Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, hali ikoje katika ligi tano bora za Ulaya msimu unapokaribia kuisha?
Tumefika hatua ya mwisho ya ligi tano bora za Ulaya, ambapo ushindani unazidi kuwa mkali na timu zinapigana kwa matumaini ya kupata matokeo mazuri kabla ya mwisho wa msimu.
Mwezi wa tano mashabiki watashuhudia mechi zikichezwa siku moja na kwa wakati mmoja, huku wakisubiri matokeo kwa hamu hadi dakika ya mwisho.
Kama kawaida, baadhi ya timu zinaweza zisiridhike kwa kushinda pointi tatu pekee ili kufikia lengo lao, lakini lazima zisubiri timu zilizo karibu nazo kwenye msimamo zijikwae.
Mashindano ya wiki za mwisho huwa yanahusu kupata nafasi ya kwanza na kushinda taji, au kufikia nafasi ambayo inachangia ushiriki wa Ligi ya Mabingwa au mashindano mengine ya Uropa, na muhimu zaidi, mashindano ya kukwepa kushushwa daraja na kubaki Ligi Kuu.
Kwa hiyo, mechi za mwisho katika kila ligi kati ya tano bora zitakuwa ngumu na zenye changamoto kwa klabu zote zinazoshindana, bila kujali kiwango cha wachezaji wao.
Majeraha ya wachezaji wakati huu muhimu huwakilisha changamoto kubwa kwa makocha na huenda yakaathiri utendaji wa timu au kiwango chake huku shinikizo na ushindani unavyoongezeka.
Wiki hii kumeshuhudiwa uthibitisho wa baadhi ya timu za Ligi Kuu kushuka daraja na maajabu ambayo yanaweza kuwa mabadiliko katika mbio za ubingwa nchini Uhispania, kwa mfano, na huko England.
Manchester City ilirejea kileleni wiki hii kutoka kwa Arsenal baada ya utawala wa muda mrefu wa Arsenal kwenye kilele.
Wakati huo huo, Barcelona walidumisha uongozi wao, pointi tisa mbele ya mahasimu wao Real Madrid. Bayern Munich walitwaa ubingwa wikendi hii .
Vipi kuhusu ligi za Ufaransa na Italia? Na je, ni hesabu zipi kwa timu zilizo katika hatua ya mwisho ya ligi tano bora za Ulaya?
Arsenal na laana ya mwisho wa ligi
Arsenal waliongoza jedwali la Premier League kwa siku 206 msimu huu na kupigiwa upato kushinda taji hilo.
Lakini laana ya mwisho ya mbio hizo imeibuka tena, na Arsenal walipoteza pointi muhimu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini hali yao ilizidi kuwa mbaya baada ya matokeo mabaya Februari na Aprili, ambayo ya mwisho ni kupoteza kwa mpinzani wao wa karibu, Manchester City, katikati ya wiki iliyopita.
Manchester City walichukua fursa ya kujikwaa kwa Arsenal zaidi ya mara moja, kupitia mechi kati yao na baadaye ushindi wao dhidi ya Burnley katikati ya juma, ilifanikiwa kuipita Arsenal na kuongoza orodha kwa tofauti ya mabao na idadi sawa ya pointi.
Huku mizunguko mitano ikisalia katika Ligi Kuu ya Uingereza, vita vya kuwania nafasi ya kwanza vinakaribia kuamuliwa kati ya Manchester City na Arsenal kulingana na jumla ya pointi zao baada ya Arsenal kuilaza Newcastle wakati City wakifuzu fainali ya FA kwa kuilaza Southampton.
- Arsenal 73 points
- Manchester City 70 points
- Manchester United 61 points
- Aston Villa 58 points
Liverpool (pointi 58) na Brighton (pointi 50) wote wanajaribu kupata angalau nafasi ya nne ili kujihakikishia kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Wolverhampton, aliyemaliza wa mwisho, na Burnley, aliyemaliza wa pili huko mwisho, wote watashushwa Daraja la Kwanza.
Tottenham Hotspurs wa kihistoria wanajitahidi kuepuka kuteremka Ligi ya Daraja la Kwanza, mradi watapata matokeo mazuri katika raundi zilizosalia.
Mara ya mwisho Tottenham kucheza nje ya Premier League ni pale iliposhuka daraja msimu wa 1977/1978 kwa mwaka mmoja pekee.
