Vita vya Iran vimeimarisha Ukraine kimkakati, Je kuna uwezekano wa uwepo wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Urusi na Ukraine hivi karibuni?

A composite image including Zelensky and Ukrainian drones
Je, vita vya Iran vinaipa Ukraine mkakati wa kumaliza mzozo na Urusi?
Muda wa kusoma: Dakika 5

Wakati rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipowasili nchini Saudi Arabia mwezi Machi, safari hiyo iliacha alama kubwa katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Kupitia mtandao wa X, rais huyo alisema ziara yake ilikuwa ya "kuimarisha ulinzi wa maisha ya watu."

Zelensky ambaye taifa lake limekuwa likipigana na Urusi kwa muda mrefu, ametumia fursa aliyonayo kueneza ujuzi walioupata wa kupigana, katika mataifa ya Ghuba haswa ikija katika matumizi ya ndege zisizo na rubani.

Ukraine imetangaza kuwa imeafikia mkataba na Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Qatar, ambao wote walishambuliwa na makombora ya Iran, kuwapa teknolojia ya ndege zisizo na rubani na vifaa vingine vya ulinzi wakitumai kunufaika na uhusiano wa kibiashara pia.

"Tunataka kusaidia mataifa ya ghuba yajilinde yenyewe, na tutaendelea kujenga uhusiano kama huu na mataiafa mengine," alisema Zelensky.

Shinikizo la nishati

Vita nchini Iran vilionekana kuiathiri Ukraine. Ilitishia kuondoa uangalifu wa Trump kutoka Ukraine na kuelekeza umakini wake Iran, na kupuuzia mazungumzo ya amani yaliyokuwa yakiendelea kati ya Kyiv na Moscow.

Urusi imeweza kuuza mafuta mengi kwa mataifa tofauti kwa bei ya juu, baada ya meli za kubeba mafuta kuzuiwa katika mlango bahari wa Hormuz. Trump aliowaondolea vikwazo vya mafuta, na kuruhusu mataifa mengine kununua mafuta ya Urusi baada ya bei ya mafuta kupanda maradufu.

Wasiwasi ni kuwa iwapo Urusi itaendelea kupata fedha nyingi, itakuwa vigumu kumaliza vita vinavyoendelea Ukraine.

Picha ya Zelesky akiwa Saudi Arabia

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha ya Zelesky akiwa Saudi Arabia
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Awali Trump alisema kuwa anaimani suluhu kuhusu vita vya Ukraine inaweza kuafikiwa haraka ikiwa kutakuwa na mazungumzo mazuri na rais wa taifa hilo Vladimir Putin.

"Nadhani kuna watu wanaofanya inakuwa vigumu kwa yeye kuafikia makubaliano" Alisema Trump

Si mara ya kwanza kwa Trump kusema hivyo kuhusu Putin huku akimshambulia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kukataa kutia Saini mkataba wa kusitisha vita.

Ila kwa sasa Zelensky anamewekeza katika kupata nafasi zitakazoinufaisha Ukraine.

Alizuru tena Saudi Arabia mwezi Aprili, ambapo alikumbana na makombora yaliyokuwa yakirushwa na Iran, ambayo Urusi pia hushambulia Ukraine nazo.

Moja ya makombora yanayotumiwa sana na Urusi kuishambulia Ukraine, ni makombora ya bei rahisi ya Iran yanayoitwa Shahed 136, na pia makombora yake ya Geran.

Wakati kombora moja la Shahed linagharimu shillingi dola 80,000 hadi 130,000, Zelensky anasema yanaweza kudunguliwa na mifumo inayogharimu dola 10,000, ambayo ni bei nafuu zaidi ikilinganishwa na mifumo ya ulinzi ya angani inayotumiwa kwa sasa inayogharimu mamilioni ya dola.

Picha ya mwanamke akisimama katika vifusi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha ya mwanamke akisimama katika vifusi

Ukraine pia imetia saini mkataba wa ushirikiano wa ulinzi na mataifa mawili ya Ulaya mwezi Aprili. Moja ilikuwa na Norway iliyogharimu dola billioni 8.6 inayojumuisha kifurushi cha dola billioni 28 hadi mwaka wa 2030. Nyingine ilikuwa na Ujerumani ambayo ilihusisha ndege zisizo na rubani za aina tofauti, makombora na mifumo ya kisasa ya ulinzi kwa gharama ya dola billioni 4.7.

