Moja kwa moja, Iran yatangaza kuweka vizuizi nje ya Mlango wa Hormuz

Akizungumza na televisheni ya taifa ya Iran, Mohsen Rezaei amesema eneo hilo litaanzia kwenye mstari wa kizuizi cha majini uliowekwa na Jeshi la Wanamaji la Marekani na kuenea hadi katika maeneo ya Ghuba.

Muhtasari

  • Kombora la Iran la "kukabiliana na meli za kivita" latumika dhidi ya Marekani kwa mara ya kwanza: Mohsen Rezaei
  • Iran yatangaza kuweka vizuizi nje ya Mlango wa Hormuz
Ruka Video uendelee
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • a
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx
  • Dangote

Moja kwa moja

Na Mariam Mjahid

  1. Bomu la Marekani huenda lilipiga harusi nchini Iran kimakosa - Gazeti la Washington

    s

    Chanzo cha picha, Iranian Red Crescent Society

    Gazeti la Washington Post limeripoti kwa njia ya kipekee siku ya Jumapili kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha shambulio lililosababisha vifo katika harusi katika mji wa Kohstak, kusini mwa Iran, huenda lilitokea baada ya moja ya mabomu sita yaliyoongozwa kwa usahihi, yaliyorushwa na ndege za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani, kupotoka na kukosa shabaha iliyokusudiwa.

    Kwa mujibu wa gazeti hilo, silaha sita za Marekani zililenga jengo la mawasiliano na huduma za simu lililokuwa karibu na eneo la sherehe, lakini moja ya mabomu hayo ilikosa shabaha na kulipiga jengo ambako sherehe ya harusi ilikuwa ikiendelea.

    Washington Post, likimnukuu mtu anayefahamu kwa karibu maelezo ya operesheni hiyo, liliripoti kuwa tathmini ya awali ya jeshi la Marekani ilionyesha kuwa tukio hilo lilisababishwa na "kosa la kombora" na si "kulengwa kwa makusudi kwa jengo ambako sherehe ilikuwa ikiendelea."

    Ripoti hiyo imechapishwa wakati Kamandi Kuu ya Marekani, CENTCOM, ikisema inachunguza taarifa kuhusu vifo vya raia vilivyosababishwa na shambulio hilo. Maafisa wa Marekani wamesema matokeo ya mwisho ya uchunguzi huo bado hayajatolewa.

  2. Kombora la Iran la "kukabiliana na meli za kivita" latumika dhidi ya Marekani kwa mara ya kwanza: Mohsen Rezaei

    j

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mohsen Rezaei, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, amedai kuwa Iran imetumia kwa mara ya kwanza kombora lililotengenezwa nchini humo, linalolenga kukabiliana na meli za kivita za Marekani.

    "Masaa 48 yaliyopita, tulifanyia majaribio kwa mara ya kwanza kombora la Iran la kukabiliana na meli za kivita dhidi ya meli ya Marekani. Kombora hilo liliwasababishia Wamarekani hali ngumu sana na wakakimbia," Mohsen Rezaei alisema katika mahojiano na televisheni.

    Kamandi Kuu ya Marekani, CENTCOM, haikujibu moja kwa moja madai ya Iran. Hata hivyo, katika ujumbe uliowekwa kwenye mtandao wa X jana, ambao unaonekana kurejelea shambulio dhidi ya meli zake mbili, iliandika: "Ujumbe kwa Walinzi wa Mapinduzi uko wazi: mkifyatua mashambulizi dhidi ya meli zetu mbili, tutawawekea gharama kubwa zaidi za kiuchumi na kuharibu meli zenu tatu."

    Taarifa hiyo iliongeza kuwa "hatutasita kuwalinda wanajeshi wa Marekani na, ikibidi, kuharibu meli chache za kubeba mafuta za Iran zilizo katika mazingira hatarishi."

    Aliyekuwa kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran alisema kuhusu madhara yanayoweza kuwakabili wanaosafirisha bidhaa katika eneo hilo: "Meli zitakazokiuka masharti na kufanya shughuli bila kushauriana na Iran zitaongezwa kwenye orodha ya vikwazo ya Iran na zitakabiliwa na madhara mengine, yakiwemo masuala ya bima na ugumu wa kupita katika eneo hilo baadaye."

  3. Iran yatangaza kuweka vizuizi nje ya Mlango wa Hormuz

    s

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mohsen Rezaei, katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, ametangaza kuwa nchi hiyo inapanga kuanzisha eneo la "marufuku ya kuingia" nje ya Mlango wa Hormuz katika siku chache zijazo. Hatua hiyo ni ya hivi karibuni zaidi kuchukuliwa na Tehran wakati mvutano wa kijeshi na kiuchumi kati yake na Marekani ukizidi.

    Akizungumza na televisheni ya taifa ya Iran siku ya Jumapili, Mohsen Rezaei alisema eneo hilo litaanzia kwenye mstari wa kizuizi uliowekwa na Jeshi la Wanamaji la Marekani na kuenea hadi katika maeneo ya Ghuba.

    Aliongeza kuwa "meli yoyote itakayoingia katika eneo hilo jipya itaongezwa kwenye orodha ya vikwazo ya Iran", lakini hakufafanua hatua ambazo Tehran itachukua dhidi ya meli zitakazokiuka vikwazo hivyo.

    Rezaei pia alisema kuwa Mlango wa Hormuz "umefungwa kabisa" na uko chini ya udhibiti wa majeshi ya Iran.

    Hata hivyo, kauli hiyo inakinzana na msimamo wa Marekani, ambao unasema kuwa meli za kubeba mafuta zinaendelea kupita katika njia hiyo muhimu ya majini.

    Zaidi ya mapipa milioni tisa ya mafuta hupita katika Mlango wa Hormuz kila siku, Waziri wa Nishati wa Marekani Chris Wright alisema Jumapili. Aliongeza kuwa usafirishaji wa mafuta kupitia njia mbadala za usambazaji umeongezeka na kufikia takriban theluthi mbili ya viwango vilivyorekodiwa kabla ya mvutano wa sasa kuanza.

    Katika hali ya kawaida, takriban moja ya tano ya mafuta na gesi asilia iliyosafishwa duniani hupita katika Mlango wa Hormuz. Hivyo, usumbufu wowote katika usafirishaji kupitia njia hiyo ya majini unaweza kuwa na athari kubwa kwa masoko ya nishati duniani.

    Kauli ya Mohsen Rezaei inatolewa wakati Marekani imezidisha shinikizo dhidi ya Iran na kukaza vikwazo dhidi ya nchi hiyo, sambamba na kuweka kizuizi cha majini kinacholenga mauzo yake ya mafuta.

    Soma Zaidi Hapa:

  4. Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya tarehe 7/09/2026.