Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya: Arsenal, Man Utd zamgombania Fernandes
Manchester United inamatumaini ya kumsajili kiungo wa Ureno na West Ham, Mateus Fernandes, mwenye miaka 21, baada ya kuizidi Arsenal katika mbio za kuwania saini yake. (Times)
Newcastle United imefufua tena nia yake ya kumsajili kipa wa Manchester City na England, James Trafford, mwenye miaka 23, huku klabu hiyo ikiendelea kuimarisha kikosi chake cha makipa. (Athletic)
Arsenal inafikiria kumsajili winga wa Real Sociedad na Hispania, Ander Barrenetxea, ambaye pia anafuatiliwa kwa karibu na klabu ya Tottenham Hotspur. (Sun)
Leeds United na Liverpool zote zinaonyesha nia ya kumsajili beki wa kati wa Midtjylland na Korea Kusini, Lee Han-beom, mwenye miaka 23. Napoli, Monaco na Lyon pia zinamfuatilia mchezaji huyo. (Teamtalk)
Brighton & Hove Albion imewasilisha ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya kumsajili beki wa Croatia, Luka Vuskovic, mwenye miaka 19, kutoka Tottenham Hotspur. (Athletic)
Real Madrid inatarajiwa kukamilisha usajili wa kiungo Mreno, Bernardo Silva, mwenye umri wa miaka 31, chini kocha anayerejea, Jose Mourinho klabuni hapo. Silva anatarajiwa kuondoka Manchester City mwishoni mwa mwezi huu baada ya mkataba wake kumalizika. (Mail)
Bayern Munich inaamini inaweza kufanikisha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Marcus Rashford, mwenye miaka 28, baada ya mazungumzo mazuri na wawakilishi wake. (Teamtalk)
Besiktas ipo katika mazungumzo ya hatua za mwisho na mshambuliaji wa Arsenal, Leandro Trossard, mwenye miaka 31, kuhusu uhamisho wenye thamani ya pauni milioni 20. (Caught Offside)
Galatasaray inamuwania kiungo mshambuliaji wa Aston Villa, Emiliano Buendia, mwenye miaka 29, huku Aston Villa ikitazama uwezekano wa kumchukua Crysencio Summerville wa West Ham, mwenye miaka 24, kama mbadala wake. (Football Insider)
Barcelona inapanga kumuondoa kipa wake Marc-Andre ter Stegen, mwenye miaka 34, ambaye anaonekana hayuko sasa katika mipango ya klabu, na itamuuza kwenda Ajax. (Fichajes)