'Chombo kitakachoundwa kitaangazia taarifa za wanaodaiwa kutekwa ambao bado hawajapatikana'
Rais Samia amesema chombo maalum cha upelelezi kitakachoundwa kwa ajili ya kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na tume kitajielekeza kuangazia masuala kadhaa ikiwemo masuala ya wanaodaiwa kutekwa ambao taarifa zao bado hazijapatikana.
Aidha chombo hicho kitaangalia na kubaini waliohusika kuratibu kupanga na kufadhili matukio ya ghasia za Oktoba29.
'Vilevile watajielekeza kubaini matukio ya vurugu na uhalifu,kwa bahati nzuri picha zipo'alieleza
Pia chombo hicho kitaangazia miili ambayo haijapatikana na walioathirika nje ya maeneo ya vurugu.





