Moja kwa moja, Shambulio baya dhidi ya harusi Iran huenda lilisababishwa na kombora la Marekani - Reuters

Shirika la habari la Reuters liliripoti katika taarifa ya kipekee kwamba, kulingana na uchambuzi wa wataalamu wa silaha waliochunguza picha na video zilizothibitishwa na shirika hilo, mlipuko huo ulisababishwa na kombora la Marekani

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Umoja wa Mataifa wasema wapiganaji wa kigeni wanachochea vita nchini Sudan

    Umoja wa Mataifa wasema wapiganaji wa kigeni wanachochea vita nchini Sudan

    Chanzo cha picha, Reuters

    Umoja wa Mataifa unasema wapiganaji wa kigeni, silaha na teknolojia ya kijeshi kutoka nje zinaendelea kuchochea vita nchini Sudan, huku nchi kama Somalia zikitajwa katika mtandao unaodaiwa kusaidia pande zinazopigana.

    Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaochunguza ukweli kuhusu mzozo huo umesema msaada huo umeongeza uwezo wa jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kufanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo ya raia yaliyo mbali na uwanja wa vita.

    Vita vilianza Aprili 2023 kutokana na mzozo wa kugombea madaraka kati ya jeshi na RSF, na hadi sasa vimewalazimisha zaidi ya watu milioni 14 kuyahama makazi yao.

    Ripoti hiyo imesema zaidi ya watu 1,000 waliuawa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika miezi mitano ya kwanza ya 2026, huku pande zote mbili zikishutumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu.

    Umoja wa Mataifa unasema baadhi ya vitendo hivyo vinaweza kufikia kiwango cha uhalifu wa kivita.

    Wachunguzi pia wanaamini kuwa mtandao unaohusisha watu na taasisi katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Chad, Libya na Somalia umeipa RSF silaha, vifaa, msaada wa vifaa na usafirishaji, mafunzo pamoja na wapiganaji wa kigeni.

    Umoja wa Mataifa pia unasema hadi wakandarasi 2,000 kutoka Colombia walisaidia kuendesha na kutunza mifumo ya ndege zisizo na rubani na silaha nyingine za kisasa zinazotumiwa na RSF.

    Baadhi yao walikuwepo wakati wa operesheni karibu na Al-Fashir, Darfur, mji ambao RSF iliuteka Oktoba 2025.

    Umoja wa Mataifa umesema mauaji yaliyofanyika huko yalikuwa na viashiria vya mauaji ya kimbari.

    UAE imekanusha mara kwa mara kutoa msaada wa kijeshi kwa RSF, huku Colombia ikisema inapinga shughuli za mamluki na imechukua hatua kukabiliana na ushiriki wa raia wake katika migogoro ya nje.

    Somalia imesema inachukulia kwa uzito tuhuma hizo, na kwamba haitaruhusu ardhi, anga au bandari zake kutumiwa kwa madhumuni ya kijeshi na pande zinazohusika katika vita vya Sudan.

    Hata hivyo, serikali hiyo imekiri kuwepo kwa mapengo katika ushirikishwaji wa taarifa kati ya serikali ya shirikisho na tawala za kikanda.

    Chad, kupitia balozi wake mjini Geneva, imekanusha tuhuma hizo na kusisitiza kuwa haina upande wowote katika mzozo huo.

    Katika kile kinachoelezwa kama vita vya ndege zisizo na rubani, Umoja wa Mataifa unasema silaha hizo zilizoingizwa kutoka nje zimeongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa jeshi la Sudan na RSF kufanya mashambulizi ya masafa marefu.

    Unaweza kusoma;

  2. Waziri wa Fedha wa Marekani: Umoja wa Ulaya umejiunga na operesheni ya kuitenga Iran kiuchumi

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Besant, akirejelea taarifa ya mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa kundi la G20, alitangaza kuwa "Umoja wa Ulaya umejiunga rasmi na 'operesheni ya kuitenga Iran kiuchumi'" na kwamba Marekani "inathamini msimamo wao thabiti na wa mapema."

    Bw. Besant aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Marekani inasimama kidete pamoja na washirika wetu kuhakikisha kuwa utawala wa uhalifu wa Iran hauwezi kutumia mfumo wa kifedha wa kimataifa kufadhili malengo yake ya nyuklia, programu za silaha, na makundi ya kigaidi yanayofanya kazi kwa niaba yake."

    Waziri wa Fedha wa Marekani amesisitiza kuwa "dunia inatoa ujumbe wa wazi kwa utawala wa Iran: 'Hatutaacha hadi njia ya mwisho ya uhai wa kifedha itakapokatwa.'"