Kando na Tottenham, Nottingham Forest na West Ham United pia wanakabiliwa na hatari ya kushuka daraja kutoka kwa Ligi Kuu ya Uingereza.
La Liga: Je, El Clasico itaamua ubingwa kwenda Barcelona?
Upinzani kati ya wapinzani wawili wa kimataifa wa El Clasico, Barcelona na Real Madrid, ulikuwa mkali na wa karibu katika msimu huu wote. Wawili hao walibadilishana nafasi ya juu zaidi ya mara moja.
Licha ya ushindi wa Real Madrid dhidi ya wapinzani wao wa jadi katika mkondo wa kwanza, Barcelona walifanikiwa kupata matokeo chanya zaidi katika kipindi kilichosalia cha msimu huu.
Real Madrid waliteseka baada ya kupata matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya Uhispania na kutimuliwa kwa kocha wao Xabi Alonso katikati ya msimu, na kuchukuliwa nafasi yake na Arbeloa.
Barcelona hawajapoteza au kupata sare katika mechi yoyote tangu Februari 16, walipofungwa 2-1 na Girona. Hii imewawezesha kutumia vyema fursa yao dhidi ya Real Madrid walio katika nafasi ya pili na kuendeleza uongozi wao hadi pointi kumi na moja.
Ikiwa pengo litaendelea kuwa kama lilivyo hadi mechi ya El Clasico kati yao huko Barcelona Mei 10, Real Madrid itakabiliwa na changamoto kubwa, kwa sababu kupoteza au sare katika mechi hii kutaipa klabu hiyo ya Catalunya ubingwa wa ligi kwa raundi tatu kabla ya msimu kumalizika.
Huku mechi ya Clasico ikikaribia, tofauti ya pointi itaweka shinikizo kwa Real Madrid. Utelezi wowote unaweza kuipa Barcelona ubingwa kabla ya mahasimu hao wawili kukutana kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Timu zote mbili zinakabiliwa na majeraha ya wachezaji muhimu, na hivi majuzi Real Madrid ilithibitisha kuwa kiungo Arda Guler na beki wa kati Eder Militao watakuwa nje kwa muda wote uliosalia wa michuano hiyo.
Barcelona walithibitisha kuwa watamkosa nyota wao anayechipukia Lamine Yamal kwa mechi zilizosalia za La Liga, huku nyota wao Mbrazil Rafinha akiendelea kuwa nje kutokana na jeraha.
Wapinzani wa karibu wa Barcelona na Madrid ni Villarreal katika nafasi ya tatu na Atletico Madrid nafasi ya nne.
Huku raundi tano zikiwa zimesalia kwenye ubingwa msimu huu, msimamo wa timu zilizo kileleni ni kama ifuatavyo.
- Barcelona 85 points
- Real Madrid 74 points
- Villarreal 65 points
- Atletico Madrid 60 points
Hatima ya timu yoyote kuhusu kusalia au kushushwa daraja kutoka Ligi Kuu ya Uhispania bado haijaamuliwa.
Angalau vilabu saba vya Uhispania vilivyo katika nafasi za chini zinakabiliwa na hatari ya kushushwa Daraja la Kwanza, zikiwemo Real Oviedo, Levante na Sevilla.
Ushindani utakuwa mkali kati ya vilabu hivi, ambavyo jumla ya pointi zao ziko karibu sana (Oviedo, katika nafasi ya mwisho, ya 20, ana pointi 28, na Mallorca, katika nafasi ya 15, ana pointi 35), na uwezekano wote unabaki wazi na pointi 18 zimesalia katika mechi sita zilizopita.
Bundesliga: Hakuna maajabu nchini Ujerumani msimu huu
Bayern Munich walitawala nafasi ya kwanza katika Ligi ya Ujerumani Bundesliga katika msimu huu wote, wakiongozwa na meneja Vincent Kompany na nyota Harry Kane, Luis Diaz na Michael Ulise.
Timu ya Bavaria imepoteza mechi moja pekee hadi sasa. Timu nyingine, kama vile wapinzani wao wa jadi Borussia Dortmund au Bayer Leverkusen, ambao walishinda taji hilo msimu wa 2023/2024, bado hawajaonyesha kiwango cha kuwania nafasi ya kwanza.
