Niger: Uwanja mkuu wa ndege walengwa huku milio ya risasi ikiripotiwa mjini Niamey

Chanzo cha picha, Getty Images
Milio ya risasi na milipuko imeripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Niger, Niamey, karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa, na kambi ya kijeshi iliyo karibu na ikulu ya rais.
Chanzo kimoja kimeiambia shirika la habari la Reuters kwamba washambuliaji walilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani na kujaribu kuvuka ukuta unaozunguka ikulu ya rais.
Inasemekana vikosi vya usalama vimefanikiwa kurejesha udhibiti wa Kambi ya Anga ya 101, iliyoko karibu na uwanja wa ndege, ingawa taarifa hiyo haijathibitishwa.
Serikali ya Niger bado haijatoa taarifa yoyote kuhusu tukio hilo, na hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo. Bado haijulikani ni nani waliofanya shambulio hilo au iwapo kuna watu waliojeruhiwa au kuuawa.
Uwanja huo wa ndege na maeneo ya kijeshi yaliyo karibu, tayari yamelengwa mara mbili mwaka huu na makundi yenye itikadi kali.
Wanamgambo wa Islamic State walishambulia eneo hilo mwezi Januari, huku kundi la JNIM lenye uhusiano na al-Qaeda likifanya shambulio jingine mwezi Juni.
Jeshi lilichukua mamlaka nchini Niger mwaka 2023, na kuipundua serikali ya kiraia iliyokuwepo, likiahidi kukabiliana na uasi ambao ulikuwa umeongezeka nchini humo.
Mamlaka za kijeshi nchini Niger zimewataka wananchi katika mji mkuu, Niamey, kuwa watulivu baada ya milio mikubwa ya risasi na milipuko kuripotiwa katika maeneo kadhaa ya mji huo.
Soma pia:



