Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Tume ya uchunguzi yasema Watu 518 walifariki dunia wakati wa ghasia za uchaguzi Tanzania

Ripoti hii inachukuliwa kama nyenzo muhimu ya kuweka wazi ukweli na kutoa mwelekeo wa taifa baada ya kipindi hicho kigumu.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Martha Saranga, Rashid Abdallah & Ambia Hirsi

  1. Kuna madai ya watu kuuawa katika nyumba zao – Tume

    Tume imepokea madai kutoka kwa waathirika na mashahidi kuwa kuna watu waliuawa au kujeruhiwa katika maeneo ambayo hayakuwa na ghasia wala vurugu.

    Kuna madai ya watu kupigwa risasi katika nyumba makazi yao, ikiwa pamoja na ndani ya nyumba, sebuleni au ndani ya maduka.

    Hizi ni tuhuma nzito za uwezekano wa matumizi ya silaha nzito kinyume na sheria za kimataifa na kikanda.

  2. Idadi ya waliofariki inaweza kuwa kubwa zaidi

    Tume imebaini kuwa kuna uwezekano kuwa badhi ya familia zimezika wapendwa wao bila kuwafikisha katika vituo vya kutolea huduma ya afya au hawakupata fursa ya kuja mbele ya tume.

    Tume pia inasema inawezekana kuwepo kwa majeruhu ambao walitbiwa nje ya mfumo rasmia na taarifa zao kutofikishwa katika vituo rasmia.

    Tume pia imepokea taarifa za watu kupotea au kutopatikna tangu wakati wa matukio ya vurugu za uchaguzi mkuu.

    Tume pia imepokea ushahidi kuwa watu 39 ambao familia ziliona miili ya wapendwa wao katika hospitali na vituo vya afya, na kutambuliwa lakini miili hiyo baadaye haikuonekana tena.

    Kwa kuzingantia hayo idadi ya vifo vya watu 518 inaweza kuwa sio idadi kamili ya waliofariki.

  3. 'Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni'

    Baadhi ya waathiriwa wa vurugu hizo waliopoteza wapendwa wao wameeleza hisia zao kwa BBC, wakisimulia maumivu, hofu na matumaini waliyonayo kufuatia tukio hilo.

    Mwanaume huyu tumehifadhi utambulisho wake alimpoteza kijana wake aliyefariki dunia kutokana na majeraha ya risasi aliyopata alipokuwa akitoka katika shughuli zake.'kijana wangu ameniachia mtoto mdogo' anayenitegemea.

    Kwa upande mwingine wake Mwanaume huyu anasema ripoti hii inamkumbusha machungu ya kumpoteza mke wake wa ndoa.'Nina wakati mgumu,tangu oktoba 30 nilimpoteza mke wangu wa ndoa'

    'Alipigwa risasi akiwa dukani kwake amekaa,nilimkuta ameshafariki dunia' alieleza. Wasamaria walinisaidia kumpeleka hospitali.Ripoti hii haina maana yoyote kwangu ikiwa hatutapata haki'.

  4. Dar es Salaam yaongoza kwa vifo wakati wa vurugu

    Huku idadi ya waliofariki wakati wa vurugu ikiwa ni watu 518, idadi ya waliofariki wanaume 490 sawa na asilimia 94.6, na wanawake 28, sawa na asilimia 5.4.

    Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa waliofariki ukiwa na vifo 182, Mwanza 90, Mbeya 80 na Arusha 53. Na 21 viikuwa vifo vya watoto. Na vifo 16 walikuwa askari na maafisa wa usalama.

  5. Tume yataja malengo ya walioshiriki katika vurugu

    Kuzuia uchaguzi: Lengo kuu ni kvurugu na kuzuia uchaguzi, lengo hili linathibitshwa na matukio mbali mbali, ikiwemo kushambulia askari, mawakala na wasimamizi wa uchaguzi, kuharibu mali za wasimamizi, vitisho, kuvamia vituo vya uchaguzi, kupora mali, kutishia waliojitokeza kupiga kura na waliopiga kura kukakwa au kujaribiwa kukatwa vidole.

    Kufikisha ujumbe: Tume inasema miongoni mwa walioshiriki katika vurugu ilikuwa ni kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa serikali, tume inasema vijana walioshiriki walipata mwanya wa kufikisha ujumbe kwa serikali kuwa wanataka kusikilizwa.