Bayern Munich ilikutana na Mainz Jumamosi, Aprili 25, katika mechi ambayo timu hiyo ya bavaria ilitoka nyuma na kuilaza Manz kwa mabao 4-3 ugenini na hivyobasi kutawazwa mabingwa
Borussia Dortmund wako katika nafasi ya pili, pointi 15 nyuma, huku kukiwa na michezo minne iliyosalia msimu huu.
- Bayern Munich pointi 82
- Borussia Dortmund pointi 67
- Leipzig pointi 62
- Stuttgart pointi 57
Hoffenheim, katika nafasi ya tano (pointi 57), na Bayer Leverkusen, katika nafasi ya sita (pointi 55), wote wanachuana kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa.
Kushuka daraja kwa Heidenheim kutoka Bundesliga sasa kunakaribia kwa kuwa wanashika nafasi ya mwisho wakiwa na pointi 19.
Eneo la hatari linapanuka na kujumuisha timu nyingine 7, ambazo pointi zao pia zinakaribiana sana.
Vilabu hivi ni pamoja na Borussia Mönchengladbach, Werder Bremen, Wolfsburg na Hamburg.
Imeelezwa kuwa idadi ya timu zinazoshindana nchini Ujerumani ni 18, sawa na ilivyo nchini Ufaransa, tofauti na Uhispania, Uingereza na Italia ambapo idadi ya timu zinazoshiriki michuano hiyo ni 20.
Ufaransa: Lens inaikimbiza Paris Saint-Germain
Paris Saint-Germain, mabingwa wa ligi ya Ufaransa na washindi wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, hawakuweza kupata taji hilo mapema mwaka huu.
Timu ya Parisian iko pointi nne pekee mbele ya Lens iliyo nafasi ya pili, huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 29.
Paris Saint-Germain wamepoteza mara tano msimu huu, majuzi zaidi dhidi ya Lyon wiki iliyopita kwa mabao 2-1, na wametoka sare mara tatu.
Paris Saint-Germain haina mpinzani wa nafasi ya kwanza isipokuwa Lens iliyoshika nafasi ya pili, kwani timu zilizoshika nafasi ya tatu na nne ziko nyuma sana kuweza kukamata timu zilizoshika nafasi ya kwanza na ya pili hadi mwisho wa mbio hizo.
Vilabu vingi vimecheza mechi 30 hadi wiki hii, na tumefikia mechi nne za mwisho za mashindano.
- Paris Saint-Germain pointi 69 (imecheza mechi 29)
- Lens pointi 63 (ilicheza michezo 29)
- Lyon pointi 57
- Lille pointi 57
Marseille, mpinzani wa jadi wa Paris Saint-Germain, anatazamia kuboresha nafasi yake kutoka nafasi ya sita. Kwa sasa ina pointi 53, mbele ya Reims katika nafasi ya tano na pointi 56.
Timu iliyo katika nafasi ya mwisho, Metz, ndiyo sasa inakaribia kushushwa daraja la kwanza, ikiwa na pointi 15 pekee.
Nantes wanawatangulia katika nafasi ya kumi na saba wakiwa na alama 20. Ni moja ya vilabu vya kifahari vya Ufaransa na vilikuwa na ushindani miaka ya nyuma, hivyo kushuka kwao daraja kunaweza kuwashtua mashabiki wao nchini Ufaransa.
Auxerre atajaribu kukwepa kushuka daraja na kuondoka nafasi ya 16 akiwa na pointi 25 hadi nafasi ambazo zingewawezesha kusalia Ligi Kuu, ikitanguliwa na Nice, ambayo ina pointi 29 katika nafasi ya 15.
Serie A: Inter Milan wanamiliki nafasi ya kwanza, vita vikali vya kuwania nafasi ya pili
Inter Milan wanakaribia kurejesha taji la Serie A msimu huu baada ya Napoli kushinda taji hilo mwaka jana.
Inter Milan wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 10 dhidi ya wapinzani wao AC Milan, jambo ambalo linawafanya wabaki na pointi nne kutwaa rasmi taji la ligi hiyo zikiwa zimesalia mechi tano.
Lakini nafasi ya pili bado haijaamuliwa kwa upande wa Milan, kutokana na jumla ya pointi kati yao, Napoli na Juventus.
- Inter Milan pointi 79
- Milan pointi 69
- Napoli 67
- Juventus pointi 64
Hatima ya Verona na Pisa inakaribia kufungwa, kwani wako katika nafasi mbili za mwisho wakiwa na alama 18, alama kumi nyuma ya Lecce walio nambari 18 na alama 28.