WARIDI WA BBC: ''Ninajichoma sindano ya kisukari popote''

b
Maelezo ya picha, Lucy Lymo hujichoma sindano mara nne kwa siku ili kudhibiti sukari yake
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Fikiria kwa miaka 12 tangu uzaliwe unakula kila kitu, inatokea ghafla tu unagundulika kuwa na changamoto ya kisukari aina ya kwanza na kutakiwa kubadili kabisa mlo wako na kuanza kula kwa masharti na uangalifu.

nilikuwa naumwa sana nikalazwa kwa kula vitu ambavyo sitakiwi kula.

'Haikuwa rahisi mwanzoni nilikuwa ninajificha na kula chipsi, kunywa soda lakini sikuacha kutumia dawa zangu' anasimulia Lucy Lymo 31 aliyejipambanua katika mitandao y akijamii kama muelimishaji wa ugonjwa wa kisukari baada ya kuugua ugonjwa huo kwa takriban miaka 20 sasa.

Lucy anasema miongoni mwa dalili alizoanza kupata ni pamoja na kujiskia kiu mara kwa mara, nilipenda sana kunywa maji mengi na vinywaji vyenye sukari, kupata njaa kali na Kwenda haja ndogo mara kwa mara.

Sisimizi walifuata mkojo wangu

Lucy anasimulia kwamba siku moja marehemu baba yake alikuta msusuru wa sisimizi wakiufuata mkojo wake kutoka nje ya mlango wa choo hadi chini ya kitanda nilichokuwa analala.

Wakati mwingine nilijisaidia haja ndogo kabla ya kufika chooni, na wakati mwingine kitandani,hata mimi ilinishangaza kwanini ninashindwa kuzuia haja ndogo? Alisaili Lucy

'Baba alisema ninahisi tuna mgonjwa wa kisukari humu ndani'

Wazazi walichukua hatua ya kunipeleka hospitali ya mwananyamanala jijini Dar es salaam hapo ndipo nilipogundulika kuwa kweli nina kisukari aina ya kwanza.

Ninakumbuka nilidhoofu kiasi kwamba safari ya kutoka nyumbani hadi kituo cha kupata usafiri nilitumia nusu saa badala ya dakika 10. Nilikuwa ninasiki akuchoka na kuishiwa nguvu, hadi nipatiwe kinywaji chenye sukari.

Wataalamu wa afya walichukua sampuli ya haja ndogo na Kwenda kupima baadae tulipewa majibu kwamba ninaugonjwa wa kisukari.

'Mama yangu alilia mbele yangu' nilikuwa mdogo kwahiyo nilililia pia lakini niliweza kuichukulia kawaida baadae kiasi kwamba hata wadogo zangu nao walichukulia kawaida tun a kuwa msaada kwangu tangu hapo.

Nilianza maisha ya masharti huku nikiendelea na masomo yangu ya sekondari. Wakati wote niliendelea kuheshimu masharti ya chakula huku siku nyingine nikishindwa na kula vibaya na kusababisha kuugua hadi kulazwa.

Mgonjwa wa kisukari anaweza kufurahia maisha na kutimiza ndoto zake kama mtu mwingine

s

Chanzo cha picha, Lucy Lymo

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Anasema ni vema jamii iachane na fikra potofu kuhusu ugonjwa huu na kuwa msaada kwa wagonjwa badala ya kuwakatisha tamaa ya kuishi.

Lucy anasema alisoma shahada ya masuala ya Bima na kufaulu vizuri na baadae kuajiriwa katika taasisi moja ya serikali nchini Tanzania.

Hadi kufika sasa nimeamini kwamba inawezekana kusoma kufaulu na kuajiriwa licha ya kuwa na changamoto hii ya kiafya.

'Kumbe mjamzito, uwe makini na sukari yako'

Mimi nimeolewa na nina mtoto mmoja wa kike, ninakumbuka safari yangu ya ujauzito haikuwa rahisi pia.

