Tetesi za soka Ulaya: Arsenal waanza mazungumzo na Araujo, Man Utd 'kutimua' wachezaji 13

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Arsenal wamefungua mazungumzo na Maxi Araujo (26) wa Sporting, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City na Manchester United. (Record)
Manchester United inaweza kuwaruhusu hadi wachezaji 13 kuondoka Old Trafford majira haya ya kiangazi huku INEOS wakipanga kufanya mageuzi makubwa ya kikosi. (Express)
United pia imemuweka kwenye orodha ya wachezaji inayowahitaji Ederson (26), kiungo wa Atalanta na Brazil. (Talksport)
Tijjani Reijnders (27) anavivutia vilabu vya Ligi Kuu England na Ulaya baada ya msimu mgumu akiwa Manchester City. (Calciomercato)
Liverpool wako tayari kulipa euro milioni 60 kumsajili Abde Ezzalzouli (24) kutoka Real Betis. (Fichajes)
Barca, Man Utd wanatoana macho kwa Leao

Chanzo cha picha, Getty Images
AC Milan wako tayari kumuachia Rafael Leao (26), huku Manchester United na Barcelona zikivutiwa naye kwa ada ya karibu euro milioni 60. (Calciomercato)
Arsenal wanamfuatilia Endrick (19), ambaye yupo kwa mkopo Lyon, na wanaweza kumsajili ikiwa hatakuwa kwenye mipango ya Real Madrid. (Caught Offside)
Lucas Bergvall (20) anatarajiwa kukataa ofa kutoka Chelsea na Aston Villa na kubaki Tottenham iwapo watakwepa kushuka daraja. (Football Insider)
Bernardo Silva (31) hataki kujiunga na klabu nyingine ya Ligi Kuu England lakini anataka kubaki Ulaya. (Football Insider)
Coventry wanapanga kutumia pauni milioni 200 kujiandaa na maisha ya Ligi Kuu, wakilenga kusajili wachezaji kama Pau Torres (29) na Conor Gallagher (26). (Fichajes)













