'Sikujua hata DR Congo iko wapi': Marekani yawapeleka wahamiaji katika nchi wasiyoijua

Carlos Alberto Rodelo, in blue T-shirt and shorts, stands next to Jorge Cubillos, in white vest and black trousers, with hands in pockets, on the balcony of their small hotel room in Kinshasa, with palm trees in the background.

Chanzo cha picha, Courtesy image

Maelezo ya picha, Carlos Rodelo (kushoto) na Jorge Cubillos ni miongoni mwa kundi la wahamiaji 15 na wanaotafuta hifadhi kutoka Colombia, Peru na Ecuador walioko katika hoteli huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mji wa Kinshasa.
    • Author, Norberto Paredes
    • Nafasi, BBC News Mundo
  • Muda wa kusoma: Dakika 6

"Nilipofika ofisini, mara tu nilipoingia ndani, niliwaona maafisa watatu wa Ice [Uhamiaji na Ushuru wa Marekani] wakiwa wamejificha, wakinisubiri."

"Waliniambia watanishikilia na huenda nikafukuzwa nchini."

"Waliponiambia wananipeleka Congo, niliwaambia hata sijui Congo ni nini au ni wapi."

"Niliwaambia nimepata hifadhi ya ukimbizi na ulinzi kutokana na Mkataba Dhidi ya Mateso (CAT).

"Waliniambia vyovyote iwavyo wataniondoa tu Marekani."

Carlos Rodelo alikuwa Marekani kwa miaka mitatu na nusu na tarehe 4 Februari 2025, jaji wa Maryland alipompa ulinzi chini ya Mkataba Dhidi ya Mateso (CAT).

Anasema jaji aliamua kuwa anaweza kubaki nchini na hatofukuzwa, ingawa hatopaswa kuondoka katika eneo la Marekani.

Makubaliano yenye utata

Seated in the White House’s Oval Office, Donald Trump holds a letter of congratulations. Standing around the US president are Rwanda Minister of Foreign Affairs and Cooperation Olivier Nduhungirehe, US Vice-President JD Vance and Secretary of State Marco Rubio, all in dark blue suits, white shirts and red or, in the case of Nduhungirehe, blue, ties, and Democratic Republic of the Congo Foreign Minister Thérèse Kayikwamba Wagner, in a blue patterned shirt and skirt.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utawala wa Donald Trump, nchini Marekani, tayari umewapeleka wahamiaji katika nchi nyingine za Afrika, ikiwa ni pamoja na Ghana, Sudan Kusini na Eswatini.

Miezi kadhaa baadaye, Carlos aliarifiwa kwamba anatakiwa kufika katika ofisi ya uhamiaji, ili kusaini hati kadhaa. Haikuwa mara ya kwanza kuitwa, kwa hivyo hakuwa na shaka. Lakini alitumia miezi minane iliyofuata kizuizini huko Louisiana.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wakati huo, anasema, aliwasilisha maombi ya ziada ya kuomba ulinzi. Lakini alifukuzwa kabla ya jaji wa shirikisho kutoa uamuzi. Alijua anakopelekwa saa chache tu kabla ya safari ya ndege kuanza. Na hakuwa peke yake.

Carlos ni mmoja wa wahamiaji 15 na wanaotafuta hifadhi kutoka Colombia, Peru na Ecuador ambao Marekani imewafukuza na kuwapeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ni wa kwanza kuwasili katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati mwezi huu chini ya makubaliano yenye utata na nchi za tatu, yaliyosainiwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

DR Congo imetetea makubaliano yake ya kuwapokea wahamiaji kutoka nchi nyingine, kama njia ya kuheshimu utu wa binadamu, ulinzi wa haki za wahamiaji na mshikamano wa kimataifa. Kukaa kwao nchini kutakuwa kwa muda, huku Marekani ikifadhili kukaa kwao.

Lakini wahamiaji na wanaotafuta hifadhi wameiambia BBC News Mundo kwamba wako katika hali ya sintofahamu ambayo hawajui jinsi ya kuikwepa na afya zao zinazidi kuzorota. Wamezuiliwa katika hoteli moja katika mji mkuu wa Kinsasha na wanaripoti kukatika kwa umeme na ukosefu wa maji ya kunywa.

"Tuna homa, kutapika na kuhara. Wanatuambia ni kawaida na miili yetu ndio inazoea Afrika," anasema Jorge Cubillos.

Kwa miaka minane, Jorge alifanya kazi ya kujenga maisha mapya nchini Marekani, baada ya kukimbia vitisho nchini Colombia.

Anasema alikuwa na kibali cha kufanya kazi, mchakato wa kupata hifadhi unaendelea na matarajio ya kukaa nchini humo.

Lakini ghafla Jorge alifukuzwa mbali na mkewe na watoto wake wanne, kutoka jimbo la Florida.

