribiwa kukatwa vidole.
Lengo jingine ni kufikisha ujumbe. Tume inasema miongoni mwa walioshiriki katika vurugu ilikuwa ni kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa serikali, tume inasema vijana walioshiriki walipata mwanya wa kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa wanataka kusikilizwa.
Na jambo la mwisho ni uporaji. Miongoni mwa wafanya ghasia, walijitokeza makundi ya waliopora mali na kuiba. Uporaji ulitokea katika maduka na maeneo mengine ya biashara yaliyotembelewa na tume.
Idadi ya waliokufa na kujeruhiwa

Takriban watu 518 waliuawa wakati wa machafuko ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025 nchini Tanzania, tume ya uchunguzi ya serikali imebaini.
Huku idadi ya waliofariki wakati wa vurugu ikiwa ni watu 518, idadi ya waliofariki wanaume 490 sawa na asilimia 94.6, na wanawake 28, sawa na asilimia 5.4.
Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa waliofariki ukiwa na vifo 182, Mwanza 90, Mbeya 80 na Arusha 53. Na 21 viikuwa vifo vya watoto. Na vifo 16 walikuwa askari na maafisa wa usalama.
Hadi kufikia tarehe 31 Machi 2026, majeruhi waliokuwa wamehudumiwa katika vituo vya afya vya umma na binafsi walikuwa ni 2,390, kati yao raia ni 2,270 na maafisa na maaskari wa vyombo vya ulinzi na usalama 120.
Tume imesema idadi hyo inaweza kuwa kubwa zaidi kwani Tume kuwa kuna uwezekano kuwa badhi ya familia zimezika wapendwa wao bila kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ya afya au hawakupata fursa ya kuja mbele ya tume.
Kiwango cha hasara
Tume imebaini kutoka vyanzo mbali mbali kuwa mali za watu binafsi na serikali zilizoharbiwa zina thamani ya shilingi za Kitanzania 125 bilioni, mali za sekta binafasi au watu binafsi zina tahamai ya blioni 89. Na mali za umma au serikali ni shilingi bilioni 36.
Mwenyekiti wa Tume amesema uchunguzi wa tume hiyo ilihusisha maeneo 202, katika wilaya 22 na mikoa 11. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Mbeya, Songwe, Mwanza, Geita, Arusha, Iringa, Dodoma, Shinyanga, Mara na Ruvuma.
Mapendekezo

Chanzo cha picha, Getty Images
Tume imetoa mapendekezo mengi ambayo yamegawika katika aina kadhaa, yale yanayohusu maridhiano ya kitaifa, kushughulikia kero za vijana hasa katika masuala ya uchumi na keroa za vyama vya siasa hasa katika masuala ya Katiba mpya ya tume ya uchaguzi.
Pia serikali na vyombo vya dola vimetakiwa kusimamia uadilifu na demokrasia ili kuepusha sintofahamu na jamii. Vilevile, tume imeitaka serikali kuunda tume ya jinai ili kushughulikia tuhuma zinazohusu Polisi kuuawa watu katika majumba yao, na matukio mengine ya jina.















