Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ni vitamini gani ni muhimu kwa afya na ni vyakula gani vina kiwango kikubwa zaidi?
Katika ulimwengu ambapo "vyakula bora" vinapigiwa debe kwa njia inayotufanya tudhani kwamba vinatupatia virutubisho vyote tunavyohitaji, tunafaa kujiuliza: ni vitamini gani ni muhimu sana?
Na, kando na sukuma wiki , spinachi , mchicha, matembele au vyakula vyovyote tunavyovienda ni vyakula gani hutusaidia kukidhi mahitaji yetu ya kila siku?
Vitamini A
Wacha tuanze na jambo muhimu zaidi.
Vitamini A, pia inajulikana kama retinol, hupatikana katika vyakula kama vile mayai, samaki wenye mafuta na bidhaa za maziwa. Ina jukumu muhimu katika kudumisha ngozi yenye afya na mfumo wa kinga.
Lakini labda inajulikana zaidi kwa mchango wake katika kuona. Vitamini A hufunga rangi nyeti kwa mwanga kwenye fimbo na seli za retina, na kutusaidia kuona, hasa katika hali ya mwanga mdogo.
Upungufu wa vitamini A, ingawa si wa kawaida sana, unaweza kusababisha matatizo makubwa ya kuona na hata upofu. Chanzo kingine cha vitamini A ni beta-carotene, inayopatikana katika matunda na mboga zenye rangi angavu kama vile karoti, pilipili, mchicha na boga.
Mwili hubadilisha beta-carotene kuwa vitamini A, ndiyo sababu tunahusisha karoti na uonaji wa gizani.
Vitamini B
Vitamini B ni familia ya virutubisho vinane tofauti, kila kimoja kikiwa na idadi na kazi yake.
Vitamini B1 (thiamin) inasaidia mfumo wa neva na kusaidia usagwaji wa chakula tumboni.
Watu walio na ulevi sugu wako katika hatari fulani ya upungufu, ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa Wernicke-Korsakoff, ugonjwa mbaya wa neva unaoathiri kumbukumbu.
B2 (riboflauini) na B3 (niasini) zina kazi sawa, wakati B9 (folate) na B12 (cobalamin) ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu. Upungufu katika wa mojawapo ya vitamini hizi kusababisha upungufu wa damu.
Folate ni muhimu sana katika ujauzito wa mapema, kwani husaidia kuzuia kasoro za mirija ya neva kama vile spina bifida. Kwa hiyo, inashauriwa kwa wanawake wajawazito au wale wanaojaribu kupata mimba.
Vitamini B hupatikana katika aina zote za vyakula, kuanzia vyakula vya jamii ya kunde hadi nyama, samaki, na bidhaa za maziwa; ni familia pana ya virutubisho katika aina mbalimbali za vyakula.
Vitamini C
Vitamini C (asidi ascorbic) ni vitamini tunayoihitaji tunapohisi kuugua kutokana na virusi au hali ya uchovu baada ya kunywa pombe( hangover), na inajulikana kama vitamini "ya uponyaji" kwasababu nzuri. Inasaidia uponyaji wa jeraha, kusaidia ukarabati wa tishu, na inachangia katika matengenezo ya mishipa ya damu na mifupa.
Upungufu wa vitamini C husababisha kiseyeye, ugonjwa ambao hapo awali ulikuwa wa kawaida miongoni mwa mabaharia, na dalili kama vile uchovu, michubuko, unyogovu, na ugonjwa wa fizi.
Kwa bahati nzuri, vitamini C hupatikana katika matunda na mboga nyingi, hasa machungwa, limao au ndimu . Ndiyo maana mabaharia wa Uingereza wa karne ya 19 walipewa madini ya chokaa ili kuzuia kiseye, na kuwapatia jina la utani "limeys."
Vitamini D
Vitamini D ni muhimu kwa mifupa, meno, na misuli. Inaweza kufyonzwa kupitia lishe, hasa kutoka kwa samaki wa mafuta, mayai, na nyama, lakini mwili pia huizalisha kwenye ngozi kutokana na kuota jua.
Katika majira ya joto, watu wengi hupata vitamini D ya kutosha kwa kuwa nje. Hata hivyo, katika miezi ya baridi, chakula Cheney vitami hii ni muhimu na, ikiwa ni lazima, virutubisho huwa muhimu zaidi.
Upungufu ni wa kawaida zaidi, hasa katika maeneo yenye jua kidogo. Ukosefu wake unaweza kusababisha mifupa kuwa laini, dhaifu na kuwa na dalili kama vile maumivu ya mfupa, kuvunjika kwa mifupa, na ulemavu, ikiwa ni pamoja na mwonekano wa kawaida wa miguu iliyoipinda (au yenye matege). Kwa watoto, hali hii inajulikana kama matege ( au Crickets ); Kwa watu wazima, inaitwa osteomalacia.
Vitamini E
Mara nyingi hupuuzwa, vitamini E husaidia kulinda seli, kusaidia kuona, na kuimarisha mfumo wa kinga. Inapatikana katika karanga, mbegu, na mafuta ya mboga, na kwa kawaida ni rahisi kuipata kwa kiasi cha kutosha kupitia lishe mbalimbali.
Vitamini F
Kwa kweli sio vitamini, "vitamini F" ni jina la utani la asidi mbili za mafuta ya omega: asidi ya alpha-linolenic (ALA) na asidi ya linoleic (LA). Mafuta haya muhimu husaidia utendaji wa ubongo, kupunguza uvimbe, na kusaidia kudumisha ngozi yenye afya na utando wa seli.
Vitamini K
Hapana, hujakosa vitamini G hadi J—zimebadilishwa jina kwa miaka mingi. Lakini vitamini K ni halisi na ni muhimu kwa kuganda kwa damu.
Upungufu ni wa kawaida zaidi kwa watoto na unaweza kusababisha michubuko na kutokwa na damu ambayo ni vigumu kukoma. Virutubisho vinafaa na hutolewa baada ya kuzaliwa.
Watu wazima wengi hupata vya kutosha kupitia vyakula kama vile mboga za kijani kibichi na nafaka ambazo hazijachakatwa.
Na mshindi ni...
Vitamini hizi zote ni muhimu, na vzote hupatikana katika aina mbalimbali za vyakula vya kila siku. Lakini ni chakula gani hutoa kiasi kikubwa zaidi?
Sukuma wiki au spinachi , samaki wenye mafuta, na mayai huchukua nafasi ya pili, ya tatu, na ya nne. Lakini nambari moja ni maini
Ndio, maini. Chakula hicho tulikiogopa sana kama watoto na ambacho mara nyingi kilipikwa kupita kiasi katika mikahawa ya shule. Lakini pia kina vitamini A, B, D, na K nyingi.
Kwa kweli, maini yana vitamini A nyingi sana kiasi kwamba inashauriwa kuyala mara moja tu kwa wiki ili kuepuka sumu ya vitamini A, na kutoyala kabisa ikiwa una mjamzito
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi