Lebanon yaitikia kujumuishwa katika makubaliano ya Marekani na Iran
Viongozi wa kisiasa nchini Lebanon wameitikia mpango ulioidhinishwa na Pakistan kati ya Marekani na Iran - ambao, Islamabad inasema, utasitisha "operesheni za kijeshi katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon".
Rais wa Lebanon Joseph Aoun anasema raia wake "wanatarajia maelewano haya kuonyeshwa kwa vitendo ambavvo zitamaliza kabisa mzunguko wa vurugu".
Amezishukuru nchi hizi "mbili" kwa kuchangia kuanzisha mkataba huo, na anasema anatumai kuwa hatua hiyo "itaashiria mwanzo wa mpango ambao utadumisha utulivu wa kikanda".
Spika wa bunge la Lebanon Nabih Berri - kiongozi wa vuguvugu la Amal na mtu anayefungamana na Hezbollah - pia amepongeza mpango huo.
Anaishukuru Iran na Marekani kwa kujumuisha kifungu cha "maalum" - kwa Israel kukomesha mashambulizi yake dhidi ya Lebanon - kama sehemu ya makubaliano.