Mataifa 10 ya Afrika yaliyo na uwezo mkubwa wa kiviwanda: Morocco yaipiku Afrika Kusini

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 5

Afrika imeshuhudia mabadiliko katika ukuaji wa kiuchumi kati ya Morocco na Afrika Kusini mwaka uliopita 2025, kulingana na Kielezo cha Maendeleo ya Viwanda cha Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB). Kulingana na ukuaji halisi wa viwanda (utengenezaji, mauzo ya nje, na ongezeko la thamani ya bidhaa), pamoja na Pato la Taifa, nchi kama vile Senegal, Namibia, na Eswatini zimepata mafanikio makubwa

Ni muhimu kusisitiza kwamba hii sio orodha ya utajiri wa jumla, bali ni orodha inayoangazia ukuaji wa viwanda iliyoanzishwa kwa misingi ya vigezo kama vile ongezeko la thamani ya viwanda, miundombinu ya viwanda, usindikaji wa ndani wa rasilimali, mauzo ya nje ya viwanda, na kadhalika.

1. Morocco

Mafanikio ya Morocco, kuwa kiongozi mpya wa viwanda barani Afrika, yalichangiwa na ukuaji wa ya sekta ya magari na anga, maeneo ya viwanda yenye mwelekeo wa mauzo ya nje, miongoni mwa mambo mengine.

"Morocco sasa ndiyo uchumi ulio karibu zaidi na mipaka ya maendeleo ya viwanda, ikiwa na alama 0.8415, ambayo inaiweka pointi 0.1585 kutoka kwa thamani ya juu ya 1," ripoti ya AfDB inaonyesha.

"Kwa mara ya kwanza katika kipindi kilichoainishwa na ripoti hiyo, Morocco imeipiku Afrika Kusini na kuwa taifa lenye uchumi wa juu wa viwanda barani Afrika - utendaji unaoakisi uboreshaji endelevu wa mfumo wake wa uzalishaji, kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zake mseto na utekelezaji mzuri wa sera yake ya viwanda," ripoti hiyo ilisema

2. Afrika Kusini

Madini, sekta ya magari, kemikali, vitu vilivyoifanya Afrika Kusini kuwa msingi wa kihistoria wa kiviwanda.

"Afrika Kusini ilipata alama 0.8396 mwaka 2024, kiwango chake cha juu zaidi tangu 2020, lakini bado ni chini ya utendaji wake wa kabla ya janga la COVID-0.8518 mwaka 2019," inaeleza ripoti ya AfDB.

"Afrika Kusini inasalia kuwa nchi yenye nguvu ya kiviwanda katika barani, lakini inaendelea kushuhudia kushuka kwa kasi kwa ushindani wake wa viwanda," inaeleza ripoti hiyo.

3. Misri

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Misri inzingatiwa kuwa nchi yenye nguvu ya kiviwanda katika eneo la Afrika Kaskazini, inashika nafasi ya tatu barani Afrika. Ufanisu huu ulichangiwa na sekta zake za nguo, kilimo biashara, na saruji. Misri pia inajivunia kuwa na soko kubwa la ndani.

"Mwaka huu pia unathibitisha kuorodheshwa kwa Misri katika nafasi ya tatu, nafasi ambayo ilifikia kwa mara ya kwanza mwaka 2020 na ambayo iliichukua kutoka Tunisia, ambayo imesalia katika nafasi ya nne," inaeleza ripoti hiyo.

4. Tunisia

Tunisia imepiga hatua ya kiviwanda barani Afrika kutokana na ufanisi wa sekta yake ya viwanda inayolenga mauzo ya nje. Nchi inazalisha na kuuza nje vifaa vya magari, vifaa vya elektroniki, na nguo.

"Hata hivyo, Tunisia imeonyesha mwelekeo wa kupanda tangu 2022, na kupunguza pengo na Misri (ikiwa na alama 0.7827 dhidi ya 0.7760, mtawalia)," ripoti ya AfDB inasema.

5. Mauritius

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Mauritius ni uchumi mdogo ambao umenufaika kutokana nakuimarika kwa viwanda vyake vyenye nguvu. Hii inachangia ongezeko la ya mauzo ya nje katika sekta ya nguo, huduma za viwandani, na biashara huria.