    Siku mbili zilizopita, Tume ya Ulaya ilitoa taarifa pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa fedha na magavana wa benki kuu wa G20 huko Asheville, ikiunga mkono vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran.

  3. Figo ya nguruwe iliyopandikizwa kwa binadamu yafanya kazi kwa siku 271

    .

    Chanzo cha picha, Kate Flock/Massachusetts General Hospital

    Figo iliyopandikizwa kutoka kwa nguruwe imefanya kazi mwilini mwa mgonjwa kwa siku 271 – muda mrefu zaidi kuwahi kurekodiwa, kulingana na madaktari nchini Marekani.

    Tim Andrews amesema upandikizaji huo ulimpa "matumaini" na kumwepusha na miezi kadhaa ya kulazimika kwenda hospitalini ili damu yake isafishwe kwa mashine.

    Timu ya wataalamu katika hospitali ya Mass General Brigham inasema kazi yao inaonyesha kuwa viungo vya nguruwe vinaweza kutumika kama "daraja" la muda hadi pale kiungo cha binadamu kitakapopatikana kwa ajili ya upandikizaji.

    Hata hivyo, kiungo hicho cha nguruwe hatimaye kilishindwa kufanya kazi na kikaondolewa, hivyo Andrews alihitaji kufanyiwa dayalisisi kwa muda mfupi kabla ya kupatikana kwa mtoaji.

    Madaktari na wanasayansi wanachunguza uwezekano wa kupandikiza viungo kutoka kwa viumbe wa spishi nyingine – kutokana na uhaba wa viungo kwa ajili ya upandikizaji.

    Nchini Marekani, takriban watu 100,000 wanasubiri figo, huku upandikizaji wa figo 25,000 pekee ukifanyika kila mwaka.

    Nchini Uingereza, zaidi ya watu 7,000 wako kwenye orodha ya wanaosubiri kupandikizwa figo.

    Andrews aliambiwa kuwa inaweza kuchukua miaka saba kufikia orodha hiyo, ilhali kwa wastani watu huishi miaka mitano tu wakiwa wanategemea matibabu ya dayalisisi.

  4. DR Congo yaahhidi kuhamisha ubalozi wake wa Israel mjini Jerusalem

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza siku ya Alhamisi kuwa itahamishia ubalozi wake nchini Israel hadi Jerusalem, ikijiunga na kundi dogo la nchi, ikiwemo Marekani, katika kuchukua hatua hiyo yenye uzito wa kidiplomasia ya kuunga mkono mamlaka ya Israel juu ya mji huo mtakatifu wenye utata.

    Kufuatia ziara ya Rais Felix-Antoine Tshisekedi, nchi hizo mbili zilisema katika taarifa kuwa zitachukua hatua za "kuhamisha ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem", bila kutaja muda maalum wa kufanyika kwa hatua hiyo.

    Taarifa hiyo ilieleza kuwa, katika mkutano wao, Tshisekedi na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walizungumzia "nia yao ya pamoja ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia".

    Soma pia:

  5. Netanyahu atishia kuipindua serikali ya Iran

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Netanyahu

    Waziri Mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amesema siku ya Alhamisi kuwa kuuangusha utawala wa Jamhuri ya Kiislamu ni jambo "linalowezekana kufikiwa," akisisitiza kuwa utawala huo ni dhaifu kuliko wakati wowote ule na unapambana ili kusalia madarakani.

    Katika hafla iliyohusisha viongozi wa kijeshi, aliongeza kuwa anaamini inawezekana "kuondoa" kabisa tishio la Iran, akilitaja hilo kuwa ndilo jukumu kuu linaloikabili Israel bado.

    Netanyahu amesema kuwa hatua ya Iran kutolenga Israel katika mzunguko wa hivi karibuni wa mashambulizi haikuwa bahati mbaya, akiongeza kuwa Tehran inafahamu vyema nguvu, silaha, na azimio la Israel.

    Netanyahu anajiandaa kushiriki katika uchaguzi wa bunge wenye ushindani mkali mwishoni mwa mwezi wa Oktoba.

    Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yisrael Katz, alisema nchi yake iko tayari kujibu "kwa nguvu kubwa" iwapo Iran itashambulia wakati wa sikukuu za Kiyahudi, zinazoanza katikati ya mwezi wa Septemba, akibainisha kuwa Iran ililenga maeneo mbalimbali katika eneo hilo, isipokuwa Israel, wakati wa mzozo huo wa hivi karibuni.

    Soma pia:

  6. Mamlaka na wakaazi wapambana kuzima moto Mlima Kilimanjaro

    .

    Chanzo cha picha, Jackson Mauki

    Mamlaka na wakazi wa kaskazini mwa Tanzania wanapambana kuzima moto unaowaka kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro, ambao ni mlima mrefu zaidi barani Afrika.

    Moto huo unateketeza eneo lililoko katika mwinuko wa takriban mita elfu tatu na mia nne juu ya usawa wa bahari.

    Afisa wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania ameiambia BBC kwamba bado haijafahamika kilichosababisha moto huo kuwaka.

    Mlima Kilimanjaro, ambao ni muhimu kwa bioanuwai na utalii, umekumbwa na visa vingine vikubwa vya moto wa nyika viliyosababisha uharibifu katika miaka ya hivi karibuni.

    Mwaka 2023, moto uliodumu kwa takriban wiki moja uliharibu eneo la kilomita 17 za mraba, sawa na takriban asilimia moja ya eneo la hifadhi ya mlima huo.

  7. Korea Kusini inajitayarisha kutuma askari kwenye Mlango Bahari wa Hormuz

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Korea Kusini

    Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti kwamba serikali ya nchi hiyo inajiandaa kupeleka vifaa na vikosi vya kijeshi ili kuunga mkono kile kinachoitwa "uhuru wa urambazaji katika Mlango-Bahari wa Hormuz" na inapanga kuanza misheni hii kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Reuters iliandika Alhamisi (Septemba 3) kwamba ripoti katika vyombo vya habari vya Korea Kusini, zikinukuu vyanzo vya serikali na kijeshi, zilisema Seoul inachukua hatua muhimu za kisheria ili kupata idhini ya bunge kwa ajili ya kupelekwa huko.

    Kulingana na ripoti hizi, baada ya kukagua mpango huo katika Baraza la Mawaziri, serikali inapanga kuwasilisha ombi rasmi la idhini ya bunge mwezi huu.

    Uwezekano wa kupelekwa kwa vikosi vya Korea Kusini unakuja huku mvutano wa usalama katika Mlango-Bahari wa Hormuz na mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara yakiongezeka katika wiki za hivi karibuni, na nchi kadhaa zinachunguza njia za kushiriki katika kulinda usalama wa meli katika njia hii ya kimkakati ya maji.

    Maafisa wa serikali ya Korea Kusini bado hawajajibu rasmi ripoti hizi.

  8. Shambulio baya dhidi ya sherehe ya harusi nchini Iran huenda lilisababishwa na kombora la Marekani - Reuters

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Shirika la habari la Reuters liliripoti katika taarifa ya kipekee kwamba, kulingana na uchambuzi wa wataalamu wa silaha waliochunguza picha na video zilizothibitishwa na shirika hilo, mlipuko uliolenga sherehe ya harusi katika mji wa Kohstak kusini mwa Iran siku ya Jumanne, ambao uliua watu watano na kujeruhi angalau 68, una uwezekano mkubwa wa kusababishwa na shambulio la moja kwa moja la silaha ya Marekani, badala ya athari isiyo ya moja kwa moja au kuruka kwa silaha hiyo baada ya kugonga lengo jingine.

    Katika ripoti hiyo iliyochapishwa Alhamisi, Septemba 3, Reuters iliandika: "Reuters iliwasilisha picha na video za shambulio hilo kwa wataalamu wanne wa silaha.

    Wataalamu hao walisema kuwa namna uharibifu ulivyotokea inaashiria shambulio la moja kwa moja la silaha moja, na si mlipuko uliosababishwa na silaha hiyo kuruka kwingine baada ya kugonga lengo jingine."

    Watatu kati ya wataalamu hao pia waliambia Reuters kwamba "ushahidi uliopo unaonyesha kuwa silaha hizo zina uwezekano mkubwa wa kuwa zimetengenezwa Marekani, na si kombora la ulinzi wa anga la Iran lililopotea njia."

    Gareth Collet, brigedia jenerali mstaafu wa Jeshi la Uingereza na mtaalamu wa kutegua mabomu mwenye shahada ya uzamivu katika uhandisi wa vilipuzi, aliambia Reuters kuwa inawezekana silaha hizo zilikosa tu lengo lake lililokusudiwa.

    Reuters inasema afisa wa Marekani, aliyeomba kutotajwa jina, alithibitisha kuwa Marekani ilifanya shambulio la anga katika eneo la Kohstak usiku wa Jumanne, kwa lengo la kuharibu vifaa vya kijeshi vya IRGC.

    Zaida Soma Hapa:

  9. Natumai hujambo na karibu katika habari zetu za moja kwa moja