Kwa mataifa ya ghuba, Zelensky alisema anatumai atapata msaada kwao wa kuisaidia Ukraine kujilinda dhidi ya Urusi.Hii ni baada ya nguvu nyingi za Marekani kuelekezwa Mashariki ya Kati

Kulenga miundo mbinu

Ukraine pia imejifunza mbinu za vita vya Iran. Kuongeza shinikizo katika vita ni kulenga vituo vya kuzalisha mafuta, na sasa wanalenga vituo vya Urusi kwa kutumia makombora ya masafa marefu yaliyotengenezwa nchini Ukraine.

Kulingana na Zelensky, tayari sekta ya mafuta Urusi imeathirika pakubwa hata kabla ya kupanda kwa bei ya mafuta.

Takwimu zinaonyesha kuwa kupanda kwa bei ya mafuta na kuondolewa kwa vikwazo kwa mafuta ya Urusi, imesaidia taifa hilo kuimarisha mapato yake zaidi ya marambili zaidi ya mapato ya kawaida katika wiki ya tatu ya vita nchini Iran.

Ila katika wiki ya nne ya vita vya Iran, Ukraine ililenga kituo cha kuzalisha mafuta cha Urusi chenye gharama ya zaidi ya dola billioni moja na kuharibu hatua ambazo walikuwa wamepiga

Vladimir Putin na Donald Trump wakisalimiana

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vladimir Putin na Donald Trump wakisalimiana

Hatua nyingine Ukraine imepiga baada ya vita vya Iran, ni kupewa mkopo wa dola billioni 78 na Umoja wa Ulaya, baada ya Kyiv kusema kuwa walihitaji fedha hizo kwa haraka kununua silaha za kijeshi.

Mkopo huo ulikuwa umezuiliwa kwa muda mrefu na taifa mwanachama wa Umoja wa Ulaya, Hungary, ambaye waziri wake mkuu wa awali alikuwa mshirika wa karibu wa Urusi.

Kukosa heshima

Baada ya kurejea madarakani, Trump alisema anaweza kumaliza vita hivyo chini ya saa 24, ila hajaweza kutimiza hilo hadi sasa.

Ujumbe wa Marekani haukifika mjini Kyiv wakati wa mazungumzo, badala yake wamejihusisha sana na vita vinavyoendelea mashariki ya kati, huku Zelensky akitaja kukosa kufika kwao kama "kukosa heshima."

Zelensky anasema mazungumzo hayo yamefikia hatua ya kuzungumzia masuala tata, ila anahofia hakuna hatua itapigwa hadi wakati vita vinavyoendelea nchini Iran vimalizike.

Wajumbe wa Marekani walioteuliwa kuhusika na mazungumzo ya kupatikana kwa amani Ukraine, Jared Kushner shemeji yake Trump na Steve Witkoff, hawajawahi kufika mjini Kyiv kwa ziara rasmi.Wawili hao walizuru Urusi mwaka uliopita na pia mwezi Januari kufanya mazungumzo ya kusitisha vita hivyo.

Utawala wa Trump umekanusha kuwa na mapendeleo na Urusi.

.

Chanzo cha picha, Reuters

Kupatikana kwa amani

Ikija katika kuishawishi Urusi kushiriki katika mazungumzo ya amani, Marekani pekee ndiyo inauwezo wa kufanya hivyo.

Putin hajaonyesha nia ya kumaliza vita hivyo hivi karibuni.

Kwa sasa dunia imeangazia sana vita nchini Iran, huku Urusi ikiendeleza mashambulizi yake nchini Ukraine na kuharibu miundo mbinu.

Ingawa uchumi wa Urusi umeathirika pakubwa kutokana na vikwazo walivyowekea, kuna hofu kuwa Putin anaweza kulenga taifa lingine na jumuiya ya kujihami ya Nato, Uholanzi na Ujerumani wakiwa walengwa wakuu.

Aidha kiburi cha Putin, hakiwezi kumruhusu kukubali kuwa ameshindwa katika vita alivyoanzisha Ukraine.

Mashaka ya Ukraine

Wakati Kyiv bado ikisubiri ushiriki wa Marekani, kwa siri maafisa wengi wa Ukraine wana shaka kwamba Marekani chini ya utawala wa Donald Trump itachukua muda kumaliza vita hivyo, huku Ukraine ikitaka kutolewa kwa dhamana ya kuhakikisha hawatashambuliwa tena na Urusi.

Mark Cancian, mshauri katika Kituo cha Center for Strategic and International Studies, anasema kuwa,

"Ni vigumu kufikiria aina ya dhamana za usalama ambazo Waukraine wataona zinaaminika vya kutosha kusaini makubaliano ya amani, na ambazo Urusi, Marekani na Ulaya wote watakubaliana nazo."