Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mohamed bin Salmán: Kwa namna gani Mwanamfalme huyu mwenye umri wa miaka 34 amekuwa na nguvu Mashariki ya kati?
Septemba 2013, nikiwa njiani kwenda kwenye hadhira ya mrithi wa kiti cha ufalme, Saudi Arabia, Salman bin Abdulaziz, sikuacha kufikiria kuhusu ziara yangu ya awali nchini humu.
Ilikuwa mwaka 2004, wakati Salman bin Abdulaziz alikuwa gavana wa jiji la Riyadh, kamanda wa jeshi ambaye aliishambulia timu ya BBC, ambayo nilikuwa sehemu ya timu hiyo. Katika mashambulizi hayo, niliumia vibaya huku mpiga picha Simon Cumbers akifariki kwa majeraha ya risasi.
Waliniambia kwamba mwanamfalme alikuja kuniona Hospitali, lakini sikuwa nakumbukumbu, lakini simkumbuki kwa sababu nilikuwa nimepoteza fahamu
Kwa sasa, Salman bin Abdulaziz ni mfalme. Mfalme mwenye afya dhaifu. Hata mwaka 2013 unaweza kusema hivyo kwa sababu alikuwa hata kutembea shida na alikuwa anazungumza kwa shida.
Nilipokuwa nakaribia, walipokuwepo watu, niligundua kuna mtu nyuma yangu, aliyekuwa akichukua mawili matatu na kuandika kwenye kitabu chake.
Nilidhani ni kiongozi wa wafanyakazi au alikuwa msaidizi wa aliyekuwa mwanamfalme wa wakati huo. Shughuli zilipoisha nilimfuata na kumuuliza yeye ni nani.
"Mimi ni mwanamfalme Mohamed bin Salman. Ni mwanasheria. Ulizungumza na baba yangu, "alijibu.
Kijana huyo, aliyekuwa na miaka kama 28, angekuja kuwa mtu mwenye nguvu duniani, na mtu mwenye utata zaidi kutokea uarabuni.
Kesi ya Khashoggi
Oktoba 2, 2018, baada ya kuingia ubalozi mdogo wa Saudi Arabian huko Istanbul, mwandishi wa habari - na mtu aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa Bin Salman - Jamal Khashoggi aliuawa na kundi la majasusi wa Saudi kutoka Riyadh. Walimuua, wakamkatakata na kuutupa mwili wake.
Maelfu ya watu waliuawa katika vita iliyoisumbua na kuiharibu sana Yemen, wengi waliuawa kutokana na mashambulizi yaliyotekelezwa na vikundi vyenye uhusiano na Saudia.
Mamia ya watu ambao walikuwa wakosoaji wakubwa wa Bin Salman aliyejulikana kwa kifupi kama MBS waliotezwa wakiwa gerezani.
Lakini kifo cha kinyama cha Khashoggi kimeifanya duniani nzima kumgeuka mwanamfalme huyo.
Serikali ya Saudi Arabia imekana mwanamfalme wake kuhusika na mauaji hayo. Lakini nchi za magharibi zinaamini kwamba MBS anajua nini kilichokuwa kinaendelea kuhusu kuawa kwa mwandishi huyo.
Ripoti zingine zinasema Shirika la ujasusi la Marekani (CIA) linaamini MBS aliagiza kuuawa kwa mwanahabari huyo.
Mwanamfalme huyo alikiri kwamba atabeba 'jukumu la kilichotokea', lakini hilo halimaanishi kwamba anakubali kuwa na hatia ya kilichotokea. Yeye na serikali wamekuwa wakipinga wakati wote kuhusu kuhusika kwao kwa kifo hicho. Usiri mkubwa wa lililotokea analo mshauri wa zamani na mtu wa karibu wa MBS: Saud al Qahtani, aliyekuwa rubani wa ndege.
Alistaafu kazi hiyo, muda mfupi baada ya kuuawa kwa Khashoggi , na alikuwa mtu wa karibu wa mwanamfalme katika mahakama ya kifalme. Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi, A l Qahtani ndiye alikuwa mratibu mkubwa wa kufuatilia watu ndani na nje ya nchi hiyo, akitumia program maalumu ya kompyuta. Wengi waliofuatiliwa ni wale waliokuwa wakosoaji wakubwa wa MBS au serikali kupitia mitandao ya kijamii.
Kufikia 2017, wakosoaji wengi kupitia mitandao ya kijamii, wapigania demokrasia na wanaharakati wa haki za binadamu walitupwa jela, Khashoggi alijua kwamba maisha yake yako hatarini. Baada ya MBS kukimbilia Marekani Juni 2017, Khashoggi aliyekuwa na miaka 59 wakati huo wa kifo chake, alianza kuandika Makala za kuukosoa mwenendo wa serikali ya MBS kupitia Washington Post .
Umaarufu wake kama mwandishi nguli Mashariki ya kati ukazidi kupaa, na hapo hofu ikaongezeka kuhusu usalama wake. Kifo chake kwenye ubalozi mdogo wa Uturuki, ikawa kashfa kubwa ya kimataifa, licha ya serikali ya Saudi kukana kuhusika.
Marekani ikawawekea vikwazo watu 17 waliodaiwa kuhusika na mauaji hayo, na aliyekuwa katika orodha ya juu ni Saud al Qahtani. Hata hivyo mpaka sasa, hakuna ushahidi thabiti unaomuhusisha moja kwa moja MBS na kifo cha mwandishi huyo.
Serikali ya Saudi ikawapeleka watu 11 waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwandishi huyo, ingawa kuna giza kuhusu adhabu zao, wengi wanaamini wamepelekwa kwa ajili ya kumlinda MBS na serikali kwa ujumla.
Tangu MBS arithi kiti na kwa kusaidiwa na mfalme, kumekuwa na jaribio la kusaidia kuficha tukio hilo kwa ajili ya kulinda hadhi ya nchi yake, wakati huo huo amekuwa mtu asiyetakwa maoni tofauti yanayotofautiana na mtazamo wake.
Wanamtandao, wanaharakati, wakosoaji na wanasiasa kutoka vyama vya siasa, wengi wameishia jela chini ya sheria ambazo haziruhusu majadiliano ama kusikilizwa kwa upande wa pili.
Hata ripoti za shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch lilibainisha kuhusu 'kuongezeka kwa vitendo vya 'ukamataji wa watu kiholela' wakiwemo wanaharakati mwaka 2018.
Inawezekana hilo, lakini anachokitaka MBS ni mabadiliko kutokea kwenye himaya ya mfalme na sio kwa watu wengine ama njia zilizozoeleka.
Loujain al Hathloul, mwanamke aliyesheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa ya miaka 30, jela, kisa ni kutetea haki za wanawake kuruhusiwa kuendesha magari.
Septemba 2018, waendesha mashitaka wa Saudia walitangaza kwamba kwa mtu yeyote atakayetuma ama kuchapicha kwa maudhui yanayokiuka maadili kwa tafsiri za Mamlaka, basi atafungwa jela miaka mitano na faini ya dola $ 650,000.
MBS alikubali jambo hilo na katika mahojiano akakiri ,watu wengi wamefungwa akisema, unapofanya mabadiliko kadhaa, mambo kama hayo hutokea.
Lakini kwa namna ganio, mtu asiyekuwa anajulikana miaka sita iliyopita, leo akawa mtu mwenye nguvu zaidi Mashariki ya kati?
"Mtoto wa taifa"
Akizaliwa Agosti 31, 1985, Mohamed bin Salman amekua katika maisha mazuri kama ilivyo kwa wanawafalme wengine karibu 5,000 nchini humo.
Akiwa mmoja wa watoto 13 wa mfalme , utoto wake aliutumia kwenye kasri la kifalme lililokuwa analindwa wakati wote. Alikuwa na wahudumu mbalimbali, wapishi, na madereva wakimsaidia wakati wote.