Wakati unapambana na kisukari,unakutana na baadhi ya watu wanakuambia kauli kama 'hee kumbe unaweza kushika mimba na kisukari chako', wewe mjamzito uwe makini na unakisukari..lakini hata baada ya kujifungua niliambiwa mgonjwa wa kisukari kumbe unaweza kujifungua? Haya yote yaliniumiza wakati mwingine lakini niliyapuuza na kuelewa kuwa watu wengi bado hawana elimu kuhusu ugonjwa huu.

Katika kipindi cha ujauzito Lucy anasema alizingatia masharti na taratibu alizopewa na wataalamu wake wa afya katika kutunza ujauzito na kuijali afya yake.

Haikuwa rahisi zipo nyakati nilikuwa nalia sana kutokana na hofu ya ugonjwa niliokuwa nao,niliogopa kujifungua mtoto mwenye kasoro au mfu au hat akupoteza maisha wakati wa kujifungua.

Nilijifungua salama kwa msaada wa wataalamu na mtoto hakuwa na changamoto yoyote.

Anasema wake alijifunza jinsi ya kumuhudumia kwa tahadhari inapotokea sukari imeshuka au kupanda.

Anajua nini cha kufanya ili kunisaidia na zaidi ya yote huniwekea pipi,biskuti au kinywaji kwenye gari ili nitumie ninapojiskia hali y akushuka kwa sukari.

'Nilichapisha mtandaoni ili kumtia moyo mtu mmoja aliyekata tamaa'

s

Chanzo cha picha, Lucy Lymo

Maelezo ya picha, Lucy Lymo

Haikuwa rahisi hapo kwanza,anasimulia Lucy huku akitabasamu.

Anasema alitamani sana kuanza kutoa elimu na kuzungumza na jamii kupiti aukurasa wake wa Instagram ambao haukuwa na wafuasi wengi,lakini lengo lake lilikuwa kumpata mtu mmoja tu ambaye atapata faraja kwa kupitia simulizi yake.

Niliingia mtandaoni siku hiyo nikaanza tu kusema leo nitazungumzia ugonjwa huu na namna ninavyojijali kwa kuchoma sindano na kutumia daw ana kufuata masharti sahihi ili kutunza afya yangu. NIkachapisha video nikijichoma sindano.

Nilishangaa sana nilipoamka kesho yake nilikuta nimepata wafuasi elfu mbili kutoka mia saba niliokuwa nao mwanzo.

Wafuasi wengi walipenda maudhui yale na kushiriki na kuniandikia maoni mengi yaliyonitia moyo na mengine kunibeza.

Alipokea kwa furaha sana wale waliomuandikia kuwa wanafarijika na kumuliza maswali kuhusu ugonjwa huo.

Kuna wale waliobeza kuwa ninatafuta umaarufu mtandaoni hao nilielewa tu kuwa bado kunahitajika elimu zaidi kwa jamii.

Hii imenifundisha kuwa si vizuri kuwa mwepesi kumsemea vibaya mtu usiyemjua kwanini yupo hivyo, ni heri kunyamaza.

Kupitia mitandao ya kijamii Lucy, mwenye furaha na bashasha amekuwa akichapisha matukio kama akiwa harusini, akiwa klabu akicheza muziki na marafiki na kujichoma sindano yake bil akujali umati wa watu.

Lucy anasema anatamani kuona mamlaka ya afya ikiangalia kwa makini matibabu ya kisukari kwani kuna utaratibu wa kujigharamia kila mgonjwa aliyefikisha umri wa miaka 25.Anasema watu wengi hawana uwezo wa kujihudumia kutokana na

Ninatamani mamlaka iruhusu dawa za sukari kupatikana bure. Nikiwa mtoto nilipata dawa bure zilizokuwa zinaletwa kwa misaada na kutolewa bure lakini ukishafika miaka 25 unapaswa kulipia.

Wanaamini ukishafika umri huo unaweza kujilipia. Ukiangalia watu wengi wanatoka familia duni wanashindwa kupata matibabu,hii inaathiri nguvu kazi ya taifa kwani watu wasiopata matibabu sahihi wanashindwa kuzalisha kwa manufaa ya taifa.