Jeshi la Marekani lamuua kiongozi wa genge la Tren de Aragua nchini Venezuela

Chanzo cha picha, Truth Social
Niño Guerrero, ambaye jina lake kamili ni Héctor Rusthenford Guerrero Flores, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa Tren de Aragua. Genge hilo ni moja ya makundi hatari Marekani Kusini na imekuwa ikilengwa na utawala wa Trump.
Rais Trump amelituhumu genge hilo kwa kushiriki katika “vita visivyo vya kawaida” dhidi ya Marekani na kulitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Rais Trump alichapisha picha za video za shambulio hilo la angani, zikionyesha jengo la kijani na kibanda kilichokuwa karibu kikilipuliwa.
Trump aliongezea kuwa operesheni hiyo ya kijeshi ilifanikishwa na “marafiki wetu nchini Venezuela, ambao tunafanya kazi nao vizuri sana”.
Mamlaka za Venezuela zimethibitisha kushiriki kwao katika kile walichokiita “operesheni ya pamoja”.
Mwezi Januari, vikosi vya Marekani vilimkamata Rais wa wakati huo wa Venezuela Nicolás Maduro na kumfungulia mashtaka mjini New York, hati ya mashtaka ikimtaja Guerrero Flores kama mshirika wake katika kutekeleza uhalifu.
Pia unaweza kusoma:





