Wanasayansi wagundua jinsi ''msongo wa mawazo unavyogeuza nywele kuwa mvi''

Woman looking at grey hairs appearing

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wanasayansi wanasema kuwa huenda wamegundua ni kwanini msongo wa mawazo husababisha nywele kugeuka kuwa nyeupe( mvi), na uwezekano wa kuzizuwia kuwa mvi bila kuweka rangi nyeusi.

Watafiti wa Marekani na Brazili walisema kuwa ugunduzi huu ulikua wa maana na unaofaa kurndelezwa ili kupata dawa inayoweza kuzuwia nywele kupoteza rangi yake kutokana na uzee.

Wanaume na wanawake wanaweza kuwa na nywele za mvi kuanzia wanapotimiza miaka 30, na kutokana na muda huu ambapo wengi huwa ni wazazi mtu anaweza kutambua ni lini rangi ya nywele hubadilika.

Ingawa kwa kawaida kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya ni mchakato wa kuongezeka kwa umri najeni, msongo wa mawazounaweza pia kuwa ni sababu sababu ya mtu kumea nywele za mvi.

Lakini wanasayansia hawakuelezea wazi ni vipi hasa msongo wa mawazo unaweza kuathiri nywele zilizoko vichwani mwetu.

Watafiti waliofanya utafiti huu uliochapishwa katika jarida la Nature kutoka Sao Paulo na Harvard, wanaamini athari zilikua na uhusiano na seli za melanocyte zinazotengeneza melanin ambayo hutengeneza rangi ya nwele pamoja na ngozi ya mwili

Na wakati wanafanya uchunguzi wao , waligundua ushahidi unaoonyesha kuwa msongo wa mawazo ni moja ya sababu za mtu kuota nywele za mvi.

"Kwa sasa tunafahamu kusema ukweli kwamba msongo wa mawazo unahusika katika mabadiliko haya kwa mwili wako na nywele, na jinsi mabadiliko yanavyotokea ," anasema Profesa Ya-Cieh Hsu, mwandishi wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Havard.

' Uharibifu ni wa kudumu'

Maumivu katika panya yalisababisha homoni za zinazoongeza mzunguko wa damu mwilini (adrenaline) na zile zinazochochea utendaji bora wa mwili (cortisol) na kufanya mapigo ya mioyo ya panya hao kwenda mbio , na kuongezeka kwa shinikizo la damu, jambo liloloathiri mfumo wa neva na kusababisha msongo mkubwa wa mawazo.

Mchakato huu uliharakisha kuongezeka kwa seli zinazoweza kubadilika ambazo hutengeneza rangi ya nywele.

"Nilitarajia msongo wa mawazo kuwa mbaya kwa mwili ," alisema Profesa Hsu.

" Lakini athari za msongo wa mawazo tulizozivumbua zilikua ni zaidi ya nilivyofikiria''

"Baada ya siku chache tu rangi zote za seli zilikua zimepotea.

"Zinapopotea , huwezi tena kutengeneza ranyi ya mwili au nywele - uharibifu unakua ni wa kudumu ."

The mouse before pain was induced (top), and some time afterwards (bottom image)

Chanzo cha picha, William A Goncalves

Maelezo ya picha, Panya kabla ya kupata maumivu (juu) na baada ya kuoata maumivu (picha ya chini )

Katika uchunguzi mwingine, watafiti, watafiti walibaini kuwa wanaweza kuzuwia mabadiliko kwa kuwapa panya dawa ya anti-hypertensive, inayotibu shinikizo la damu.

Na kwa kulinganisha jeni za panyawakati anapokua na maumivu na panya mwingine, waliweza kutambua protini inayohusika katika kuzuwia seli zisipate msongo.

Wakati protini hizi ( cyclin-dependent kinase (CDK) ) zilipozuiwa- matibabu pia yalizuwia mabadiliko ya rangi ya manyoya yake

Hili linaacha fursa kwa wanasayansi kusaidia kuchelewesha kumea kwa nywele za mvi kwa kulenga protini za CDK kwa dawa.

" Matokeo yao sio dawa ya kuzuwia nywele mtu kupata nywele za mvi," Profesa Hsu aliiambia BBC.

"Matokeo ya utawiti wetu, yaliyopatikana katika panya, ni mwanzo tu wa safari ndegu ya kutafuta jinsi tunavyoweza kutumia kwa watu.

"Pia inatupa wazo juu ya namna msongo wa mawazo unavyoweza kuathiri maeneo mengine ya mwili," alisema.