Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Alhamisi: Man Utd yamtupia jicho Summerville
Winga wa West Ham Crysencio Summerville, anawindwa na Manchester United. Arsenal wanajiandaa kuwasilisha ofa kwa winga wa Norway, Antonio Nusa, huku Everton wakifikiria kumsajili Rico Lewis wa Manchester City.
Manchester United watamlenga winga wa West Ham Crysencio Summerville, mwenye umri wa miaka 24, iwapo Marcus Rashford ataondoka msimu huu wa kiangazi. Mshambuliaji huyo wa Uholanzi anakadiriwa kugharimu takriban pauni milioni 30. (Guardian - subscription required)
Arsenal wanajiandaa kuwasilisha ofa ya takribani pauni milioni 34 kwa winga wa Norway mwenye umri wa miaka 21, Antonio Nusa, kutoka RB Leipzig. (CaughtOffside)
Manchester City wamefahamisha Lille kwamba wanataka kumleta kiungo wa Morocco mwenye umri wa miaka 18, Ayyoub Bouaddi, moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza badala ya kumrudisha kwa mkopo katika klabu hiyo ya Ufaransa. (TeamTalk)
Manchester City wanamfuatilia mshambuliaji wa Senegal mwenye umri wa miaka 18, Ibrahim Mbaye, wa Paris Saint-Germain, huku Aston Villa na Tottenham pia wakimwania. (FootMercato)
Sunderland wanajiandaa kuwasilisha ofa ya kumsajili beki wa Ufaransa,19, Dayann Methalie, kutoka Toulouse. (Football Insider)
Everton wanafikiria kumsajili beki wa kulia wa Manchester City, Rico Lewis, huku Nottingham Forest, Bournemouth na Fulham pia zikimwania Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 21. (TeamTalk)
Hull City wanatarajiwa kukamilisha usajili wa winga wa Sweden mwenye umri wa miaka 24, Elliot Stroud, kutoka Mjallby katika dili la pauni milioni 3 wiki hii. Pia wana matumaini ya kukamilisha usajili wa kipa wa Olympiacos na timu ya taifa ya Ugiriki, Konstantinos Tzolakis, mwenye umri wa miaka 23. (Sky Sports)