    Wizi na uporaji: Miongoni mwa wafanya ghasia, walijitokeza makundi ya waliopora mali na kuiba. Uporaji ulitokea katika maduka na maeneo mengine ya biashara yaliyotembelewa na tume.

  6. Mbinu 16 zilitumika kufanikisha ghasia na vurugu - Tume

    Ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, 2025, chini ya Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mohamed Chande, amesema takaribani mbinu kumi na sita zilitumika wakati wa kutekeleza vurugu hizo.

    Akitaja baadhi ya mbinu hizo amesema, kuweka vizuiz barabarani, kuchoma moto, matumizi na ishara mbali mbali za kutambuliana, matumizi ya pikipiki, kufanya ghasia katika maeneno mengi kwa wakati mmoja.

  7. Tume yasema matukio ya vurugu yalifadhiliwa

    Tume imepata ushahidi kuwa matuko ya vurugu yalipangwa, yaliratibiwa, yalifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo.

    Waratibu walitumia mbinu mbalimbali, ikiwemo kuwasajili vijana.

    Tume hiyo inasema waratibu hao walikuwa wakizunguka maneno mbalimbali katika vyuo vikuu, masoko na vituo vya mabasi, na kuwaandikisha watu ili kushiriki katika ghasia za Oktoba 29.

    Tume inasema waratibu hawakumamatwa kwa sababu hawakuwepo wakati wa vurugu.

  8. Wanasiasa na Wanaharakati watajwa kuchochea vurugu Oktoba 29

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, Jaji Mohamed Chande, amesema kauli mbiu na matamko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na waharakati yalichochea vurugu, kwani walitumia changamoto za wananchi, kama fursa za kuwashawishi kushiriki ghasia hizo.

    Tume imebaini kulikuwa na vichocheo vikubwa vitatu vya kufanya ghasia:

    Mitandao ya kijamii: Amesema mitandao ilitumika kabla na baada ya uchaguzi mkuu, na wabuni mada ambao walihamasisha watu wasishiriki katika uchaguzi mkuu au kuhakikisha haufanyiki.

    Kauli mbiu: Amesema baadhi ya wanasiasa waliwahamasisha watu kufanya ghasia kwa kutumia kauli mbiu kama, "no reforem no election, Oktoba hatutiki, Oktoba tunatoka, tumedhamiria uchaguzi hautofanyika, Samia Must God, Tunataka kukomboa nchi yetu, hakuna uchaguzi chini ya serikali hii, tunahakikisha nchi haisimami, hakutakuwa na uchaguzi bila mabadiikio ya mfumo, serikali imepoteza uhalilia, serikali iondoke, wagombea sio halali.

    Wanasiasa: Kundi la tatu la vichocheo, ni baadhi ya maeneo ya nchi ambapo wagombea wa viti vya udiwani na ubunge, ambao waliona ghasia zinawasaidia kudai mabadiliko ya mfumo na kupata wagombea ndani vya vyama vyao, nao waliwahamasisha wafuasi wao kufanya ghasia.

  9. 'Walinipa mchongo utakaonitoa kwenye umaskini' - shahidi

    Shahidi aliyefika mbele ya tume aliiambia Tume jinsi alivyopewa pesa ili kushiriki kwenye maandamano yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa Tanzania.

    Kwa mujibu wa mwanyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktona 29 Othman Chande baathi ya wa waandamanaji walipewa hadi shi;ingi 10,000 za Tanzania kushiriki.

    Wizi na uporaji ulishuhudiwa baada ya makundi makubwa ya watu kujitokeza kuanza kuiba na kupora mali na kulikua ushahidi wa picha mjongea na mnato.

  10. Hayakuwa maandamano ya amani bali ghasia- Jaji Chande

    Tume imehitimisha kuwa maandamano yaliyofanyika hayakuwa ya amani bali ghasia kinyume cha katiba na sheria.

    Ni haki ya kikatiba ya kila mtu kupiga kura, ghasia zilipangwa na kutekelezwa siku ya kutekeleza haki ya kikatiba ya wananchi kupiga kura.

