BBC News, Swahili - Habari
Habari Kuu
Kenya yathibitisha visa vinne vipya vya Ebola, idadi yafikia saba
Wizara imesema mgonjwa mpya wa kiume alikuwa tayari amewekwa karantini tangu tarehe 6 Oktoba 2026. Wahudumu watatu wa afya, wanaume wawili na mwanamke mmoja wenye umri wa miaka 29, 35 na 32 mtawalia, wamekuwa karantini tangu tarehe 9 Oktoba.
Iran yakanusha kuhusika na mashambulizi ya Wahouthi nchini Saudi Arabia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amekataa madai yoyote yanayoiunganisha nchi hiyo na mashambulizi ya Wahouthiakieleza wako tayari kuwa wapatanishi kati ya Wahouthi na Riyadh ili kufanikisha maridhiano.
Mshindi wa taji la Miss Grand International 2026, Jihan Dimack, apokelewa kwa shangwe Tanzania
Jihan amesema anajivunia kuzaliwa Tanzania, nchi anayoitaja kuwa mfano wa amani, upendo na umoja. Alieleza kuwa Watanzania wana utamaduni wa kuishi na kufanya kazi kwa ushirikiano, bila kujali tofauti za asili, dini au mila.
Vita vya Iran, Wahouthi na makubaliano na Putin: Migogoro mitatu inayofungamana Washington
Wakati mashambulizi ya Wahouthi yaliyosababisha vifo vya watu katika uwanja wa ndege wa Riyadh yakiongeza hatari ya vita dhidi ya Iran kupanuka, athari za mzozo huo zimefika hadi Washington, ambako juhudi za Donald Trump za kudhibiti bei za mafuta kupitia makubaliano na Urusi zimekabiliwa na ukosoaji, hata miongoni mwa Warepublican.
Wagombea wote 7 wa ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wapingwa na kura ya turufu
Taarifa za vyombo vya habari vya Marekani zinaashiria kuwa Washington inawapinga wagombea wote saba wanaowania nafasi hiyo.
Kwa nini mkataba wa Rwanda wa kuandaa mbio za Langalanga-F1 bado unazua utata
Mashindano ya Formula 1 yanatarajiwa kurejea barani Afrika mwanzoni mwa miaka ya 2030, lakini mkataba wa Rwanda wa kuandaa mbio hizo umezua tuhuma kwamba nchi hiyo inatumia michezo kuboresha taswira yake ya kimataifa.
Tetesi za Soka Jumamosi: Bellingham akubali mkataba mpya Real Madrid
Kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham, yuko tayari kuendeleza maisha yake ya soka katika uwanja wa Santiago Bernabéu. Arsenal na Liverpool zimeelezwa gharama ya kumsajili winga wa Brentford, Kevin Schade, huku Manchester United na Chelsea zikiwa miongoni mwa klabu zinazofuatilia mustakabali wa Jules Koundé katika Barcelona.
Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola
Mgonjwa huyo ni mwanamke mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni ndugu wa karibu wa wagonjwa wa kwanza na wa pili waliothibitishwa kuwa na maambukizi hayo.
Nani anayeongoza Kanisa Katoliki wakati Papa anapougua?
Wataalamu wanaeleza kuwa sheria za kanisa (canon law), ambazo zinafafanua kwa kina taratibu za kumrithi Papa anapofariki au kujiuzulu, hazitoi mwongozo wa kutosha katika hali ambapo Papa bado yuko hai lakini hawezi kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
Je, kaswende inaweza kuambukizwa kwa kubusiana?
Kabla ya mwaka 2021, Sri Lanka ilikuwa ikiripoti visa vya kaswende visivyofikia 100 kwa mwaka. Hata hivyo, kwa mujibu wa daktari bingwa Nimali Jayasuriya, idadi hiyo imeongezeka kwa kasi na kufikia visa 1,500 kwa mwaka hivi sasa.
Iran: Lango la Hormuz halitafunguliwa hadi Marekani itakapoondoka
Msemaji wa jeshi la Iran, Mohammad Akraminia, amesema kufunguliwa tena kwa Mlango-bahari wa Hormuz kunategemea kuondoka kwa vikosi vya Marekani katika eneo hilo.
Mashambulizi ya Houthi dhidi ya Saudi Arabia yataathiri ibada ya Umrah?
Katika siku za hivi karibuni, wanamgambo hao wameshambulia viwanja muhimu vya ndege nchini Saudi Arabia, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Riyadh.
Unataka kupunguza gharama za data?
Soma mtandao wetu wa maandishi kwa gharama ndogo za data.
Gumzo mitandaoni
Joseph Kabila: Kutoka urais hadi kuongoza muungano unaojumuisha M23
Kwa zaidi ya miongo miwili, Joseph Kabila Kabange amekuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za DRC.
Mwaka mmoja baada ya Raila: Nini kimebadilika?
Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga kimeacha alama kubwa katika siasa za Kenya, huku mjadala ukiendelea kuhusu urithi wake na mwelekeo wa kisiasa alioujenga kwa zaidi ya miongo minne.
BBC Africa Eye: Ni nani aliwapiga risasi waombolezaji wa Raila Odinga?
Uchambuzi wa BBC Africa Eye wa video na picha 1,500 umeonyesha kuwa waliouawa katika hafla ya kumuaga Raila Odinga hawakuwa karibu na eneo la vurugu.
Mataifa saba yanayolipa mshahara mkubwa zaidi Afrika
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya iliwapiku majirani zake Tanzania, Uganda na Rwanda, lakini ikabaki nyuma ya Djibouti, ambayo ndiyo iliyoongoza sio Afrika Mashariki pekee bali pia bara zima kwa wastani wa dola 2,836 kwa mwezi.
'Mwaka mmoja bila Polepole umekuwa mgumu sana'- Familia
Kaka yake, Godfrey Polepole, ameiambia BBC kuwa familia imekuwa ikipitia kipindi kigumu tangu kutoweka kwa ndugu yao, huku juhudi za kumtafuta zikigonga mwamba.
Wafahamu wafanyabiashara wenye utata kama Wicknell Chivayo
Kilichowaunganisha wengi wao ni simulizi ya kuanzia maisha ya kawaida au ya umaskini na baadaye kufikia utajiri mkubwa na ushawishi wa kisiasa au kijamii.
Kwa nini Marekani iliziondoa kwa ghafla ndege zake za kurusha mabomu kutoka Uingereza?
Hatua ya ghafla na ya kina ya kuondolewa kwa ndege nzito za Marekani zenye uwezo wa kubeba mabomu siku ya Jumapili ilikuja kwa kasi kiasi cha kuacha kila mtu akijiuliza ni nini kilichosababisha hatua hiyo
Mambo 5 muhimu kuhusu mradi wa kiwanda cha mafuta cha Dangote nchini Kenya
Mradi huo unatajwa kuwa miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya miundombinu kuwahi kutekelezwa nchini Kenya tangu ilipopata uhuru.
Miji bora zaidi duniani mwaka 2026 na siri za mafanikio yake
Ni nini kinachoufanya mji uwe wa kuvutia kiasi cha watu kutaka kuishi humo, kufanya kazi au hata kuutembelea?
Mwaka mmoja bila Raila: Ni nani amenufaika zaidi na pengo aliloacha katika siasa za Kenya?
Hakuna mwanasiasa mwingine katika historia ya kisasa ya Kenya ambaye ameacha pengo la kisiasa linalozua mjadala mkubwa kama Raila Odinga.
Sir Wicknell alipataje utajiri wake?
Chivayo ameacha kampuni, mali na mahusiano na watu wenye ushawishi, lakini pia ameacha maswali ambayo huenda baadhi ya majibu yake ameondoka nayo.
Uvumbuzi 9 wa kijeshi wa ajabu zaidi kuwahi kubuniwa duniani
Wasovieti walihitaji njia ya kuzuia vifaru vya Wanazi haraka. Afisa mmoja akatoa pendekezo la kikatili na la kushangaza: kwa nini wasitumie mbwa?
BBC News Swahili sasa ipo WhatsApp
Vipindi vya Redio
Listen Next, Amka Na BBC, 05:59, 19 Oktoba 2026, Muda 29,30
Kipindi cha habari, mahojiano na makala kila siku saa kumi na mbili na saa moja asubuhi Afrika Mashariki
Sikiliza, Dira Ya Dunia, 18:29, 16 Oktoba 2026, Muda 1,00,00
Kipindi cha habari, makala na mahojiano cha kila siku kuanzia saa kumi na mbili unusu jioni Afrika Mashariki
Sikiliza, Amka Na BBC, 06:59, 16 Oktoba 2026, Muda 29,30
Kipindi cha habari, mahojiano na makala kila siku saa kumi na mbili na saa moja asubuhi Afrika Mashariki
Sikiliza, Amka Na BBC, 05:59, 16 Oktoba 2026, Muda 29,30
Kipindi cha habari, mahojiano na makala kila siku saa kumi na mbili na saa moja asubuhi Afrika Mashariki
Dira ya Dunia TV
Kipindi cha habari motomoto, kinachowaweka watazamaji karibu zaidi na yanayojiri duniani























