Akasoma sheria katika chuo kikuu cha King Saud na wengi wanamuona kama 'mtoto wa taifa'.
Ni kawaida kwa nchi kama Saudi Arabia, kumkuta mwanaume akiwa na wake wanne, lakini MBS, ana mke mmoja, na amekuwa hapendi maisha yake binafsi kufuatiliwa.
Amewezaje kuwa mwanamfalme mwenye nguvu kutoka kuwa mwanasheria wa kawaida?
Jibu ni rahisi tu ni mjumuiko wa nguvu za kisiasa, kubebwa na nguvu ya wazazi wake, hasa mfalme, na tabia yake binafsi iliyojengwa katika sifa za kutawala.
Baada ya kuwa sehemu ya serikali kwa miaka kadhaa, akipewa nafasi muhimu na baba yake, mwaka 2015 umaarufu wa MBS ulianza kushika kasi
Kifo cha mfalme Abdullah, mwezi Januari mwaka huo, ilimaanisha kwamba, ufalme unaenda kwa baba yake, Salman bin Abdulaziz, aliyeupokea akiwa mtu mzima wa miaka 80.
Hapo akateuliwa kuwa waziri wa ulinzi na kiongozi wa mawaziri katika mahakama ya kifalme. Kuanzia wakati huu alikuwa anaweza kusema na kuamua chochote. Mambo yalianza kubadilika na nguvu zake ziliongezeka.
Kwa mfano mwaka 2015 alianzisha mpango wa kupambana na kila kitu kusini mwa nchi hiyo. Wakati huo huo Yemen palikuwa na kundi la waasi la Haouthi lililoshika hatamu na kudhibiti eneo la magharibi mwa nchi hiyo, katika mji wa Sana'a.
Bila kuwashirikia viongozi wenzake, wala kutoa taarifa alianzisha vita dhidi ya kundi hilo la Haouthi na kuongoza muungano wa nchi 10 uliokuwa unapambana na kundi hilo.
Mapigano yaliyoathiri sana Yemen na kuathiri zaidi ya watu milioni 20
Ilikuwa June 20, 2017 historia ya MBS ilipobadilika, baada ya mwanamfalme aliyekuwa arithi mikoba, na aliyeteuliwa rasmi, Mohamed bin Nayef aliitwa na mfalme Salman na kumtaka akane wadhifa huo, ili MBS achukue nafasi.
Na kwa sheria zilivyo Saudi Arabia, nguvu ya mfalme haipingwi na anachokisema lazima kiheshimiwe, hakuna majadiliano. Baada ya kupewa mamlaka hayo, Novemba 2017 aliamuru kukamatwa kwa watoto
Ikaonekana kama mapinduzi yamefanyika bila umwagaji damu. Novemba 2017, akaamuru wanawafalme 200 waliokuwa maarufu wakamatwe kwa tuhuma za rushwa.
Watoto hao wa wafalme waliwekwa jela ya kifahari, ambayo ni hotel maarufu ya Ritz Carton huko Riyadh. Wengi walimkosoa MBS kwa hatua hiyo lakini hakujali.
Hakuna uhakika wa leo ama kesho chini ya MBS, kama Saudi Arabia itazingatia demokrasia. Wanaokosoa, wanaohoji masuala yoyote kuhusu familia ya kifalme ama sera zake wanajiweka katika hatari ya kuishia jela.
Kwa miaka mingi, MBS amekuwa akifurahia kuungwa mkono kwake na baba yake, mfalme Salman, na kwa mamlaka za kimahakama za kifalme, kesi ya Khashoggi ni kama itasahaulika tu.
Kwa alivyo, yeye ni Saudia Arabia na Saudi Arabia ni yeye. Na kwa utaratibu ulivyo baba yake atakapofariki, yeye ndiye atarithi mikoba yake katika taifa hilo la Mashariki ya kati, sio tu kwa muongo mmoja, bali pengine kwa miaka 50 ijayo.