    Hitimisho la tume kilichotokea siku ya uchaguzi mkuu, haikua maandamano ya amani bali ghasia, hayakuzingatia matakwa ya katiba na sheria za nchi

  11. Waandamanaji walipewa simu- Jaji Chande

    Matumizi ya mitandao ya kijamii, waliibuka wabuni mada kwenye mitandao, ikiwemo mada za kutoshiriki uchaguzi mkuu, na kupanga mbinu na kuwaelekeza waliokubali vurugu.

    Walioshiriki kufanya ghasia, waliokuja mbele ya tume, walipewa simu za mkononi na kupiga picha za maeneo mbalimbali ya ghasia na kurusha moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii ili kuibua hasira kwa wananchi, na waliaminishwa jeshi la Tanzania lipo upanda wao. anaendelea kusema Mwenyetkiti wa Tume Othman Chande.

  12. Vyanzo vya ghasia: Tume yabainisha vyanzo vitano na vichocheo

    Jaji Chande ametaja sababu za kisiasa ,ikiwemo madai ya Tume huru ya uchaguzi, changamoto za kiuchumi ajira ugumu wa maisha, kijamii kama vile kukosekana kwa uzalendo kuwa miongoni mwa vyanzo vya ghasia za uchaguzi wa Oktoba 29.

    Kwanza: Masuala ya kisasa ikiwemo madai ya katiba mpya, maboresho ya tume huru ya uchaguzi

    Pili: Masuala ya kijamii, ukosefu wa ajira, maisha magumu na mazingira ya kibiashara, utitiri wa kodi

    Tatu: masuala ya kijamii yanayohusisha mmonyoko wa maadili na kukosa uzalendo na kutokushughuliwa kwa madai ya rushwa, kupotea na kutekwa kwa watu

  13. Mamia ya picha na video zatumika katika uchunguzi

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchuguzi wa Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, Jaji Mohamed Chande amesema tume yake imetumia picha mnato 450 na pcha mjongeo 880.

    Mwenye kiti huyo amesema picha hizo zilipatikana na kuwasilishwa na mashuhuda wa matukio, vyombo vya ulinzi na usalama na vyanzo vya wazi ikiwemo vyote vya habari na mitandao na kijamii.

    Ingawa amekiri baadhi ya picha na video hizo zilikuwa ni za kughushi.

  14. Uchunguzi wa Tume ulihusisha mikoa 11

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, Jaji Mohamed Chande, amesema uchunguzi wa tume hiyo ilihusisha maeneo 202, katika wilaya 22 na mikoa 11.

    Akitaja imikoa hiyo amesema ni Dar es Salaam, Mbeya, Songwe, Mwanza, Geita, Arusha, Iringa, Dodoma, Shinyanga, Mara na Ruvuma.

  15. Habari za hivi punde, Jaji Othman Chande aanza kuwasilisha ripoti

    Hafla ya kukabidhi ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Oktoba 29 imeanza rasmi Ikulu jijini Dar es Salaam.

    Mwenyekiti wa Tume, Jaji Othman Chande, ameanza kuwasilisha mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan baada ya miezi kadhaa ya maswali na mjadala kufuatia matukio yaliyohusiana na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

    Tayari viongozi mbalimbali, mabalozi pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wamewasili kufuatilia tukio hilo linalochukuliwa kuwa la kihistoria kwa mustakabali wa taifa.

  16. Hafla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Matukio ya Oktoba 29 yaanza

    Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kupokea Ripoti ya Tume ya Tume ya Uchunguzi wa Oktoba 29 katika Ikulu ya Dar es Salaam.

    Tume hiyo iliundwa kuchunguza matukio hayp baada ya Uchaguzi wa Tanzania wa Oktoba 29, mwaka 2025 kukumbwa na matukio yaliyoweka historia, maandamano, vurugu, vifo na utumiaji wa nguvu kubwa kutoka kwa polisi.

  17. Habari picha: Wageni waanza kuwasili Ikulu Tanzania

    Wageni mbalimbali wameanza kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam Tanzania katika shughuli ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi itakayobidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan hii leo.

    Viongozi wa dini, mabalozi, na viongozi wa kisiasa wamehudhuria.

  18. Mashambulizi ya Marekani na Israel mzizi wa ukosefu wa usalama Ghuba, Hormuz - Iran

    Serikali ya Iran katika mtandao wa X inaeleza kwamba Waziri wa masuala ya kigeni wa taifa hilo amekutana na mjumbe maalum wa Korea Kusini Chung Byung-ha mjini Tehran, ambapo Waziri huyo ameyataka mataifa hayo “kuwa na msimamo thabiti katika kulaani mashambulizi ya Marekani na Israel.”

