Moja kwa moja , Marekani yaidhinisha uuzaji wa makombora ya Patriot kwa Ukraine

Marekani imeidhinisha uuzaji wa makombora 500 aina ya Patriot kwa Ukraine, ambazo ni silaha muhimu za kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi.

Muhtasari

  • Rais Ruto na Putin wakubaliana kusitisha uajiri wa Wakenya katika jeshi la Urusi
  • Qatar yaendeleza juhudi ya kuwa mpatanishi kati ya Marekani na Iran
  • Maandamano mapya yatarajiwa Ufaransa, serikali ikiahidi kudumisha usalama
  • Marekani yaidhinisha uuzaji wa makombora ya Patriot kwa Ukraine

Moja kwa moja

Na Beldeen Waliaula

  1. Tetesi za Soka: Man United yammezea mate Fermin Lopez wa Barcelona

    .
    Maelezo ya picha, Mchezaji wa Barcelona, Fermin Lopez

    Manchester United inamuwinda kiungo wa Barcelona Fermin Lopez, mwenye umri wa miaka 23, raia wa Hispania, huku klabu hiyo ikilenga kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha la usajili la Januari

    Beki wa Manchester United, Lisandro Martinez, anatarajiwa kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, huku Barcelona na Atletico Madrid zikionyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28.

    Wakati huo huo, Arsenal inammezea mate mshambuliaji wa Club Brugge, Nicolo Tresoldi.

    Klabu kadhaa za Ligi Kuu England zinamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Minnesota United, Kelvin Yeboah, mwenye umri wa miaka 26 huku Everton ikiwa inaongoza katika mbio za kumsajili raia huyo wa Ghana.

    Nayo Manchester United inazidi kuonyesha nia ya kumsajili beki wa Fulham, Calvin Bassey, raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 26.

    Winga wa Nottingham Forest, Omari Hutchinson, raia wa England mwenye umri wa miaka 23, anayeichezea AC Milan kwa mkopo, anatarajiwa kurejea katika klabu yake msimu ujao wa majira ya kiangazi. AC Milan imeanza kuelekeza nguvu zake katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Endrick, raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 20.

  2. Rais Ruto na Putin wakubaliana kusitisha uajiri wa Wakenya katika jeshi la Urusi

    .
    Maelezo ya picha, Picha ya Vladimir Putin na William Ruto

    Kenya na Urusi zimekubaliana kusitisha uajiri wa raia wa Kenya kujiunga na jeshi la Urusi, kufuatia mazungumzo kati ya Rais William Ruto na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow.

    Makubaliano hayo yaliyofikiwa baada ya wawili hao kufanya mkutano katika Ikulu ya Kremlin, yataifanya Kenya kutambuliwa kama nchi isiyoruhusiwa kuajiriwa raia wake kujiunga na jeshi la Urusi.

    Hatua hiyo inalenga kufunga njia zilizokuwa zikitumika kuwaandikisha Wakenya kupigana katika vita kati ya Urusi na Ukraine.

    Makubaliano hayo yameafikiwa huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kuajiriwa kwa mamia ya Wakenya katika jeshi la Urusi.

    Rais William Ruto amesema Rais wa Urusi Vladimir Putin amethibitisha kujitolea kwa nchi yake kusitisha uajiri wa Wakenya kujiunga na jeshi la Urusi.

    "Nilimshukuru Rais Putin kwa kuthibitisha kuwa Wakenya hawataendelea kuandikishwa katika jeshi la Urusi, kwa kuwa Kenya imeainishwa kama nchi isiyoruhusiwa kuwa chanzo cha uajiri wa wanajeshi," alisema Rais Ruto.

    Aidha, Ruto ametangaza kuteuliwa kwa afisa wa jeshi anayeshughulikia masuala ya ulinzi katika Ubalozi wa Kenya mjini Moscow, ili kuratibu kurejea nchini kwa Wakenya walioenda Urusi kupigana vita.

    Afisa huyo atashirikiana na Wizara ya Ulinzi ya Urusi kuratibu taratibu za kuwarejesha Wakenya hao, kushughulikia fidia zao na kuhakikisha wanarejea nchini salama.

    Soma pia:

  3. Qatar yaendeleza juhudi ya kuwa mpatanishi kati ya Marekani na Iran

    .

    Mazungumzo ya kuwapatanisha Marekani na Iran yanaoongozwa na Qatar, yanaendelea hii leo mjini Doha.

    Hapo jana, ujumbe wa Qatar ulifanya mazungumzo ya muda mrefu na maafisa wa Iran mjini Tehran.

    Shirika la habari la Axios limeripoti kuwa, ikinukuu chanzo kimoja cha kidiplomasia, kuwa wapatanishi wa Qatar walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara na Ikulu ya Marekani wakati wa mkutano huo uliochukua saa 12 hapo jana.

    Chanzo hicho kilisema: "Maendeleo chanya yamepatikana na majadiliano yanaendelea ili kuwezesha kuafikiwa kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran."

    Juhudi hizi mpya za kidiplomasia zinafuatia barua kutoka kwa Makamu wa Rais wa Marekani, J.D. Vance, kwenda kwa Mohsen Rezaei, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, akitoa wito wa kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

    Mazungumzo hayo yanafanyika wakati baadhi ya wachambuzi wakionya kuwa iwapo Warepublican watapata kipigo kikubwa katika uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani, Rais Donald Trump anaweza kuagiza operesheni kubwa ya kijeshi dhidi ya Iran.

    Soma pia:

  4. Maandamano mapya yatarajiwa Ufaransa, serikali ikiahidi kudumisha usalama

    .

    Ufaransa imesema iko tayari kuwatuma polisi 70,000 kudumisha usalama, huku maandamano mengine yakitarajiwa kufanyika hii leo.

    Maandamano hayo yamechochewa na hasira za wananchi wanaolalamikia kupanda kwa gharama ya Maisha na huduma duni za serikali za utawala wa Rais Emmanuel Macron.

    Maandamano hayo ya kitaifa, yanayotarajiwa kufanyika hii leo, usiku wa sherehe za Halloween, yanakuja wiki mbili baada ya ghasia na uporaji wa mali kuwashtukizia vikosi vya usalama, na kusababisha uharibifu wa maduka, majengo ya umma na biashara katika miji mbalimbali nchini Ufaransa.

    Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nunez ameahidi kutoruhusu hali kama hiyo kujirudia.

    "Kila mtu yuko tayari kuhakikisha tunachukua hatua kali dhidi ya jaribio lolote la kuvuruga amani," Nunez alisema katika mkutano na waandishi wa habari mapema wiki hii.

    Soma pia:

  5. Marekani yaidhinisha uuzaji wa makombora ya Patriot kwa Ukraine

    .

    Marekani imeidhinisha uuzaji wa makombora 500 aina ya Patriot kwa Ukraine, ambazo ni silaha muhimu za kujilinda dhidi ya mashambulizi ya anga ya Urusi.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ameonya kuwa huenda ikachukua "miaka kadhaa" kabla ya makombora hayo kufika nchini humo.

    Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imesema makombora hayo ya kisasa ya kuzuia mashambulizi ya angani, aina ya PAC-3, yana thamani ya dola bilioni 2.1 na kwamba gharama yake italipwa kikamilifu na washirika wa Ukraine barani Ulaya na Canada.

    Zelensky amerudia wito wake kwa Marekani kuharakisha kutoa mifumo yake ya makombora ya Patriot, ambayo ndiyo silaha pekee yenye uwezo wa kuzuia makombora hatari ya Urusi aina ya ballistic.

    Hatua hii ya hivi karibuni imekuja kufuatia mvutano kati ya Zelensky na Rais wa Marekani Donald Trump mapema mwezi huu, baada ya Marekani kulegeza vikwazo dhidi ya Urusi kama sehemu ya makubaliano ya kupata mafuta ya dizeli kutoka Urusi.

    Trump aidha alisema ni wakati mwafaka kwa Ukraine kupata kiongozi mpya ambaye anaweza kufanikisha makubaliano ya kumaliza vita na Urusi.

    Urusi ilianzisha uvamizi mkubwa nchini Ukraine mwezi Februari mwaka 2022, baada ya awali kuteka eneo la Crimea na baadhi ya maeneo ya Donbas mashariki mwa Ukraine.

    Soma pia:

  6. Hujambo na karibu kwenye matangazo yetu ya moja kwa moja Jumamosi ya leo