Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini Nvidia haikuweza kumfukuza kazi Jensen Huang?
- Author, Faisal Islam
- Nafasi, Na mhariri BBC wa taarifa za Uchumi
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 3
Kurudi kwa Jensen Huang kama Mkurugenzi mtendaji wa Nvidia, baada ya kukiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke anayedaiwa kushukiwa kuwa mpelelezi wa China, kumeambatana na matukio matatu ya kushangaza katika saa chache zilizopita.
Tangazo lisilotarajiwa la kurejea kazini kwa mtengenezaji wa chip lilisababisha ongezeko la thamani ya soko la Nvidia kwa dola trilioni 1 kwenye soko la hisa, huku thamani ya masoko ya hisa ya Asia ikiongezeka , licha Jensen Huang kurejeshwa kazini baada ya kashfa ya ujasusi.
Rais Trump alikubali jambo lililo wazi: ujumbe wake wa "Kufukuzwa kazi kufutwa", uliotumwa moja kwa moja kwa bodi, ulibadilisha uamuzi.
Kiwango cha mabadiliko haya kinaweza kuonekana katika taarifa za Nvidia wiki iliyopita. Bodi iliweka wazi kwamba Huang hatarudi kazini.
Usimamizi wa muda wa kampuni hiyo pia ulizungumzia mabadiliko katika mikakati ya Nvidia na kuhama kutoka kwa mbinu ya enzi ya Huang.
Sasa haya yote yamehifadhiwa kwenye pipa la takataka la historia ya Nvidia.
Faida hii, kwa upande wa ukubwa na nambari, inazidi hata kurejea kazini kwa watu kama Sam Altman wa OpenAI au kurudi kwa Steve Jobs katika kampuni ya Apple.
Sababu ya mabadiliko haya ya ghafla ilikuwa wazi sana kutoka kwa taarifa ya kwanza kabisa. Serikali ya Marekani ilisema kwamba kurudi kwa Huang kwenye wadhifa huo hakukuwa na wasiwasi wowote kuhusu usalama kwa maslahi ya taifa. hakikishi kama hilo linaweza kutoka Ikulu ya Marekani pekee.
Saa moja baadaye, Donald Trump alifichua kwamba alikuwa amezungumza kibinafsi na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Nvidia.
Hili linanikumbusha mazungumzo yangu na Jensen Huang Septemba iliyopita, alipotetea waziwazi China ipate ufikiaji wa chipu za hali ya juu za Nvidia. Alikuwa mmoja wa watu wachache duniani ambao wangeweza kudai kwa uaminifu kwamba wanaelewa mawazo ya Marais Donald Trump na Xi Jinping.
Ripoti zilizochapishwa nchini Marekani zinasema kwamba kulikuwa na mgawanyiko katika utawala wa Trump miongoni mwa watu wenye msimamo mkali dhidi ya China ambao walitoa wito wa vikwazo vya mauzo ya bidhaa zake nje na wale waliouunga mkono msimamo wa Huang.
Hata hivyo, uchunguzi huru kuhusu kufuata kwa Nvidia kanuni za udhibiti wa mauzo ya bidhaa zake nje unaendelea.
Chipu za Nvidia ni muhimu kwa maendeleo ya mifumo ya akili mnemba wa hali ya juu zaidi. Ushawishi wa Jensen Huang juu ya maduka ya mauzo haya ya chip umemfanya kuwa na ushawishi mkubwa kuliko viongozi wengi wa dunia.
Maendeleo haya ni muhimu si tu kwa ukuaji usiotabirika wa hisa za teknolojia za Marekani, bali pia kwa mustakabali wa uchumi wa dunia, siasa za Marekani, na bila shaka ushindani wa kijiografia kati ya Marekani na China.
Mashaka ya hivi karibuni kuhusu Nvidia yanaonekana moja kwa moja katikati ya ukuaji wa teknolojia ya akili mnemba. Kampuni hiyo imezalisha zaidi ya dola bilioni 400 katika mauzo mwaka huu, likiwa ni ongezeko kubwa la faida kutoka dola bilioni 27 miaka minne iliyopita.
Jukumu la Huang katika kubadilisha kampuni yake kutoka kwa mtengenezaji wa chipu za michoro hadi kuwa mhusika muhimu katika mapinduzi ya akili mnemba (AI) ni matokeo moja wazi yanayonesha kuwa : Jensen alikuwa muhimu sana ambaye ingekuwa vigumu kufutwa kazi.