Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza
kuwa Marekani imefikia makubaliano na Venezuela ya kudhibiti zaidi ya
mapipa bilioni 65 ya mafuta nchini humo.
“Makubaliano haya ya kihistoria yatazidisha
zaidi ya mara mbili akiba ya mafuta ya Marekani,
utaongeza kwa kiasi kikubwa
usambazaji wetu wa mafuta na kupunguza
bei ya petroli kwa Wamarekani wote,” Trump aliandika kwenye mitandao ya
kijamii.
Rais
wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, amepongeza makubaliano hayo, akisema
yatasaidia kufufua uchumi wa taifa lake.
Trump
alikuwa ameahidi kutumia akiba ya mafuta ya
Venezuela, ambayo ni kubwa zaidi duniani, baada ya Marekani kumkamata rais wa taifa hilo Nicolás Maduro, mapema mwaka huu.
Hivi
karibuni, Trump amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kupunguza bei za mafuta
nchini Marekani, ambazo zimepanda
kutokana na mzozo wa Iran.
Waziri
wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, alitaja
makubaliano hayo ya mafuta kuwa “ushindi mkubwa kwa wananchi wa Marekani na Venezuela.”
Hata hivyo, maelezo machache kuhusu makubaliano hayo yametolewa.
“Kwa
wananchi wa Venezuela, makubaliano haya yataleta karibu dola bilioni 100 za
uwekezaji kutoka sekta binafsi, na
kutengeneza ajira zenye mishahara
mizuri na kuimarisha uchumi wa
Venezuela,” Rubio alichapisha
kwenye mitandao ya kijamii.
Maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo hayajatolewa.
Trump alidai kuwa makubaliano hayo yalifikiwa “bila gharama yoyote kwa walipa
kodi wa Marekani.”