Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya: Madrid kutoa ofa ya dunia kwa Oliseh
Real Madrid itawasilisha ofa ya pauni milioni 130 kwa winga wa Bayern Munich na Ufaransa, Michael Olise (24), iwapo Florentino Perez atachaguliwa tena kuwa rais wa klabu hiyo. (Telegraph)
Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Arne Slot, ambaye alitimuliwa wiki iliyopita, ameikataa ofa ya Fulham ambayo inatafuta mrithi wa Marco Silva. (Talksport)
Jaribio la Barcelona la kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Julian Alvarez, limegonga mwamba. Atletico Madrid inaendelea kupanga kikosi chake ikiwa na nyota huyo, huku Arsenal ikitajwa kumtaka lakini mchezaji huyo hataki kuhamia London. (Cadena Ser)
Mshambuliaji wa Chelsea, Liam Delap (23), anaweza kujiunga na Fulham ikiwa Kieran McKenna atateuliwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo. (Talksport)
Aliyekuwa kocha wa Crystal Palace, Oliver Glasner, anaongoza katika mbio za kuwa kocha mpya wa AC Milan mbele ya Mauricio Pochettino. (Gazzetta dello Sport)
Winga wa AC Milan, Rafael Leao (26), amesema anahitaji changamoto mpya na anaamini Ligi Kuu England au La Liga zitakuwa hatua nzuri kwake. (Sport TV kupitia Football Italia)
RB Leipzig inaamini mshambuliaji wa Ivory Coast, Yan Diomande (19), atasalia klabuni hapo licha ya Liverpool kuongeza juhudi za kumuwania. (Teamtalk)
Newcastle United ipo karibu kukamilisha usajili wa kwanza wa majira ya joto baada ya kukubaliana dau la pauni milioni 24 kwa ajili ya kipa wa Reims, Ewen Jaouen (20). (Northern Echo)
Meneja wa Tottenham, Roberto De Zerbi, anadaiwa kutaka beki wa Croatia, Luka Vuskovic (19), aondoke klabuni msimu huu wa joto. (Football Insider)
Hull City inachunguza uwezekano wa kumsajili winga wa Venezuela, Luis Fernando Carrero (19), kutoka Deportivo Tachira kabla ya kumpeleka kwa mkopo NK Maribor. (Sky Sports)
Everton imewasiliana na Middlesbrough kuhusu kiungo wa England, Hayden Hackney (23), lakini bado iko mbali na kiwango cha fedha kinachotakiwa na Boro. (Teesside Live)
Barcelona inaweza kumfuata beki wa Chelsea, Marc Cucurella (27), iwapo itaamua kumuuza Alejandro Balde (22) katika dirisha hili la usajili. (Marca)