"Mauritius imeorodheshwa ya tano lakini iko nyuma kwa kiasi kikubwa, ikiwa na alama 0.6731 mwaka 2024, ambayo ni zaidi ya pointi 0.1 chini ya nchi nne zilizoimarika kiuchumi."

"Mauritius, Eswatini na Namibia ziko nyuma ya Afrika Kusini na ni miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa katika ukanda wa kusini mwa Afrika," ripoti hiyo inafichua.

6. Algeria

Ukuaji wa viwanda wa Algeria unasukumwa na sekta yake ya nishati, na ukuaji wa sekta ya mafuta, ujenzi, na kadhalika. Algeria pia inafanya juhudi kubwa kubadilisha tasnia yake.

Ikiwa na alama 0.6661, Algeria ni miongoni mwa nchi zilizofanya vyema katika faharasa hii ya ukuaji wa viwanda barani Afrika kwa mwaka wa 2025.

7. Eswatini

Eswatini imefikia ukuaji wakr wa kiviwanda kutokana na sekta ya nguo yenye mwelekeo wa mauzo ya nje na ushirikiano wake katika biasha ya kikanda. Ikiwa na alama 0.6509, Eswatini ni kati ya nchi 10 zinazofanya vizuri kulinga na viwango vya AfDB.

"ukuaji wa kiviwanda wa Eswatini umeendelea kuwa thabiti kwa muda, na mabadiliko makubwa yanahusu nafasi ya sita, imekuwa iikipiganiwa kati yake na Algeria na tangu 2010 (isipokuwa 2023, wakati Algeria ilipoishinda Mauritius na kushika nafasi ya tano)," ripoti hiyo inasema.

8. Senegal

Ukuaji wa haraka na wa kimkakati wa Senegali umefikiwa kupitia maendeleo ya sekta yake ya viwanda vya kilimo na soko la ndani. Mbali na ujenzi wa hivi majuzi wa miundombinu ya viwanda, yenye alama 0.6368, Senegal "imepiga hatua kutokana na uboreshaji wa viashiria vyake vya moja kwa moja, hasa uwekezaji na ufadhili wa sekta binafsi."

"Kwa upande wa viwango, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djibouti, Gabon, Benin, Mauritania, Somalia, Senegal, Rwanda, Guinea na Sierra Leone ziliimarika, na kupata nafasi tano au zaidi katika kipindi kilichozingatiwa," ilibaini ripoti hiyo.

9. Namibia

Kwa muundo wa uundaji wa viwanda vya madini, Namibia ilipata alama 0.6295, ikishika nafasi ya 9 katika orodha ya Maendeleo ya Viwanda ya AfDB ya 2025 (IDI). Nchi hii inachakata rasilimali zake za madini na kuwekeza kwenye vifaa na nishati.

Namibia ni miongoni mwa nchi zilizoorodheshwa zaidi Kusini mwa Afrika, pamoja na Afrika Kusini, Mauritius na Eswatini.

10. Ivory Coast

Kipitia uimarishaji wambinu za ukuzaji wa kakao na ukuzaji wa chakula cha kilimo, Ivory Coast imepanda hadi nafasi ya 10 kwa alama 0.6173.

"Juhudi zimefanywa, haswa katika usindikaji wa malighafi. Ikumbukwe kuwa Côte d'Ivoire kimsingi ni nchi ya kilimo yenye uzalishaji mkubwa wa bidhaa za kilimo kila mwaka.

Tangu 2016, serikali imefanya mageuzi ambayo yameimarisha mfumo mpya wa uwekezaj, hususan uwekezaji wa kigeni katika sekta kama vile kakao, ambayo leo hii imefikia viwango vya juu- 46% ya kiwango cha usindikaji wa kakao," Emmanuel Travis, Mkurugenzi Mkuu wa Viwanda katika Wizara ya Biashara na Viwanda ya Ivory Coast, alielezea BBC.

Nchi kama Kenya, Gabon, DR Congo, Nigeria na Botswana zinafuata katika 10 bora mtawalia.

Afŕika haitegemei tena uuzaji wa nje wa malighafi zake, lakini inazibadilisha kwa kutengeneza nafasi za kazi na kuongeza thamani.