Safari ya Congo

Surrounded by high-rise buildings, Kinshasa's Boulevard du 30 Juin is busy with traffic.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata safari ya kwenda Kinsasha haikuwa ya kibinadamu, kundi hilo linasema

Kutoka chumba chake kidogo cha hoteli, anaiambia BBC News Mundo: "Sikuwahi kufikiria nitaishia Afrika. Nilidhani vilikuwa vitisho tu."

Hata safari ya kwenda Kinsasha haikuwa ya "kibinadamu," kundi hilo linasema.

"Lilikuwa jambo la kustaajabisha kwa sababu tulitumia zaidi ya saa 25 tukiwa tumefungwa kiunoni, mikononi, na miguuni, na mfuko uliokuwa na tufaha, chipsi na chupa ya maji ndani," Jorge anasema. "Hali ikuwa mbaya."

Baada ya vita vya kisheria ambapo alitumia miezi 14 kizuizini nchini Marekani, Marta, ambaye aliomba jina lake libadilishwe, anasema aliachiliwa chini ya usimamizi tarehe 13 Februari 2026. Alikuwa na kibali cha kufanya kazi na alikuwa akifuatilia mchakato wa uhamiaji "kwa njia sahihi."

Chini ya miezi miwili baadaye, maafisa wa Ice waligonga mlango wa nyumba yake huko Texas, wakamwonyesha nakala ya agizo - kupitia kioo - na kumwambia wako pale ili kuthibitisha anwani yake.

"Sikuona tatizo lolote na nilifungua mlango," Marta anasema.

Dakika chache baadaye, maafisa walimwomba aandamane nao hadi ofisini, ili kumwekea kifaa cha kufuatilia GPS. Hakutilia shaka - hadi walipomfunga pingu.

Marta alipelekwa katika Kituo cha Magereza cha Bluebonnet, huko Anson, Texas, na baada ya siku tatu alihamishiwa katika Kituo cha Magereza cha Prairieland, huko Alvarado, ambapo alizuiliwa peke yake kwa karibu siku mbili.

"Walinifungia chumbani. Hawakunipa chakula wala maji. Kulikuwa na baridi kali," anasema.

Familia yake haikuweza kumpata. Na baada ya kuchanjwa dhidi ya homa ya manjano na kuhamishiwa Louisiana, aliambiwa anapelekwa DR Congo siku iliyofuata.

Sheria zinasemaje?

Two US Immigration and Customs Enforcement agents, one with a shaved head and wearing bullet-proof vests labelled "POLICE ICE", stand on a descending escalator.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wawili wa Uhamiaji na Forodha nchini Marekani

"Kwa hivyo niko hapa, Congo," Marta anasema. "Nahisi haki zetu za binadamu zimekiukwa."

"Kuna taarifa nyingi potofu kwenye mitandao ya kijamii. Wanasema sisi ni wahalifu na tunastahili kinachotupata."

BBC News Mundo imewasiliana na Ice kwa ajili ya kutoa maoni.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Haki za Binadamu (IRDH) na wakili wa haki za binadamu Hubert Tshiswaka anasema makubaliano kati ya DR Congo na Marekani yanavunja ahadi za kimataifa kuhusu ulinzi wa wakimbizi.

"Hakuna msingi wa kisheria wa kuwapeleka watu kutoka nchi zingine hadi Congo, hasa kutoka Marekani," ameiambia BBC News Mundo. "Zaidi ya hayo, watu hawa hawajafanya kosa lolote, kwa hivyo pia hakuna msingi wa kisheria wa kuwaweka kizuizini."

Mwanamke mwingine wa Colombia ambaye aliomba kutotajwa jina anasema alifukuzwa baada ya kukaa wiki kadhaa katika Kituo cha Magereza cha Eloy, huko Arizona.

"Waliniita ofisini, wakisema wanataka kuondoa GPS yangu. Na nilipofika, waliniambia watanizuia kwa sababu wamenitafutia nchi ya tatu," anasema.

Sasa, hana uhakika kama anataka kurudi Marekani, maisha "yanatisha" na serikali inafanya mambo yasiyo ya kibinadamu.

"Yote yaliyotokea na yote niliyopitia, nani anayeweza kunihakikishia kwamba sitapitia haya tena na katika siku zijazo hawatanipeleka nchi nyingine?" anasema.

"Kinachofanywa na rais si cha kibinadamu — si yeye tu bali pia watu wanaofuata armi zake."

"Naamini katika serikali hii, wao ni vibaraka tu wanaotumiwa na mtu na rais, wakiwaweka watu kizuizini bila ya sababu."

"Kutumia muda mwingi kizuizini bila kutenda uhalifu wowote inaumiza sana. Na hali ndani ya vituo vya kizuizini si nzuri zaidi."

"Kama ningelazimika kuchagua kati ya Congo na Barranquilla, Colombia — mahali ninapotoka — ningechagua Barranquilla, kwa sababu hapa sifanyi chochote," anasema.

"Lakini kurudi Barranquilla kutayaingiza maisha yangu hatarini."