Kombe la Dunia 2026: Kipi cha kukitarajia katika nusu fainali?

- Author, Adwaidh Rajan
- Nafasi, BBC
- Iliyochapishwa
- Muda wa kusoma: Dakika 4
Kombe la Dunia sasa limesalia na mataifa manne tu tunapoelekea nusu fainali. Ufaransa, Uhispania, Uingereza na Argentina.
Tutarajie nini katika mechi nne za mwisho?
Ufaransa & Uhispania

Chanzo cha picha, Getty Images
Ufaransa dhidi ya Uhispania, Uwanja wa Dallas, Jumanne. Kwa kuwa timu kali zaidi barani Ulaya zitakabiliana, mechi hii ina sifa zote ya kuwa fainali ya Kombe la Dunia.
Kylian Mbappe alitawala vichwa vya habari tena huku Ufaransa ikiishinda Morocco 2-0 na kufika nusu fainali, akifikisha jumla ya mabao manane katika mashindano hayo na kuwa nyuma ya Lionel Messi kwa bao moja tu katika kinyang'anyiro cha kuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia.
Nguvu kubwa ya Ufaransa ni ubora wao uwanjani, huku Ousmane Dembele akifunga bao la ushindi katika robo fainali na kufikisha idadi ya mabao matano.
Michael Olise ametoa cheche ya ubunifu kwa timu ya Didier Deschamps na anaongoza mashindano hayo akiwa na pasi tano za mabao.
Ubora huo ni muhimu dhidi ya timu ya Uhispania, ambayo iliwashinda Ufaransa 2-1 katika nusu fainali na kisha kushinda Euro mwaka 2024.
Kuna hisia kwamba Uhispania ni bora zaidi. Kivutio chao kikuu ni Lamine Yamal ambaye bado hajaonesha makali yake kikamilifu katika Kombe la Dunia. Winga huyo wa Barcelona amefunga bao moja tu - dhidi ya Saudi Arabia katika hatua ya makundi.
Mikel Oyarzabal aliyefunga mabao manne ameshindwa kufunga katika mechi mbili zilizopita, hivyo kikosi cha Luis de la Fuente kilihitaji uingiliaji kati wa dakika za mwisho kutoka kwa mchezaji mbadala Mikel Merino ili kuwashinda Ureno na Ubelgiji katika raundi ya mtoano.
Wakitaka kuongeza ushindi wa kombe la dunia, mbali na ule wa 2010, Uhispania wanatumai Yamal, ambaye atatimiza miaka 19 usiku wa kuamkia leo, ataitumia nusu fainali hii kuonyesha uwezo wake zaidi.
Takwimu muhimu

Chanzo cha picha, Getty Images
Ufaransa itacheza katika nusu fainali yao ya nane ya Kombe la Dunia, ikilingana na Brazil, huku Ujerumani pekee ndio imecheza nusu fainali 12.
Uhispania wako kwenye rekodi bora zaidi zaidi ya kutoshindwa katika historia yao na sasa wameepuka kushindwa katika kila mechi kati ya 36 zilizopita tangu walipopoteza 1-0 dhidi ya Colombia Machi 2024. Wameshinda 27 na kutoka sare tisa kati ya mechi zao katika kipindi hicho.
Huu utakuwa mchezo wa pili tu wa Kombe la Dunia kati ya timu hizo. Ufaransa ama Les Blues walitoka nyuma dhidi ya Uhispania na kushinda 3-1 walipokutana katika raundi ya 16 mwaka 2006.
England & Argentina

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
England dhidi ya Argentina, Uwanja wa Atlanta, siku ya Jumatano. Hii itakuwa nusu fainali ya pili ya Kombe la Dunia kwa England tangu 2018, lakini mabingwa watetezi Argentina wanacheza na Three Lions kwa mara ya kwanza baada ya miaka 60.
Ni mechi iliyojaa shauku na ushindani – kwani ni miaka 40 imepita tangu Diego Maradona kuitoa England katika hatua ya robo fainali nchini Mexico.
Wakati huu, Argentina ina nyota mwingine nambari 10 katika safu yao ya ushambuliaji. Lionel Messi ambaye hajawahi kukutana na England.
Messi mfungaji bora wa muda wote wa Kombe la Dunia katika mashindano haya, kwa sasa anaongoza mbio za Golden Boot pamoja na Kylian Mbappe wa Ufaransa, wakiwa na mabao manane.
Lakini Uingereza ina namba 10 wao hatari, Jude Bellingham, amefunga mabao mawili katika kila moja ya michezo yake miwili iliyopita ya mtoano - huku nahodha Harry Kane akiwa na mabao sita hadi sasa.
Hakuna taifa lolote kati ya haya mawili ambalo limeonesha kiwango kikubwa sana katika Kombe la Dunia hili la sasa, zote zimehangaika katika kushinda katika hatua za mtoano ili kufikia hatua hii.
Hata kocha wa Thomas Tuchel wa England, ameitaka timu yake ionyeshe ubora zaidi kuliko walivyofanya katika ushindi wa robo fainali dhidi ya Norway.
Takwimu muhimu

Chanzo cha picha, Getty Images
England imefika nusu fainali katika mashindano manne makubwa tangu 2018. Timu ya Three Lions imeshinda michezo minne mfululizo ya Kombe la Dunia, rekodi yao nzuri zaidi ya ushindi ndani ya shindano moja tangu 1966.
Tuchel ni kocha wa pili wa Uingereza kutoshindwa katika michezo yake sita ya kwanza ya Kombe la Dunia akiwa kocha – wa kwanza alikuwa Alf Ramsey mwaka 1966, baada ya mechi sita (alishinda tano, sare moja).
Argentina wamefika katika fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya tatu katika matoleo manne yaliyopita - 2014, 2022, 2026. Kabla ya 2014, hawakuwa wamefika nusu fainali tangu 1990.














