Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Marekani yaishambulia Iran kwa usiku wa saba mfululizo

Jeshi la Marekani limesema linazidisha mashambulizi ili kudhoofisha vikosi vya kijeshi vya Iran, huku Iran ikiripoti milipuko karibu na Mlango Bahari wa Hormuz.

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Mwanaharakati wa India aliyegoma kula kwa siku 20 apelekwa hospitalini kwa nguvu

    Mwanaharakati na msomi wa India Sonam Wangchuk, ambaye alikuwa kwenye mgomo wa kula kwa siku 20 zilizopita huko Delhi, ameondolewa kwa nguvu kutoka eneo lake la maandamano.

    Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 59 alikuwa akiandamana kuunga mkono harakati za kejeli mtandaoni zinazoitwa Cockroach Janta Party (CJP) zinazotaka mageuzi ya kielimu. Waandamanaji walikuwa wamepanga maandamano hadi bunge la India siku ya Jumatatu.

    Wangchuk alikuwa amegoma kula chakula wakati wa kiangazi chenye joto kali, huku akila chumvi na maji tu. Alikuwa amepunguza uzito zaidi ya kilo 9 na alikuwa na maumivu makali.

    Mwanzilishi wa CJP Abhijeet Dipke sasa ameanza mfungo usiojulikana badala yake. Anasema maandamano ya kuelekea bungeni yataendelea na amemtaka Waziri Mkuu Narendra Modi ajiuzulu.

    Dipke aliambia BBC kwamba alikuwa ameenda nyumbani kwa rafiki yake asubuhi ili kupumzika wakati polisi walipofika na kukataa kumruhusu aondoke.

    Video kutoka kwenye tovuti ya maandamano siku ya Jumamosi zilionyesha machafuko yakizuka kabla tu ya saa 1:30 kwa saa za huko (02:00 GMT) wakati polisi kadhaa na wanajeshi walipoingia ghafla kwenye jukwaa ambalo mwanaharakati huyo alikuwa amelala. Waandamanaji waliojaribu kuwazuia walisukumwa mbali.

    Walimfunika kwa mapazia ya shuka kabla ya kumtoa jukwaani. Dakika chache baadaye, ambulensi ilionekana ikiondoka kwa kasi.

    Mke wa mwanaharakati huyo Gitanjali Angmo baadaye alichapisha kwenye mtandao wa X kwamba alikuwa "katika hospitali ya Safdarjung ambapo amelazwa".

    Soma Zaidi:

  2. Marekani yaishambulia Iran kwa usiku wa saba mfululizo

    Jeshi la Marekani limesema limefanya mashambulizi kwa usiku wa saba mfululizo dhidi ya Iran tangu Rais Donald Trump atangaze makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda "yamefutiliwa mbali".

    Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa X, Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) iliandika kwamba vikosi vyake "vimeshambulia maeneo ya uchunguzi, miundombinu ya vifaa vya kijeshi, maghala ya silaha yaliyopo chini ya ardhi, na uwezo wa kijeshi wa majini".

    Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) lilisema meli mbili za mafuta zililipuka katika Mlango-Bahari wa Hormuz wakati zikipita kwenye sehemu ya njia ya meli iliyokuwa na mabomu ya ardhini. Taarifa hiyo ilipuuzwa na Hata hivyo, Centcom ilisema kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

    Vikosi vya kijeshi vya Jordan vilisema vilidungua makombora 10 ya Iran yaliyorushwa kwenye anga yake usiku huo, ingawa hakukuwa na majeruhi wala uharibifu wowote.

    Centcom ilisema kuwa ilimaliza mashambulizi yake saa 21:30 kwa saa za Marekani Mashariki (02:30 BST) baada ya kufanya mashambulizi hayo kwa muda wa saa kadhaa.

    Katika taarifa yake, Centcom ilisema: "Vikosi vya Marekani vilitumia ndege za kivita, ndege zisizo na rubani, na meli za kivita pamoja na vifaa vingine katika operesheni hiyo."

    Shirika la habari la serikali ya Iran, Fars, lilisema meli mbili za mafuta "zililipuka na kushika moto wakati zikipita kwenye njia iliyokuwa na mabomu ya ardhini kusini mwa Mlango wa Hormuz". Baadaye, Centcom iliandika kwenye X: "Kama madai mengi ya IRGC, hii si kweli."

    Usafirishaji wa meli katika Mlango muhimu wa Hormuz umesitishwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuendelea kwa mashambulizi ya kulipizana kisasi kati ya vikosi vya Marekani na Iran.

    Soma Zaidi:

  3. Hujambo. Karibu katika matangazo yetu mubashara tarehe ni 18/07/2026.