    Inaripoti Araghchi akisema kwamba Iran imechukua hatua chini ya sheria za kimataifa kulinda usalama na maslahi yake, ikiongeza kuwa washambuliaji wanapaswa kuwajibishwa.

    Jeshi la wanamaji la Iran (IRGC) limedai kushambulia meli tatu katika lango la bahari - zikikamata mbili - baada ya kuapa kulipiza kisasi kufuatia Marekani kuizuia meli ya mizigo yenye bendera ya Iran.

    Unaweza kusoma pia:

  19. Lamine Yamal apata jeraha

    Lamine Yamal amepata majeraha wakati akipiga penalti iliyoipa Barcelona ushindi mwembamba dhidi ya Celta Viga na kuongeza kileleni mwa La Liga kwa pointi tisa.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alifunga penalti dakika ya 40 kwenye Uwanja wa Nou Camp baada ya kuingia ndani ya eneo la hatari na kuangushwa na Yoel Lago.

    Lakini mara tu baada ya kuingiza mpira wavuni kipa Lamine Yamal alikwenda chini huku ameshika paja lake la kushoto.

    Alitoka uwanjani kwa msaada wa madaktari wa timu na kuelekea moja kwa moja kwenye handaki huku nafasi yake ikichukuliwa na Roony Bardghji.

    Ushindi huo unawafikisha mabingwa watetezi wa La Liga, Barcelona - ambao wamebakiwa na michezo sita - kuelekea kutetea ubingwa wao.

    Hansi Flick anatumai jeraha la Lamine Yamal halitamzuia kucheza mechi ya Clasico mwezi ujao dhidi ya Real Madrid iliyo katika nafasi ya pili, huku Uhispania ikiwa na wasiwasi kuhusu utimamu wa mwili wa kijana huyo kwa Kombe la Dunia mwezi Juni.

    Lamine Yamal, ambaye amefunga mabao 16 na kutoa pasi 11 za mabao katika La Liga msimu huu, alitajwa kuwa Mchezaji Bora Kijana Katika Mashindano ya Euro 2024 huku Uhispania ikitwaa kombe hilo.

    Pia unaweza kusoma:

  20. Lebanon yaishutumu Israel kwa kumshambulia mwandishi wa habari na kumuua

    Waziri mkuu wa Lebanon ameishutumu Israeli kwa uhalifu wa kivita baada ya mashambulizi ya anga ya Israeli kumuua mwandishi mmoja wa habari na kumjeruhi mwingine kusini mwa Lebanon siku ya Jumatano.

    Maafisa nchini Lebanon wanasema Amal Khalil na Zeinab Faraj walishambuliwa kimakusudi walipokuwa wakitafuta hifadhi katika nyumba baada ya shambulio la awali la anga kupiga gari lililokuwa mbele yao, na kuwaua wanaume wawili.

    Maafisa hao pia wanalishutumu Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) kwa kushambulia ambulensi kwa makusudi ilipojaribu kuwafikia waandishi wa habari katika kijiji cha Tayri.

    Jeshi la IDF limekana kwamba limezuia timu za uokoaji kufika katika eneo hilo na kusema haliwalengi waandishi wa habari.

    Waandishi wa habari Khalil, 43, ambaye alifanya kazi katika gazeti la Lebanoni la Al-Akhbar, na Faraj, mpiga picha huru, walikuwa wakisafiri pamoja.

    Wanaume wawili waliofariki hawajatajwa majina.

    Mapema mwezi huu, waandishi wa habari wawili waliuawa katika mashambulizi tofauti ya Israel nchini Lebanon.

    Mwezi uliopita, waandishi wa habari watatu wa Lebanon waliuawa katika shambulio la Israel katika mji wa Jezzine, waajiri wao walisema.

    Kwa uchache watu 2,475 wameuawa katika mashambulizi ya Israeli nchini Lebanon tangu vita vya hivi karibuni vianze, na zaidi ya 7,500 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka ya Lebanon. Idadi hiyo inajumuisha wanawake 274 na watoto 177.

    Pia unaweza kusoma: