Viongozi wa Marekani na Iran wamesaini makubaliano ya awali
ya amani yanayolenga kukomesha vita hivyo, na kuanza kutekelezwa mara moja.
Mkataba huo unajumuisha kufungua tena Mlango-Bahari wa
Hormuz, mpango wa dola bilioni 300 (£224bn) kwa ajili ya "ujenzi
mpya" wa Iran, na Marekani kukomesha "aina zote za vikwazo"
dhidi ya Iran.
Lakini suala la mpango wa nyuklia wa Iran, sababu kuu
iliyotajwa na Marekani kwa mzozo huo, bado halijajadiliwa kwa muda wa siku 60 za
kusitisha mapigano ulioongezwa.
Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisaini makubaliano hayo nchini Ufaransa wakati wa mkutano wa kilele wa G7, alitetea pendekezo hilo, akisema litaepusha "janga la kiuchumi". Hata hivyo, alionya kwamba Marekani "itaishambulia" Iran ikiwa hakuna makubaliano ya mwisho yatakayofikiwa.
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian pia alisaini hati hiyo Jumatano, Tehran ilithibitisha.
Spika wa bunge la Iran na mjumbe mkuu wa mazungumzo Mohammad Bagher Ghalibaf aliviambia vyombo vya habari vya serikali kwamba imani yake kwa Marekani bado ipo, na Iran "iko katika hali ya tahadhari".
"Ikiwa adui haelewi lugha ya mantiki, tutaingia tena na lugha ya nguvu," aliambia chombo cha habaro cha serikali cha Fars.
Marekani na Israel zilianzisha vita dhidi ya Iran mnamo tarehe 28 Februari, na kumuua Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei na maafisa wakuu wa kijeshi siku ya kwanza.
Trump aliwaambia waandishi wa habari nchini Ufaransa katika eneo la mapumziko la Evian-les-Bains kando ya ziwa, ambapo mkutano wa kilele wa G7 uliandaliwa, kwamba mpango huo utaepusha " dhiki kwa dunia nzima".
"Sikutaka kuona janga la kiuchumi," Trump aliwaambia waandishi wa habari. "Kama ungeendelea hivi, hilo lingetokea."