Moja kwa moja , Trump asema mkutano wa kihistoria na Xi na Putin tayari ni “ushindi” hata kabla ya kuanza

Mkutano huo wa kipekee unaowakutanisha viongozi wa mataifa yenye silaha nyingi zaidi za nyuklia duniani huenda usizae makubaliano makubwa, kwa mujibu wa wachambuzi.

Muhtasari

Trump asema mkutano wa kihistoria na Xi na Putin tayari ni "ushindi" hata kabla ya kuanza

Ruka Video uendelee
  • xx
  • Wicknell Chivayo
  • Kijanangoma
  • xx
  • Besigye
  • .
  • xx
  • xx
  • xx
  • Lungu
  • xx
  • xx
  • d
  • s
  • Sonko
  • xx
  • xx
  • xx
  • xx

Moja kwa moja

Na Faidha Ngaga

  1. Xi aahidi 'kushirikiana na pande zote' ndani ya APEC kukuza maendeleo

    .

    Tunaendelea kupata dondoo zaidi kutoka kwa hotuba ya kiongozi wa China, Xi Jinping, aliyoitoa mapema na kufungua kikao cha jumla cha mkutano huo.

    Xi ametoa wito wa maendeleo jumuishi katika kujenga jumuiya ya Asia na Pasifiki, akisema Beijing iko tayari “kushirikiana na pande zote” katika kuendeleza maendeleo na ushirikiano.

    Kwa lengo hilo, China itaanzisha Kituo cha Tafiti za Jumuiya ya Asia na Pasifiki mjini Shenzhen, kwa ajili ya kufanya tafiti za sera na kutoa mchango wa kitaalamu, amesema.

    China pia itaanzisha taasisi za ushirikiano katika maeneo kama teknolojia ya kidijitali, nishati safi na ukuaji wa kijani, miongoni mwa mengine, Xi amesema.

    Kama tulivyoripoti awali, Xi katika hotuba hiyo hiyo alitangaza kuwa China itatumia dola milioni 20 kuendeleza ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo.

    Tutaendelea kukuletea dondoo zaidi kutoka kwenye kikao hicho cha jumla kadri zitakavyopatikana.

    Unaweza pia kusoma:

  2. Trump asema mkutano wa kihistoria na Xi na Putin tayari ni “ushindi” hata kabla ya kuanza

    .

    Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kuwa mkutano wake wa Alhamisi na viongozi wa China na Urusi, Xi Jinping na Vladimir Putin, tayari ni “ushindi” hata kabla ya kufanyika, huku China ikimkaribisha kwa heshima kubwa.

    Mkutano huo wa kipekee unaowakutanisha viongozi wa mataifa yenye silaha nyingi zaidi za nyuklia duniani huenda usizae makubaliano makubwa, kwa mujibu wa wachambuzi. Hata hivyo, umeibua wasiwasi miongoni mwa mataifa madogo yanayohofia kwamba maslahi yao yanaweza kupuuzwa.

    Katika mahojiano na Fox News, Trump alijivunia mapokezi ya kifahari aliyopatiwa alipowasili, ambayo yalitofautiana na yale ya viongozi wengine, akiwemo Putin. Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, aliwasili bila hafla yoyote maalum ya mapokezi.

    Xi alimlaki Trump uwanjani, jambo ambalo limetokea kwa mara ya kwanza kwa kiongozi yeyote wa kigeni tangu awe rais wa China. Hatua hiyo ilikuwa ya kujibu ukarimu wa Trump, ambaye alimkaribisha Xi katika Kituo cha Kijeshi cha Joint Base Andrews mwezi Septemba walipokutana mara ya mwisho. Viongozi hao pia walikumbatiana kwa muda mfupi.

    “Huyu ni rais mkubwa, mmoja wa marais wakubwa wa China, na hajawahi kwenda uwanjani kumpokea mtu,” Trump alisema alipoulizwa anatarajia kupata nini kutoka kwa mkutano huo wa kipekee wa viongozi hao watatu.

    Wakati huo huo, Trump, Xi na Putin wamewasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mabadilishano cha Shenzhen, ambako mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) unafanyika, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China.

    Mkutano huo ulianza kwa kikao cha pamoja cha viongozi, ambapo Trump aliwahutubia washiriki akisisitiza nafasi ya Marekani katika eneo la Pasifiki.

    “Marekani imekuwa nguvu ya Pasifiki kwa mamia ya miaka, na tunaendelea kufanya kazi ili kukuza ukuaji wa uchumi, uthabiti, mamlaka kamili ya nchi, ustawi na amani katika eneo hili lote,” alisema.

    Aliongeza kuwa uhusiano wa Marekani na mataifa ya eneo hilo umekuwa imara kwa muda mrefu.

    Trump pia alisema anafurahia kuripoti kuwa Marekani kwa sasa “inastawi kwa kiwango ambacho haijawahi kushuhudiwa hapo awali.”

    “Kimekuwa kipindi cha ajabu sana kuona yaliyotokea,” alisema.

    Mkutano huo wa viongozi watatu unaendelea kufuatiliwa kwa karibu duniani kote, huku wengi wakisubiri kuona iwapo utaweka msingi wa ushirikiano mpya kati ya Marekani, China na Urusi au kubaki kuwa ishara ya nguvu za kidiplomasia za mataifa hayo makubwa.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Hujambo! na karibu kwenye matangazo yetu Mubashara, leo Alhamisi 19/11/2026