Moja kwa moja, Maandamano ya kupinga wahamiaji Afrika Kusini yashuhudiwa, raia wawili wa Nigeria waripotiwa kufa

Maandamano ya “March and March Movement,” yanayopinga uhamiaji yamefanyika mjini Pretoria, mojawapo ya miji yenye wahamiaji wengi nchini Afrika Kusini.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi & Beldeen Waliaula

  1. Mfalme Charles III kuhutubia bunge la Congress nchini Marekani

    Picha ya Mfalme Charles III na Donald Trump

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Picha ya Mfalme Charles III na Donald Trump

    Hii leo ni siku ya pili ya ziara ya siku nne ya Mfalme Charles III na Malkia Camilla nchini Marekani.

    Wafalme hao watahudhuria hafla ya kijeshi katika ikulu ya White House kabla ya kufanya mkutano na Rais wa taifa hilo Donald Trump.

    Mfalme Charles III, anatarajiwa kuandikisha historia, kuwa kiongozi wa pili wa kifalme kutoka Uingereza kulihutubia bunge la Marekani la Congress, baada ya mamayake Malkia Elizabeth II, kufanya hivyo mwaka wa 1991.

    Hotuba ya mfalme Charles III inatarajiwa kusema kuwa “mara kwa mara nchi zetu mbili zimekuwa zikipata njia za kuja pamoja na kushirikiana”

    Ziara ya Mfalme Charles III, inajiri wakati kumekuwa na mvutano kati ya Uingereza na Marekani kuhusu vita vya Iran, na inatarajiwa kuwa ziara ya mfalme itasaidia kutatua mvutano huo na kurekebisha uhusiano wa Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Donald Trump.

    Kwa picha: Mfalme Charles III na Malkia Camilla walipowasili nchini Marekani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Pia unaweza kusoma:

  2. Ukraine yaishtumu Israel kwa kupokea shehena ya nafaka 'iliyoibwa' na Urusi

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Ukraine imesema kuwa meli iliyokuwa imebeba nafaka kutoka eneo linalokaliwa na Urusi ilikuwa inajiandaa kupakua shehena hiyo katika bandari ya Haifa nchini Israel.

    Mvutano wa kidiplomasia umeibuka kufuatia madai kuwa Israel imekuwa ikipokea shehena za nafaka kutoka maeneo ya Ukraine yanayodhibitiwa na Urusi.

    Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa “meli nyingine” iliyobeba nafaka “iliyoibwa na Urusi” imewasili katika bandari ya Israel na inajiandaa kupakua shehena hiyo.

    Zelensky alisema kuwa mamlaka za Israel “haziwezi kuwa hazijui” kuhusu shehena zinazowasili katika bandari za nchi hiyo, na kusema kuwa kushindwa kuzuia usafirishaji wa nafaka zinazoibwa na Urusi, kunadhoofisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili.

    Waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Gideon Saar, aliikosoa Ukraine kwa kutoa madai kama hayo hadharani, akisisitiza kuwa “hakuna ushahidi” ila suala hilo litachunguzwa.

    Msemaji wa ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, aliwaambia waandishi wa habari kuwa “angependa kutozungumzia kabisa suala hilo au kujihusisha nalo.”

    Urusi imekuwa ikikanusha madai kwamba inaiba nafaka ya Ukraine.

    Pia unaweza kusoma:

  3. Kiongozi wa genge la kuuza dawa za kulevya la CJNG nchini Mexico akamatwa

    Picha ya Flores akiwa amekamatwa

    Chanzo cha picha, SEMAR via REUTERS

    Maelezo ya picha, Picha ya Flores akiwa amekamatwa

    Vikosi vya usalama nchini Mexico vimemkamata mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la Jalisco New Generation Cartel(CJNG).

    Audias Flores Silva ambaye pia anajulikana kama “El Jardinero” au “The Gardener” alipatikana akiwa amejificha katika handaki moja, baada ya kuzingirwa na maafisa 500 wa usalama siku ya Jumatatu.

    Maafisa hao walisema kuwa Flores, mwenye umri wa miaka 45, alikuwa mshirika wa karibu wa mtu aliyekuwa akitafutwa sana nchini Mexico, Nemesio “El Mencho” Oseguera, ambaye alifariki miezi miwili iliyopita.

    Flores alikuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa kundi la CJNG ambao walitarajiwa kumrithi El Mencho, ambaye alikuwa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya.

    Tofauti na El Mencho ambaye alifariki kutokana na majeraha baada ya kupambana na maafisa wa usalama akizuia kukamatwa kwake, Flores hakupigana na maafisa hao.

    Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilikuwa imetangaza zawadi ya dola million tano kwa yeyote atakaye mkamata.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Maandamano ya kupinga wahamiaji Afrika Kusini, yasababisha vifo vya raia wawili wa Nigeria

    Maandamano Afrika Kusini

    Chanzo cha picha, Thuthuka Zondi/BBC

    Maelezo ya picha, Maandamano Afrika Kusini

    Maandamano ya “March and March Movement” inayopinga uhamiaji nchini Afrika Kusini yamefanyika mjini Pretoria.

    Maandamano hayo yametokea baada ya mfululizo wa visa vya kuwashambulia wahamiaji maarufu kama xenophobia, wakiwalenga raia wa kigeni nchini humo.

    Waaandamanji hao walikuwa wamebeba fimbo na mabango yaliyoandikiwa “tutaandamana hadi tushinde. Kama kupigania nchi yangu inanamaanisha mimi ni mbaguzi, basi najivunia kuwa hivyo”

    Ingawa sababu kamili ya maandamano hayo haijatolewa, maandamano sawia ya awali yalikuwa yakuwashinikiza raia wa kigeni waondoke nchini humo.

    Maandamano haya yametokea baada ya vifo vya raia wawili wa Nigeria.

    Pia unaweza kusoma:

  5. "Nilinukuliwa vibaya", Rais Ruto asema kuhusu Kiingereza cha Nigeria

    Rais wa Kenya,William Ruto

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya,William Ruto

    Rais wa Kenya Wiliam Ruto, amepuuzia matamshi yake ya awali aliposema kuwa Wanaigeria hawajui kiingereza, akidai kuwa alinukuliwa vibaya na kauli zake zilichukuwa nje ya muktadha.

    Ruto alitoa ufafanuzi huo hii leo katika kongamano la kuwekeza katika madini inayoendelea mjini Nairobi, baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Nigeria Yusuf Tuggar.

    Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya, Ruto alimwambia Tuggar afikishe salamu zake kwa Rais Bola Tinibu na “watu wazuri wa Nigeria ambao pia ni wakwe zangu”

    “Nilirekodiwa nikizungumza na wananchi, ilikuwa mazungumzo ya faragha ila mtu akaamua kuyaweka hadharani. Walitafsiri vibaya maneno yangu. Ukweli ni kwamba nilikuwa nikizungumza kuhusu jinsi sisi tulio bara Afrika tunazungumza Kiingereza kizuri” Alisema Ruto.

    Awali katika kongamano tofauti, Rais William Ruto alikuwa amekejeli Kiingereza cha Nigeria kwa kusema “elimu yetu ni nzuri,tunazungumza Kiingereza kizuri. Ukimskiza Mnaigeria akiongea utashangaa anasema nini, utahitaji mkalimani hata kama wanazungumza Kiingereza.”

    Video hiyo ilisambaa mitandaoni na kukashifiwa vikali.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Marekani 'inadhalilishwa' na Iran - Kansela wa Ujerumani

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz

    Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, amesema kuwa Marekani ‘inaiaibishwa’ na Iran, akidai kuwa Iran imeishinda maarifa utawala wa Trump ikija katika suala la kufanya mazungumzo.

    Siku mbili zilizopita Trump alihairisha safari ya ujumbe wa Marekani kuelekea mjini Islamabad, Pakistan, kufanya mazungumzo na Iran. Duru ya kwanza ya mazungumzo hayo yalioongozwa na naibu wa rais wa Marekani JD Vance yaliambulia patupu.

    Merz amesema upande wa Trump ndio ‘unachezewa’.

    “Wairani wako na ujuzi ikija katika suala la kufanya mazungumzo au labda pia hawana ujuzi huo kwa kuwaruhusu wajumbe wa Marekani kusafiri hadi mjini Islamabad na kuwaacha waondoke bila makubaliano yoyote.” Alisema Merz.

    “Taifa nzima linadhalilishwa na uongozi wa Iran haswa na viongozi wa jeshi la mapinduzi. Natumai hili litaisha hivi karibuni.”

    Iran waliwasilisha hapo jana pendekezo la kusitisha vita, iliyojumuisha kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz na kufanya mazungumzo pembeni hapo baadaye kuhusu silaha za nyuklia, makombora na kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.

    Pia unaweza kusoma:

  7. IS yadai kutekeleza mashambulizi yaliyosababisha vifo vya watu 29 Nigeria

    .

    Watu wenye silaha wamewauwa takriban watu 29 katika shambulizi dhidi ya kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa jimbo la Adamawa nchini Nigeria, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Kundi la Islamic State (IS) limedai kuhusika na shambulizi hilo, bila kubainisha nia yake.

    Mamlaka na wakaazi wa eneo hilo wanasema wanamgambo hao walivamia uwanja wa mpira ambapo watu walikuwa wamekusanyika na kufyatua risasi kiholela, kabla ya kuchoma nyumba, maeneo ya ibada na pikipiki.

    Gavana wa jimbo hilo Ahmadu Umaru Fintiri aliweka picha zake mitandaoni akiwasili katika eneo la tukio, huku akielezea shambulio hilo kama "udhalilishaji mkubwa".

    Akikagua uharibifu katika eneo hilo, msemaji wa gavana aliandika kwenye Facebook kwamba "wakaazi bado wana hofu".

    Familia nyingi "zimetoroka kwa kuhofia mashambulizi zaidi", msemaji huyo aliongeza.

    Mashambulizi yanayohusishwa na wapiganaji wa kundi la Islamic State yameripotiwa kaskazini-mashariki mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Hormuz ni silaha ya nyuklia ya kiuchumi ya Iran - Rubio

    Rubio

    Chanzo cha picha, AFP via Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio ametaja hatua ya kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kuwa "sawa na silaha ya nyuklia ya kiuchumi" na kusema kuwa Iran inajaribu kuitumia dhidi ya dunia.

    Katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox News nchini Marekani, Marco Rubio alisema kuwa "Iran inajigamba kwamba inaweza kushikilia mateka asilimia 20 hadi 25 ya nishati duniani." Aliongeza kusema Iran ikiruhusiwa kumiliki silaha za nyuklia, "itashikilia mateka eneo lote la Mashariki ya Kati."

    Marco Rubio alisema anatumai kuwa baada ya mzozo huu, dunia nzima itakuwa imetambua tishio linaloletwa na Iran.

    Kulingana naye, kile ambacho Iran inataka kufanyia ulimwengu kupitia silaha za nyuklia, kwa sasa inafanya kupitia mafuta.

    Rubio aidha amesema kuwa, wahusika wote katika serikali ya Iran ni watu wenye misimamo mikali, lakini wapo baadhi yao wanaoamini kuwa ni lazima waendeshe nchi na uchumi.

    Waziri huyo pia amesisitiza kuwa, Marekani haitaki kuwadhuru wananchi wa Iran.

    Akizungumzia maandamano dhidi ya serikali ya Iran mapema mwaka huu na ukandamizaji wa serikali dhidi ya waandamanaji alisema: "Tulitaka watu wa Iran wasikilizwe badala ya kuwaua watu 30,000 hadi 40,000 mitaani."

    Soma zaidi:

  9. 'Huu ni uharamia katika maji ya kimataifa'- Iran yalalamikia Marekani kukamata meli yake nyingine

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Iran imelaani vikali hatua ya Marekai kukamata meli yake nyingine iliyokuwa imebeba mafuta ghafi katika Bahari ya Hindi.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baghaei aliitaja kitendo cha Marekani kuwa ni "uharamia".

    Baghaei aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Hatua hii kwa kweli ni uhalalishaji wa wazi uharamia na ujambazi wa kutumia silaha baharini.”

    Msemaji huyo wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran aliendelea kusema: "Marekani lazima iwajibike kikamilifu kwa mwenendo wake unaokiuka sheria; hatua ambayo inakiuka misingi ya sheria za kimataifa na biashara huria ya kimataifa na kutishia kanuni za kimsingi za usalama wa baharini."

    Aliandika chapisho hilo kujibu barua ya Wakili wa Wilaya ya Columbia, Jeanine Ferris Piro, akitangaza kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa meli ya mafuta kwa ombi la ofisi yake katika mahakama ya shirikisho, akiandika: "Usiku mmoja, kwa mujibu wa hati iliyotolewa na ofisi yangu na iliyotiwa saini na hakimu wa shirikisho, wanajeshi wa Marekani vimekamata meli ya Iran MT Majestic (zamani MT Phoenix) katika bahari ya Hindi ikiwa na takribani mapipa milioni 1.9 ya mafuta ya Iran.

    Maelezi zaidi:

  10. Afisa wa Marekani: Trump hajaridhika na pendekezo la Iran

    Donald Trump

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Donald Trump

    Afisa mmoja wa Marekani alisema siku ya Jumatatu kuwa Rais Donald Trump hakuridhishwa na pendekezo la Iran la kumaliza vita kwa sababu halikuzungumzia mpango wa nyuklia wa Iran.

    Shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa huyo wa Marekani akisema, akimzungumzia Trump: "Hapendi pendekezo hili."

    Mapema Jumatatu, Trump alijadili pendekezo hilo na washauri wake wakuu wa usalama wa kitaifa.

    Mzozo wa Marekani na Iran umesalia palepale huku usambazaji wa nishati kutoka eneo hilo ukipungua.

    Vyanzo vya habari vya Iran vilisema mapema Jumatatu kwamba pendekezo hilo litaahirisha majadiliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran hadi vita vitakapoisha na mizozo inayohusiana na urambazaji kutoka Ghuba kutatuliwa.

    Tangu mwanzoni Washington imesisitiza kuwa masuala ya nyuklia lazima yashughulikiwe.

    Vyanzo vya habari kutoka Pakistan, vikifanya kazi kama mpatanishi, viliripoti kuwa juhudi za kukomesha uhasama kati ya Marekani na Iran hazijakoma.

    Hata hivyo, matumaini ya kufufua mazungumzo ua amani yamefifia tangu Trump atangaze wikendi iliyopita kwamba anaahirisha ziara ya mjumbe wake maalum Steve Wittkopf na mkwe wake Jared Kushner mjini Islamabad, mji mkuu wa Pakistan.

    Pia unaweza kusoma:

  11. Idadi ya watu walionyongwa Korea Kaskazini iliongezeka sana wakati wa janga - ripoti

    Korea Kaskazini iliwanyonga jumla ya watu 358 waliohukumiwa kifo kati ya 2011 na 2024, kulingana na ripoti ya shirika lisilo la kiserikali.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Korea Kaskazini iliwanyonga jumla ya watu 358 waliohukumiwa kifo kati ya 2011 na 2024, kulingana na ripoti ya shirika lisilo la kiserikali.

    Utekelezaji wa hukumu ya kifo uliongezeka sana nchini Korea Kaskazini wakati wa janga la Covid-19, kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Seoul.

    Kuanzia Januari 2020 hadi mwishoni mwa 2024, takribani watu 153 walinyongwa au kuhukumiwa kifo - ongezeko kubwa kutoka kwa watu 44 katika miaka mitano kabla ya janga hilo, kulingana na ripoti ya Transitional Justice Working Group (TJWG).

    Baadhi ya makosa yalihusiana na dini, ushirikina na maudhui ya kitamaduni ya kigeni - ikiwa ni pamoja na utumiaji wa tamthilia za K na K-pop.

    Idadi ya mauaji ilipungua kati ya 2015 na 2019 kufuatia shinikizo la kimataifa kufuatia uchunguzi wa kihistoria wa Umoja wa Mataifa.

    Lakini mauaji yaliongezeka mnamo 2020, baada ya Pyongyang kufunga mipaka yake, ilisema TJWG.

    Shirika hilo lisilo la kiserikali liligundua kuwa mauaji nchini Korea Kaskazini yalifikia kilele mwanzoni mwa miaka ya utawala wa Kim, huku zaidi ya watu 80 wakinyongwa mwaka 2013.

    Idadi hiyo inaonekana kupungua kufuatia uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ambao uligundua kuwa Pyongyang ilikuwa ikitekeleza ukiukaji wa haki za binadamu kimfumo.

    Maelezo zaidi:

  12. Meli ya kifahari ya Urusi yapitia Hormuz licha ya Mlango huo wa Bahari kufungwa

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Meli kubwa inayohusishwa na mmoja wa washirika wakuu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin imepitia Mlango-Bahari wa Hormuz, licha ya njia hiyo muhimu ya baharini kufungwa.

    Meli ya kifahari ya Nord, yenye urefu wa mita 142, inayohusishwa na bilionea wa Urusi Alexey Mordashov, ilisafiri kutoka Dubai hadi Muscat, Oman mwishoni mwa juma, mojawapo ya meli kadhaa za kibinafsi zilizovuka bahari hiyo katika miezi ya hivi karibuni.

    Iran imeshirikiana na Urusi katika mazungumzo ya ngazi ya juu wiki hii huku mzozo kati yake na Marekani kuhusu kufunguliwa tena kwa mlango huo wa bahari ukiendelea.

    Takriban moja ya tano ya usambazaji wa mafuta ghafi na gesi asilia (LNG) husafirishwa kupitia njia ya majini.

    Mordashov, ambaye ana uhusiano wa karibu na Putin, hajaorodheshwa kama mmiliki rasmi wa meli hiyo ya kifahari. Lakini, rekodi za Nord zinaonyesha kuwa ilisajiliwa kwa kampuni inayomilikiwa na mkewe mnamo 2022.

    Nord, anayekadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 500, aliondoka Dubai Ijumaa usiku na kufika Al Mouj, marina katika mji mkuu wa Oman, Jumapili asubuhi, kulingana na data za jukwaa la Marine Traffic.

    Usafiri wa baharini kupitia mkondo wa Ghuba kwa sasa iko katika sehemu ndogo ukilinganisha na viwango vya kabla ya vita.

    Mzozo huo umechangia kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta duniani, huku kiwango cha kimataifa cha mafuta ghafi ya Brent kikipanda hadi dola 109 za Kimarekani kwa pipa siku ya Jumatatu.

    Iran imeendelea kudhibiti usafiri wa meli kupitia njia hiyo muhimu ya majini baada ya Rais Donald Trump kutangaza kuwa vikosi vya Marekani vitaweka kizuizi cha kijeshi dhidi ya bandari za Iran.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Mshukiwa wa shambulio la Washington ashtakiwa kwa jaribio la mauaji dhidi ya Trump

    .

    Chanzo cha picha, @REALDONALD TRUMP / TRUTHSOCIAL

    Mtu mmoja mkaazi wa Californiameshtakiwa kwa jaribio la kumuua Rais wa Marekani Donald Trump katika tukio ambalo limeibua maswali kuhusu usalama katika Ikulu ya White House.

    Cole Tomas Allen, 31, pia alishitakiwa kwa makosa mawili ya kupatikana na silaha alipofikishwa mbele ya mahakama mjini Washington DC siku ya Jumatatu.

    Alikuwa amebeba bunduki ya otomatiki, bunduki ya kusukuma maji na visu vitatu alipokuwa akipita eneo la ukaguzi wa usalama kwenye wakati wa dhifa ya Waandishi wa Habari cha White House siku ya Jumamosi, waendesha mashtaka wanasema.

    Afisa wa maalum wa ulinzi alijeruhiwa wakati wa shambulio hilo. Mshitakiwa anakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani akipatikana na hatia.

    Akiwa amevalia ovaroli ya bluu yeenye alama ya jina, mshukiwa alionekana mtulivu katika mahakama ya Jumatatu katika mji mkuu wa taifa hilo. Alizungumza kwa upole huku akijibu karibu kila swali kutoka kwa hakimu kwa kutumia maneno "ndio, kwa heshima yako" au "hapana, kwa heshima yako".

    Aliifahamisha mahakama umri wake na kuongeza kuwa alikuwa na shahada ya uzamili.

    Wachunguzi wanasema mwanamume huyo wa California mwenye umri wa miaka 31 alitaka kuwaua maafisa wengi iwezekanavyo wa ngazi ya juu.

    Wakati wa tukio la Jumamosi usiku, Trump, Makamu wa Rais JD Vance, wajumbe wa baraza la mawaziri na maafisa wengine wa Ikulu ya White House waliondolewa kwenye ukumbi wa hoteli ya Washington Hilton baada ya milio ya risasi kusikika.

    Soma zaidi:

  14. Karibukwa matangazo ya moja kwa moja.